Tetesi 5 kubwa za soka jioni hii: Saliba kuziba nafasi ya Rudiger Madrid?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 2

Real Madrid ama Los Blancos wanatafuta beki mpya wa kati wa kiwango cha juu cha kimataifa ili kujenga safu ya ulinzi, William Saliba akitajwa kufaa zaidi (Goal)

Kuna minong'ono kwamba mikataba inaweza kufutwa, na kuna wengine wataondolewa hasa nafasi ya ulinzi ambapo, timu hiyo imekuwa ikifanya vibaya msimu huu. Mmoja wa mabeki walio katika orodha ya kufungashiwa virago ni beki wa kati, Mjerumani Antonio Rudiger.

Saliba amekuwa kwenye kiwango bora na kuwa mmoja wa mabeki bora katika ligi kuu ya England, katika misimu mitatu mfululizo

Mfaransa huyo bado ana mkataba na arsenal, lakini uwepo wa dhana ya wafaransa kupenda kucheza Madrid, na uwepo wa rafiki yake Kylian Mbappe huenda kukamshawishi kuachana na the Gunners na kujiunga na Madrid.

Liverpool yapata mbadala wa Alexander - Arnold

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Liverpool imeanza mazungumzo na mlinzi wa Freinburg, Kilian Sildillia ili kuziba nafasi ya mlinzi wake, muingereza Trent Alexander Arnold, anayetimkia Real Madrid.

Arnold amesalia na miezi miwili tu kumaliza mkataba wake Anfield, na ameonyesha wazi kwamba hataongeza mkataba huo ili kutimkia Madrid.

Kocha Arne Slot, anayekaribia kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu, ameanza kusaka mbadala wake na yuko tayari kumnunua mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 22 (Teamtalk)

Barcelona wanapanga kuzungumza tena Nico Williams anasakwa na Arsenal

,

Chanzo cha picha, Getty Images

Barcelona wanatarajiwa kupeleka ofa Athletic Club kwa ajili ya kumnasa winga Nico Williams, wakati huu wakijiandaa kuingia kwenye mazungumzo na nyota huyo.

Klabu hiyo ya Catalan ilijaribu kumsajili winga huyo msimu uliopita wa joto kufuatia kiwango chake bora alichokionyesha kwenye michuano ya Euro 2024 mwaka jana, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 aliamua kusalia katika timu hiyo ya Basque kwa angalau mwaka mmoja zaidi.

Barca, hata hivyo, hawajakata tamaa kumnasa huku Sport wakiripoti kuwa wako tayari kuanzisha mazungumzo juu ya uhamisho wa majira ya kiangazi. (Goal)

Gavi kuzeekea Barcelona

a

Chanzo cha picha, Getty Images

Wakati huo huo nyota wa Barcelona, Gavi akizungumzia kuhusu mustakabali wake Barcelona anasema "nataka kuzeekea Barca, katika mpira hujui kitakachotokea kesho, lakini niko tayari"

ni kweli kwenye mpira mengi yanaweza kutokea, ikiwemo kupata majeraha, lakini kwa hakina nitasaini kusalia Barca', alisema leo (Romano).

"Victor Osimhen anataka kuja Chelsea"

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Kiungo wa zamani wa Chelsea John Obi Mikel ameweka wazi tena kuwa Victor Osimhen anataka kujiunga na The Blues.

Victor Osimhen anasakwa na Chelsea, wakati ambao kocha wake Enzo Maresca ametengewa kiasi cha £58m kwa ajili ya mshambuliaji huyo.

"Sikiliza, itakuwa jambo la kusikitisha sana ikiwa hatutampata mchezaji ambaye alitushabikia na kutuunga mkono tangu akiwa mtoto na anataka kuchezea Klabu hii ya Soka," alisema kwenye The Obi One Podcast.

"Anampenda Drogba, atataka kuvunja rekodi, kutupa vikombe, kuturudisha kileleni", anasema Obi (Football London)