Je, teknolojia inaweza kuufanya ubongo ufanye kazi vizuri zaidi?

Imagem de um cérebro humano suspenso sobre um fundo claro com eletrodos coloridos

Chanzo cha picha, Getty Images

    • Author, "CrowdScience" Program
  • Muda wa kusoma: Dakika 4

Je, una orodha ndefu ya manunuzi unayohitaji kukumbuka? Au majina ya wageni wa mkutano muhimu?

Kuna mbinu za kumbukumbu tunazotumia kufundisha ubongo ili ufanye kazi vizuri zaidi. Hii ni njia inayojulikana kama "programu" ya kuimarisha uwezo wa akili.

Lakini je, tunaweza pia kutumia "hardware," yaani, vifaa vinavyotoa ishara za umeme kwenye ubongo?

Hadi sasa, teknolojia hii imetengenezwa kusaidia kurejesha kazi za ubongo kwa wagonjwa wa baadhi ya neva.

Mfano mmoja ni kuchochea ubongo kwa kina (DBS), mbinu ngumu iliyotumika kwa miaka mingi kutibu watu wenye magonjwa Parkinson.

'Pacemaker' ya ubongo

Profesa Francesca Morgante kutoka Chuo Kikuu cha City St George, London, amebaini athari za DBS kwa wagonjwa wake.

"Ikiwa inaangaliwa kwa wale ambao dawa zao haziwezi kudhibiti dalili zao," alisema profesa huyo katika programu ya redio ya BBC World Service, CrowdScience.

DBS inahusisha upasuaji wa kuingiza waya kwenye ubongo. Ugonjwa wa Parkinson huuwa seli zinazotengeneza kemikali ya dopamine.

Dopamine ni muhimu kwa ishara katika sehemu za ubongo zinazodhibiti mwendo wa mwili. Bila dopamine ya kutosha, wagonjwa wanaweza kupata dalili kama kutetemeka na kufifia kwa misuli. Ugonjwa huu unazidi kuwa mbaya kwa muda, na hadi sasa hakuna tiba ya kudumu.

DBS inahusisha upasuaji wa kuingiza 'jenereta' chini ya ngozi, karibu na koo. Vimeunganishwa na waya maalumu zinazowekwa kwenye sehemu zilizoharibika za ubongo ili kuzichochea kasi ndogo ya umeme.

Profesa Morgante anasema kifaa hiki hufanya kazi kama pacemaker ya ubongo, kusaidia kurejesha ishara za kawaida za ubongo.

Profissional de assistência médica inclina-se sobre um paciente deitado na cama de um hospital, preparando-se para uma cirurgia do cérebro

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kuchochea ubongo kunahusisha upasuaji wa kuingiza nyaya ndani ya ubongo, zinazounganishwa na mifumo ya umeme wa ubongo

Hakuna suluhisho moja kwa wote

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kuchochea ubongo kwa kina kunaweza kusaidia kupunguza baadhi ya dalili za ugonjwa wa kutetemeka au Parkinson, lakini si kila wakati kunakuwa na matokeo chanya. Njia za mitandao mikubwa ya mishipa ya fahamu 'neva' zinazoelezea ishara za umeme wa ubongo ni ngumu na hazijafahamika kikamilifu.

"Kuna dalili nyingi zaidi kuliko kutetemeka na matatizo ya mwendo," anaeleza Lucia Ricciard, pia kutoka Chuo Kikuu cha City St George, London.

"Kati ya hizo ni pamoja na msongo wa mawazo, wasiwasi, kukosa ari, matatizo ya kumbukumbu, na shida ya kulala."

Utafiti unaonyesha DBS inaweza kusaidia kupunguza baadhi ya dalili hizi, kama msongo wa mawazo na wasiwasi, lakini utafiti zaidi bado unahitajika.

Kila ubongo ni wa kipekee, na hakuna suluhisho moja linalofaa kwa kila mtu. Waya zilizowekwa katika DBS zina vipande kadhaa vinavyounganishwa na neva tofauti. Wataalamu lazima wafahamu ni vipande vipi vinavyostahili kuchochewa ili kupata matokeo bora.

Ilustração da saúde da substância negra de dois cérebros

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Picha inayoonyesha seli za ubongo. Kushoto ni seli zilizoharibika za mgonjwa wa Parkinson (rangi ya chungwa), kulia seli za ubongo ambazo hazijaathirika.

Kuweka kumbukumbu sawa na zamani

Haijulikani bado kama kuchochea ubongo kunaweza kuboresha kazi nyingine za ubongo, kama kumbukumbu, lakini jambo hili linaendelea kufanyiwa utafiti.

Kumbukumbu za binadamu zinakusanyika kwenye eneo la ubongo linaloitwa hippocampus, ambalo linapokea taarifa kutoka sehemu nyingine za ubongo na kuzihifadhi muda mfupi au mrefu.

Miaka kadhaa iliyopita, timu ya Profesa Robert Hampson kutoka Chuo Kikuu cha Wake Forest, Marekani, ilifanya majaribio kupitia panya, ikitumia kazi za kumbukumbu na kuona mifumo ya umeme inayoibuka kabla ya panya kufanya uamuzi.

Timu yake iligundua kuna mifumo inayohusiana na kazi sahihi ya kumbukumbu na makosa yake, na kuanza kujiuliza kama inawezekana kuathiri mifumo hii na "kurekebisha kumbukumbu inaposhindwa."

Rato de laboratório

Chanzo cha picha, Fotografixx via Getty Images

Maelezo ya picha, Utafiti ulifanywa kwa panya kuchunguza mizunguko ya kumbukumbu ya ubongo kupitia maabara

Majaribio ya teknolojia kwa kibinadamu

Hampson alianza majaribio ya kwanza kwa binadamu ya kifaa kinachoitwa hippocampal neural prosthesis.

Kama DBS, inahitaji upasuaji wa kuweka waya kadhaa, zinazolengwa kwenye hippocampus. Teknolojia hii bado haijakamilika. Kwa sasa, badala ya kuingiza pacemaker ndani ya binadamu, waya zinaunganishwa kwenye kompyuta kubwa ya nje, inayoweza kutuma na kupokea ishara kutoka ubongo.

Katika majaribio kwa wagonjwa wenye kifafa, matokeo yameonyesha dalili nzuri: Wagonjwa waliopata matatizo makubwa ya kumbukumbu walionyesha kuboresha 25%–35% ya uwezo wao wa kuhifadhi taarifa kwa muda wa saa 1 hadi 24.

Neurologista de costas para a câmera, observando imagens do cérebro em uma tela grande à sua frente

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Estão sendo atualmente testados ou empregados diferentes métodos de estimulação cerebral em uma série de condições neurológicas, como a depressão e a epilepsia

Matarajio ya baadaye

Profesa Hampson anaamini teknolojia hii siku moja inaweza kusaidia watu wenye matatizo ya kumbukumbu kama ugonjwa wa Alzheimer's.

Lakini je, inaweza kuboresha ubongo wa mtu yeyote, siyo tu wagonjwa wa magonjwa ya ufahamu?

"Hadi sasa hatujui sababu za baadhi ya watu kuwa na kumbukumbu bora kuliko wengine," anasema.

Na bila shaka, kuna masuala ya kimaadili kuzingatiwa, pamoja na hatari zinazohusiana na upasuaji wa ubongo.

"Kumbukumbu ni kiini kinachotufanya tuwe tulivyo, na kile tunachotaka ni kutoibadilisha," Hampson anahitimisha.