Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
‘’Wanaume hutoa mimba za watoto ambao tayari wamezaliwa’’
‘’Sikujui wewe, sijui asili yako, macho yako, urefu wako, uzito wako, mikono yako, sauti yako. Sijui chochote kukuhusu wewe. Na bado ni wewe.’’
Muda mfupi baada ya siku yake ya kuzaliwa kuadhimisha miaka 40, mwandishi kutoka Mexico Alma Delia Murillo alianza kumtafuta baba yake ambaye aliamini kuwa amekufa kwa miongo kadhaa.
Na kuanza kuangazia maisha yake.
Anasimulia safari yake, iliyojaa picha za kila aina.
Murillo alikuwa na umri wa miaka 7 baba yake alipotoweka.
‘’Alikwenda kutafuta sigara na hakurudi tena’’.
Utoto wake ulibainishwa na huko kutelekezwa, umaskini na njaa.
‘’Kukua na ndugu saba ndio jambo la kuchekesha zaidi’’, anasema akiwa na tabasamu lake kubwa.
Yeye pia ni mwandishi wa riwaya 4, alifanya kazi kwa miongo miwili katika mashirika hadi alipojipa ujasiri na kuachana na ‘’mfadhaiko huo,’’ na kujitolea kwa shauku yake katika fasihi.
BBC Mundo ilipata fursa ya kuzungumza naye.
Katika maisha, kiuhalisia jinsi mwanamume anavyochukuliwa wakati amemtekeleza mtoto wake ni tofauti sana na wanaume.
Utakuta utoaji mimba umepigwa marufuku katika nchi nyingi lakini hautawahi kuona watu wanafanya maandamano dhidu ya wanaume wanaotelekeza Watoto wao.
Kwa miaka mingi unaamini kwamba baba yako amekufa, na unapogundua kwa bahati kwamba sivyo, unaandika kwamba ‘’inastahili zaidi kuwa na baba aliyekufa kuliko baba ambaye hakupendi’’.
Je, unafikiri familia za mzazi mmoja bado ni unyanyapaa?
Ndiyo bila shaka.
Hii inaanzia na takwimu hadi kusimulia yanayojiri, hadi hadithi za kuumiza moyo.
Kwa takwimu mtu anaweza kujificha katikati ya namba, lakini unapozungumzia hili pengine wakati wa mkutano, wa kula chakula Pamoja na kadhalika, kutokuwepo kwa baba kwa sababu alikutelekeza kunaweza kuwa aibu.
Kushirikisha hilo na kulifanya kuwa sehemu ya utambulisho wetu kwa umma bado ni vigumu, na ingawa watu wengi hawapendi, nitasema: inahusiana na suala la mfumo dume ambapo hisia hizi haziwekwi kwenye mazungumzo ya umma.
Sisi wanawake tuko tayari zaidi kufanya hivyo kuliko wanaume.
Inashangaza kwamba wakati unamtafuta baba yako, kwa njia fulani pia unampata mama yako.
Ni kitendawili kizuri sana.
Mama yangu alinipa zawadi kubwa.
Alinipa uhuru.
Alipokuwa anatoka nyumbani, aliniuliza ‘’utaondoka’’.
Alinipa nafasi ya kuondoka ninapotaka.
Alinipa nguvu ya kuishi bila kufikiria yanayojiri.
Na mimi, kama watu wengine, nina deni kubwa kwa mama yangu.
Niliweza kusoma chuo kikuu kwa sababu alifanya kazi ya nyumba, na kila nikielezea hili hadharani au kuandika, haujui idadi ya watu wanaoniambia kwamba wana historia saw ani hiyo na wala sio aibu kulizungumzia.
Alikuwa mkarimu sana.
Pia alinipa furaha yake, ambayo bado inaonekana haielezeki kwangu.
Katika kila jambo alilopitia, kifo cha mtoto wake wa kwanza, tukio la mmoja wa dada zangu kuchomeka, madharau aliyopitia, siku zote alikuwa mwanamke mwenye furaha.
Ndio maana mwisho najaribu kumrudishia asante kwa kumpa uwezo ambao hakuwa nao maana alikaa kwa miaka 20 tangu aliponizaa na kulea akihangaika, na mimi leo namwambia ‘uko huru nenda utakako’ sio tu uwe mama, lakini pia uwe mwanamke.
Mama pia anaweza kuwa mwanamke katika upendo.
Nadhani mama yangu alikuwa na homa ya kutaka kupata upendo .
ngono.
Nikiwa mtoto nilikasirishwa na jambo hilo, lakini sasa nasema, jinsi alivyoishi vizuri na jinsi alivyoweza kuwa shahidi wa hili.
Wacha tuzungumze juu ya safari ya kumtafuta baba yangu.
Au tuseme kusafiri, kwa sababu safari iko katika ngazi kadhaa ...
Ndiyo, kwa kweli ni mfululizo wa safari.
Sio tu safari ya barabarani nikimtafuta baba ambaye sikuwa nimemwona kwa miaka 40, bali pia safari ambayo asili yake inasimuliwa, unatoka wapi na wewe ni nani.
Na wakati wewe ni kama mimi, mwanamke ambaye alikulia katika eneo la pembezoni, katika nchi ya Amerika Kusini, mwenye nywele nyeusi, vizuri, una hadithi ya kusema ambayo itahusisha tabaka, vurugu, unyanyasaji wa kijinsia na kadhalika, au sio?.
Lakini kwasababu mimi ni mwandishi, wanaposema eti nimeandika juu ya uana harakati, hilo linanifanya nitabasamu, kwasababu kwangu mimi, ni suala la kuketi na kusimulia uzoefu wako.
Safari hii pia ina kumbukumbu zake kijamii.
Kuna takwimu za kutisha, ambazo zinasema kwamba kwa vizazi vitatu vijavyo watu wanabaki katika hali sawa ya kijamii na kiuchumi, kiwango cha mapato sawa na wazazi wao.
Mbali na unyanyasaji wa wazi zaidi ambao wewe mwenyewe uliteseka, kuna mwingine wa kila siku zaidi, ‘kuishi kwa upweke’
Hakuwezi kuwa na shaka kwamba kuna maendeleo katika masuala ya jinsia, lakini pia huwezi kupinga ukweli wa kuwa mazungumzo yanaendelea haraka kuliko vitendo.
Ukweli wa mambo
Ukiwa una kazi kama yangu, kwa mfano, yenye kusababisha wasiwasi mwingi,ambayo ninahitaji kuwa peke yangu wakati ninaandika, nataka ukimya na upweke, lakini watu wamekuwa wakinihukumu sana, huyu ni mbinafsi na kadhalika.
Lakini ninahitaji kipindi hicho.
Nimejaribu kuishi katika ndoa na sijafanikiwa.
Hata hivyo, wakati hili la kutelekeza watoto linaendelea, kingine kinachojitokeza ni visa vya wanawake kuuawa.
Mwishowe, hitimisho ni kwamba wanaume wanaua kwa sababu wanaweza, kwa sababu wanajua kuwa hakuna kitakachotokea kwao, kwa sababu waendesha mashtaka hawafuatilii kesi.
Kwa sababu hata waliokiri kutekeleza mauaji ya wanawake huachiliwa na kuwa huru.
Sasa tunakabiliwa na jambo la kutisha kwa kuwa katika nchi kama vile Mexico kumekuwa na tabia ya kuchoma wanawake wakiwa hai au kwa asidi.
Kwa hivyo nadhani kwamba, bila shaka, tunaweza kuingia katika mada laini zaidi na kujadili kama elimu, kuruhusu, jambo la kitamaduni, lakini napenda kuwauliza wanaume, kugeuka na kuwaambia, "hey, si lazima pia kuwa. kujiuliza kwanini wanafanya hivyo, kwanini wanaweza, kwanini sheria hazifanyi kazi?Ndio, impunity inabidi ivurugike kwa masharti ya kisheria, kimahakama, kwenye ofisi za waendesha mashitaka, lakini wanaume nao wanapaswa kuvurugwa.Nadhani huo ndio moyo wa hiyo.
Bila shaka baada ya simulizi hii, kuna mengi ambayo bado yanahitajika kufanywa katika jamii ili kurekebisha hali halisia na kufanya dunia mahala salama na pa furaha kuishi kwa kila mmoja wetu.