Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mchoro wa Ramani ulivyosaidia kukutanisha familia China
Mwanamume mmoja wa China ambaye alitekwa nyara kwa zaidi ya miaka 30 iliyopita ameunganishwa tena na mama yake mzazi baada ya kuchora ramani ya kijiji chake cha utotoni kupitia kumbukumbu zake.
Li Jingwei alikuwa na umri wa miaka minne tu aliposhawishiwa kutoka nyumbani kwao na kuuzwa katika kituo cha kusafirisha watoto kinyume cha sheria.
Tarehe 24 Desemba alionesha ramani iliyochorwa kwa mkono katika programu ya video, Douyin, ambayo polisi walilinganisha na kijiji kidogo na mwanamke ambaye mtoto wake wa kiume alitoweka.
Baada ya vipimo vya DNA, waliukutanishwa tena katika kitongoji cha Yunnan siku ya Jumamosi.
Pcha za video za kuungana kwao zinawaonyesha wawili hao wanakutana kwa mara ya kwanza baada ya miongo mitatu huku Li Jingwei akiondoa kwa uangalifu barakoa ya mamake ya kujikinga na virusi vya corona ili kumuangalia vizuri kabla ya kuangua kilio na kumkumbatia.
"Miaka thelathini na tatu ya kungoja, usiku mwingi wa kutamani, na hatimaye ramani iliyochorwa kwa mkono kutokana na kumbukumbu, huu ni wakati mahususi wa kuachiwa baada ya siku 13," Bw Li aliandika kwenye ukurasa wake wa Douyin kabla ya kukutana kwao kulikokuwa kukitarajiwa."Asante, kila mtu ambaye amenisaidia kuungana na familia yangu."
Bw Li alitekwa karibu na mji wa kusini-magharibi wa Zhaotong katika kitongoji cha Yunnan mwaka wa 1989 na baadaye akauzwa kwa familia iliyokuwa ikiishi umbali wa zaidi ya kilomita 1,800.
Sasa anaishi Guangdong kusini mwa Uchina, hakufanikiwa kuwauliza wazazi walezi waliomu asili au kutafuta hifadhidata za DNA kuhusu asili yake. Kwa hiyo aliamua mtandao.
"Mimi ni mtoto ambaye natafuta nyumbani kwetu. Nilipelekwa Henan na jirani mwenye upara mwaka 1989, nilipokuwa na umri wa miaka minne," alisema kwenye video hiyo, ambayo imetumwa na maelfu kwenye mtandao.
"Hii ni ramani ya eneo la nyumbani kwangu ambayo nimeichora kutokana na kumbukumbu zangu," alisema akiinua ramani hiyo ya kijiji iliyochorwa hovyo, ambapo kulikuwa na vitu kama vile jengo ambalo aliamini kuwa ni shule, msitu wa mianzi na bwawa dogo.
Utekaji nyara wa watoto si jambo geni nchini China, jamii ambayo inathamini sana kupata mtoto wa kiume.
Watoto wengi hutekwa nyara wakiwa na umri mdogo na kuuzwa kwa familia nyingine. Mwaka wa 2015, ilikadiriwa kuwa watoto 20,000 hutekwa nyara kila mwaka.
Mwaka 2021 kulikuwa na mifano mingi ya vijana waliounganishwa tena na wazazi wao wa kibaolojia baada ya kutokuwa nao kwa muda mrefu.
Mwezi Julai 2021, Guo Gangtang aliunganishwa tena na mtoto wake wa kiume wa miaka 24 baada ya kutekwa nyara katika jimbo la Shandong.