B-2: Ndege ghali zaidi ya kijeshi duniani Iliyoishambulia Iran

Muda wa kusoma: Dakika 4

Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza mapema Jumapili kwamba jeshi la Marekani limefanya "shambulio lenye mafanikio makubwa" katika maeneo matatu ya vituo vya nyuklia vya Iran, ikiwa ni pamoja na kituo cha kurutubisha uranium cha Fordow.

"Tumekamilisha shambulio letu la mafanikio katika maeneo matatu ya nyuklia nchini Iran... Fordow, Natanz, na Isfahan," Trump alisema katika chapisho kwenye akaunti yake ya mtandao wa Kijamii.

"Ndege zote sasa ziko nje ya anga ya Iran. Mzigo mzima wa mabomu umerushwa kwenye eneo la, Fordow," aliongeza.

Tangazo hilo la Trump limekuja siku mbili tu baada ya kusema kuwa ataamua "ndani ya wiki mbili" ikiwa ataungana na mshirika wake Israel kuishambulia Iran.

Shambulio hilo la kushtukiza la Marekani, lililopewa jina la "Operesheni Midnight Hammer," lilitekelezwa kwa kutumia ndege saba aina ya B-2 ambazo hazikutambuliwa na walinzi wa anga wa Iran, kulingana na Washington.

Kulingana na Pentagon, haya yalikuwa mashambulizi mkubwa zaidi ya operesheni yaliofanywa na ndege za kimkakati wa B-2 katika historia ya Marekani.

Kwa mara ya kwanza, Washington ilitumia mabomu yenye nguvu zaidi ya GBU-57, ambayo yana uzito wa tani 13 na yana uwezo wa kupenya makumi ya mita kwenda chini kabla ya kulipuka.

Tehran ilikuwa imetishia mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya majeshi ya Marekani katika Mashariki ya Kati iwapo Trump angeishambulia, lakini rais huyo wa Marekani alitoa wito wa "amani."

Trump alisisitiza, "Hakuna jeshi lingine duniani linaloweza kufanya hivi. Sasa ni wakati wa amani."

Katika ripoti hii, BBC inaangazia ndege aina ya B-2 ambapo kwa mujibu wa Reuters, kila ndege ya Marekani B-2 inagharimu karibu dola bilioni 2.1, "na kuifanya ndege ya hii ya kijeshi kuwa ya gharama kubwa zaidi kuwahi kutengenezwa."

Je, ndege za B-2 zina umuhimu gani?

Jeshi la Marekani lilituma ndege aina ya B-2 kwenye kisiwa cha Guam cha Pasifiki cha Marekani kabla ya Trump kutangaza kushambulia maeneo matatu ya nyuklia ya Iran, na kuungana rasmi na Israel katika kufanya mashambulizi ya anga kwenye maeneo ya nyuklia ya Iran.

Ndege hizo zilitumwa Guam kutoka Missouri, Marekani, iliyoko takriban kilomita 9,500 mashariki mwa Fordow.

Ni vyema kutambua kwamba ndege hizi kubwa, zenye mabawa ya zaidi ya mita 50, ndizo zenye uwezo wa kubeba mabomu ya GBU-57 Massive Ordnance Penetrator (MOP), yenye kilo 13,608 na uwezo wa kupenya mahandaki, ambayo wataalamu wanasema ni muhimu kwa kuharibu kituo cha nyuklia cha Iran.

Kituo hicho kinaaminika kuwa chini ya mita 100 chini ya ardhi na kulindwa na saruji iliyoimarishwa.

Licha ya ubora wake mkubwa wa anga, Israel haina silaha zinazohitajika kuharibu kituo hicho, hatua ilioifanya kuomba msaada wa Marekani.

Haijulikani ni kwa nini Guam ilichaguliwa kuwa kituo cha ndege hizo kabla ya mashambulizi hayo.

Maafisa wa Marekani waliiambia CBS News, mshirika wa BBC wa Marekani, kwamba kituo cha Guam kinaaminika kutoa usiri bora zaidi wa utendaji kazi kuliko Diego Garcia.

Wiki iliyopita, takriban ndege 30 za kijeshi za Marekani zilihamishwa kutoka Marekani hadi Ulaya, kulingana na data ya kufuatilia safari iliyokaguliwa na BBC.

Ndege zinazohusika ni ndege za usafiri za kijeshi za Marekani, zinazotumiwa kujaza mafuta ndege za kivita na vilevile kwa mashambulizi .

Kulingana na Flightradar24, angalau saba kati ya ndege hizi, zote za KC-135, zilisimama katika kambi za ndege za Marekani nchini Uhispania, Scotland, na Uingereza.

Mienendo ya ndege hizi inakuja huku kukiwa na ripoti kwamba Marekani pia imehamisha shehena ya ndege - USS Nimitz - kutoka Bahari ya Kusini ya China kuelekea Mashariki ya Kati.

Nimitz hubeba kikosi cha ndege za kivita na inaambatana na ndege za kuharibu makombora.

Marekani pia imehamisha ndege za kivita za F-16, F-22, na F-35 katika kambi za Mashariki ya Kati, maafisa watatu wa kijeshi waliambia Reuters siku ya Jumanne.

Ndege za kujaza mafuta, ambazo zimesafirishwa hadi Ulaya katika siku chache zilizopita, zinaweza kutumika kujaza mafuta ndege za mwisho zilizosalia