Hii ndio hatari ya mafuta ya kupikia

..

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 5

Awali unene ulitazamwa kama tatizo la nchi za Magharibi pekee, lakini katika miaka ya hivi karibuni limegeuka kuwa tatizo katika nchi za kipato cha kati kama India.

Ili kukabiliana na hili, Waziri Mkuu Narendra Modi ameanzisha kampeni ya kitaifa dhidi ya unene kupita kiasi.

Katika kipindi cha redio cha "Mann Ki Baat" kilichofanyika tarehe 23 Februari, aliwahimiza watu kupunguza ulaji wa mafuta kwa asilimia 10, akisema kuwa hiyo ni hatua muhimu katika kupunguza unene.

"Kuifanya nchi kuwa yenye afya, lazima tukabiliane na unene. Uzito uliopitiliza wa mwili husababisha matatizo na magonjwa mengi," alisema Modi katika hafla hiyo.

Tafiti zinaonyesha nini?

Akiongea kwenye kipindi cha 'Mann Ki Baat' alisema, "Kulingana na utafiti mmoja kati ya watu wanane anatatizo la unene uliokithiri.

Idadi ya watu wanaosumbuliwa na unene imeongezeka maradufu katika miaka michache iliyopita."

"Unene wa kupindukia miongoni mwa watoto umeongezeka mara nne.

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani, watu wapatao bilioni 2.5 duniani kote walikuwa na uzito wa kupindukia mwaka 2022.

Hiyo, walikuwa wazito kuliko uzito unaotakiwa," alisema.

Mnamo 2024, The Lancet ilifanya utafiti. Mnamo 2022, watoto milioni 12.5 kati ya umri wa miaka 5 na 9 nchini India walikuwa na uzito kupita kiasi.

Kati ya hao, milioni 7.3 ni wavulana na milioni 5.2 ni wasichana, kutoka milioni 4 tu mwaka 1990.

Unene umekuwa tatizo linalotia wasiwasi si miongoni mwa watoto tu bali pia miongoni mwa watu wazima.

Kwa mujibu wa utafiti huo, mnamo 2022, wanawake milioni 44 na wanaume milioni 26 wenye umri wa zaidi ya miaka 20 nchini India walikuwa wanene.

Mnamo 1990, idadi hii ilikuwa wanawake milioni 2.4 na wanaume milioni 1.1.

Utafiti wa Tano wa Kitaifa kuhusu afya ya familia pia uliangazia shida ya unene nchini India.

Kulingana na ripoti hiyo, 23% ya wanaume na 24% ya wanawake katika umri wa miaka 15 hadi 49 nchini India wana tatizo la umeme uliopitiliza.

Ambapo, mwaka 2015-16, takwimu hii ilikuwa 20.6% kwa wanawake na 18.9% kwa wanaume.

Mafuta yana jukumu gani?

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Ulaji mbaya na mtindo wa maisha wa unatajwa kuwa sababu kuu za kunenepa kupita kiasi.

Hata hivyo, mara nyingi watu hupuuza ukweli kwamba mafuta tunayoongeza kwenye mlo wetu kila siku huchangia tatizo hilo.

Dk. Mahendra Narwaria, rais wa All India Society for Advanced Study and Obesity, anasema, "Chakula cha Wahindi kina wanga na mafuta mengi.

Mafuta na samli hutumiwa kufanya chakula chochote kiwe kitamu zaidi.

Kutokana na hili, miili yetu hukusanya mafuta. Kwa kuwa hatufanyi mazoezi mengi, mafuta mwilini hayayeyuki."

"Mlo wetu una wanga nyingi sana. Hizi hubadilika na kuwa mafuta zinapoingia mwilini.

Zaidi ya hayo, mafuta pia hujilimbikiza katika miili yetu. Hii huongeza hatari ya unene."

"Kiwango cha mafuta ya miili yetu huwa juu kila wakati.

Hata kama mtu ni mwembamba, mafuta ya mwili wake bado ni 30-40%, ambayo ni ya juu sana. Kwa upande mwingine, wanariadha wana 7-8% ya mafuta ya mwili."

"Ikiwa tuna mafuta mengi katika mwili wetu, uwezo wetu hupungua. Matokeo yake, uzito wa mwili wetu huongezeka."

Dk Parmeet Kaur, mtaalamu mkuu wa lishe katika taasisi ya AIIMS, Delhi, alisema, "Kutumia mafuta kuliko kiasi kinachopendekezwa kunapunguza kasi ya ufanyajikazi wa miili yetu.

Hii inasababisha kuongezeka kwa mafuta ya mwili na uzito.

Zaidi ya hayo, hutupatia kalori za ziada badala ya kutupa nyuzinyuzi, vitamini muhimu na madini."

Dk. Raman Goel, daktari wa upasuaji wa kiafya katika Hospitali ya Wockhardt huko Mumbai, alisema, "Kwa ujumla mafuta yana mafuta mengi.

Miili yetu hupata kalori zake nyingi kwenye mafuta.

Kwa kila kalori nne tunazopata kutoka kwenye protini, tunapata kalori tisa kutoka kwa mafuta.

Kwa hivyo, chochote tunachokula na kalori nyingi kinaweza kusababisha kunenepa, hasa kwa watu ambao tayari ni wanene."

Unapaswa kutumia mafuta kiasi gani?

..

Chanzo cha picha, Getty Images

Dk. Mahendra Narwaria anasema kuwa unene unaweza kudhibitiwa kwa kutumia mafuta kidogo.

Kadiri watu wanavyotumia mafuta mengi, kiasi cha mafuta mwilini huongezeka.

Dk. Parmeet Kaur alisema, "Mafuta hutusaidia kuyeyusha vitamini kama vile A, D, E, na K katika miili yetu.

Kwa hiyo, miili yetu inahitaji kiasi fulani cha mafuta."

Pia anasema, "Watu wanapaswa kutumia mafuta kulingana na umri wao.

Hata hivyo, mtu ambaye hana shughuli nzito anapaswa kutumia vijiko 4-5 tu vya mafuta kwa siku.

Hiyo ni, gramu 20-25 za mafuta kwa siku.

Hii ni nyingi kwa mtu mmoja."

Hata hivyo, mafuta sio sababu pekee ya uzito kuwa mkubwa.

Dk. Raman Goyal alisema, "Kuna sababu nyingi za kunenepa kupita kiasi. Je, unajua ni kiasi gani cha peremende kinachotumiwa nchini India? Pipi pia huongeza unene."

Nitumie mafuta gani?

...

Chanzo cha picha, Getty Images

Parmeet Kaur anasema, "Nchini India, tunapaswa kutumia mafuta ambayo yanapatikana katika mikoa yetu husika.

Kwa mfano, mafuta ya alizeti na pumba za mchele yanapatikana Kusini mwa India.

Mafuta ya karanga yanapatikana Gujarat na mafuta ya haradali katika majimbo mengine."

Anasema, hatupaswi kutumia tena mafuta yaliyotumiwa kukaangia.

Tunapaswa pia kuepuka bidhaa zilizotengenezwa kutokana na mafuta yenye haidrojeni.

Pia, ubora wa mafuta pia ni muhimu. Kupasha joto kupita kiasi mafuta yetu ya kupikia haina manufaa kwa mwili.

Mamlaka ya Usalama wa Chakula nchini India (FSSAI) inasema kwamba unapaswa kuepuka kutumia tena mafuta yaliyotumika kwa sababu yanaweza kusababisha unene uliopitiliza.

Tovuti ya Harvard School of Public Health inasema kwamba mafuta haya mabaya hayafai kwa mwili.

Hii huongeza uvimbe katika mwili, ambao unaweza kusababisha ugonjwa wa moyo, kiharusi, kisukari cha aina ya 2, na matatizo kwenye mfumo wa kinga.