Uvamizi wa ardhi ya Lebanon: Ni matukio gani yanayoweza kutokea?

h

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Vikosi vya Israel na vifaru vikipelekwa katika mpaka wa Lebanon
Muda wa kusoma: Dakika 5

Siku ya Jumatano, mkuu wa majeshi ya Israeli aliwataka wanajeshi wake kujiandaa kwa "uwezekano wa kuingia " nchini Lebanon, wakati jeshi la Israeli lilitangaza kwamba limeita vikosi viwili vya akiba kwa ajili ya "operesheni za kazi" kaskazini.

Waziri wa ulinzi wa Israel Yoav Galant awali aliahidi kuwarudisha wakazi wa kaskazini mwa Israel katika makazi yao, na kusisitiza kuwa mashambulizi ya Hezbollah yameingia katika awamu mpya huku rasilimali zaidi zikielekezwa upande wa kaskazini.

Jumatatu iliyopita, mashambulizi hayo yalifikia hatua muhimu kwa upanuzi wa wigo na kusababisha uvamizi wa Israel nchini Lebanon. Mtu yeyote anayefuatilia hali katika eneo hilo atajiuliza iwapo mzozo utaongezeka na kufikia kiwango Israel itafanya operesheni ya ardhini ndani ya Lebanon.

Je, uvamizi dhidi ya Lebanon utakuwaje iwapo utafanyika?

Katika vita vya awali nchini Lebanon, Israel ilitumia mbinu mbalimbali za operesheni zake za ardhini, kulingana na hali ya mabadiliko ya vita.

Vita vya 1982 - Uvamizi wa Ardhi ya Kina:

Katika vita vya mwaka 1982, maelfu ya wanajeshi, wakiongozana na mamia ya vifaru na magari ya kivita, walivuka mpaka kati ya Lebanon na Israel. Uvamizi huo ulikuwa mkubwa na uliambatana na mashambulizi makubwa ya anga, na majin wakati vikosi vya Israeli vilipopenya katika maeneo mengi na viliweza ndani ya wiki moja kufika viungani mwa mji mkuu, Beirut, na kuuzingira.

Uvamizi huo ulifanyika kwa makundi matatu, mawili kati ya hayo yalianza katika eneo linalojulikana kama Galilaya Finger kuelekea Bonde la Bekaa mashariki mwa Lebanon na maeneo ya milima ya kati, na eneo la tatu lilikuwa kando ya barabara ya pwani kutoka kusini hadi Beirut.

Uvamizi huo pia ulijumuisha kutua majini kwa mizinga ya kivita kaskazini mwa mji wa Sidoni.

f

Chanzo cha picha, Reuters

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Vita - Uvamizi mdogo wa ardhi:

Uvamizi wa ardhini mwaka 2006 ulikuwa mdogo na ulifanyika kwa kasi ndogo ikilinganishwa na mwaka 1982, na ulijikita katika miji ya Lebanon na maeneo ya ndani ya ukanda wa mpaka, na kwa umbali wa kilomita chache ndani ya Lebanon.

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa wa Israel Yoav Stern alifafanua, wakati wa mahojiano yake na BBC, kwamba hali ya uvamizi wa ardhini ujao utakuwa sawa na ule uliotokea mwaka 1982, lakini badala anasema kuwa utakuwa "uvamizi wa polepole, wa tahadhari na mahesabu, ikiwa ni pamoja na uvamizi wa miji kusini mwa Lebanon mmoja baada ya mwingine, badala ya kuanzisha uvamizi wa haraka na kina. Utakuwa sawa na kile kilichotokea mwaka 2006, lakini zaidi katika eneo la Lebanon, kufikia Mto Litani."

Stern alihusisha matarajio yake na ukweli kwamba Hezbollah imekuwa katika miji ya kusini mwa Lebanon kwa muda mrefu, jambo ambalo linazuia uwezekano wa kuikalia miji hii na haraka.

Katika mahojiano na BBC, Brigedia Jenerali Hisham Jaber, mkuu wa kituo cha Mashariki ya kati cha mafunzo na utafiti mjini Beirut, alisema kwamba Israel itavamia kusini mwa Lebanon na kubaki huko kwa muda mrefu. Israel ilishuhudia matokeo ya uvamizi wa ardhini mwaka 2006 na kabla ya hapo, kwa mujibu wa Brigedia Jenerali Jaber. Kwa hiyo, inawezekana kwamba aina ya uvamizi itakuwa mbali na kile kilichotokea katika 1982 au 2006.

Brigedia Jenerali Jaber anatarajia kwamba operesheni za ardhini za Israel nchini Lebanon zitapunguzwa kwa uvamizi wa mpakani katika eneo finyu sana ambalo linajumuisha maeneo machache, na kwamba kila uvamizi ambao Israeli inaweza kuufanya hautazidi siku moja kwa muda.

Brigedia Jenerali Jaber anaamini kuwa Israel itaachana na chaguo la uvamizi wa ardhini kwa kuendelea kuzidisha mashambulizi yake ya anga, kufanya mauaji, na operesheni za usalama wa mtandao.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Uvamizi wa ardhi utakuwa wapi?

Wakati wa hotuba yake Alhamisi iliyopita kufuatia mashambulizi ya mabomu ya mabomu nchini Lebanon Katibu mkuu wa Hezbollah Hassan Nasrallah, alijibu kauli ya afisa wa jeshi la Israeli kuhusu uvamizi wa Lebanon la kuanzisha ukanda wa usalama ndani ya ardhi yake, akisema kwamba kile Israel inachoona kama tisho la kuanzisha ukanda wa usalama, Hezbollah inakiona kama "fursa ya kihistoria ambayo itakuwa na athari kubwa katika vita."

Katika hotuba yake, Nasrallah alitaja ukanda wa usalama ambao Israel ilianzisha mwaka 1978 kusini mwa Lebanon, akimaanisha eneo la mpaka kati ya Lebanon na Israel.

Brigadia Jenerali Jaber, ambaye awali alisesama hapatakuwa na hali ya uvamizi wa ardhini, anatarajia kwamba operesheni za ardhini za Israeli, ikiwa zitatokea zitakuwa na mipaka ya "maeneo machache sana katika miji ya mpaka wa Lebanon," lakini hakupinga kwamba Israeli itafanya kile kinachofanana na "operesheni za haraka za makomandoo" katika maeneo mengine ya Lebanon.

Stern, kwa upande mwingine, anatarajia kutakuwa na upeo wa operesheni ya ardhini ya kujumuisha kusini mwa Lebanon, yaani, eneo kati ya mpaka wa Lebanon na Israeli na Mto Litani - lakini hakupinga uwezekano kwamba masuala ya mbinu yanaweza kuilazimisha Israeli kupenya baadhi ya maeneo ya kaskazini mwa Litani na kisha labda kupenya katika maeneo yaliyo ndani ya Lebanon ili kufanikiwa kulazimisha mazungumzo katika siku zijazo.

Malengo ya uvamizi huo yatakuwa nini?

Lengo lililotangazwa la vita vya mwaka 1982 na operesheni zake za ardhini lilikuwa ni kuihamisha miji kaskazini mwa Israel kutoka kwenye maeneo yanayoweza kulengwa na roketi na silaha zilizofyatuliwa na wapiganaji wa Kipalestina kusini mwa Lebanon, kwa kuwasukuma kilomita 40 kutoka mpaka wa Lebanon na Israel.

Lengo lingine liliwa ni kuharibu miundombinu ya shhirika la ukombozi wa Palestina, ikiwa ni pamoja na makao yake makuu mjini Beirut, na kuviondoa vikosi vya Syria kutoka Lebanon, kwa mujibu wa Israel.

Shambulio la Israel la mwaka 1982 halikuishia kusini mwa Lebanon, bali lilijumuisha maeneo mengi katika milima ya Bekaa, Chouf na Beirut.

Brigadia Jenerali Jaber anaamini kwamba uvamizi wa ardhi ndogo, iwapo utatokea utalenga kufikia "thamani ya maadili" na hakuna zaidi.

Stern anaamini kwamba Israel italenga, kupitia kwa vyovyote kuingia kusini mwa Lebanon, kuwasukuma wapiganaji wa Hezbollah kaskazini mwa Mto Litani, kwa sababu mbili kuu: "kuzuia ufyatuaji wa makombora ya masafa mafupi kuelekea miji ya Israeli, na kuzuia kujirudia kwa shambulio kama la Oktoba 7 kaskazini mwa Israeli."

Katika hotuba yake, Hassan Nasrallah alidokeza kuwa Israel inafikiria kuanzisha ukanda wa usalama ndani ya Lebanon kwa lengo la kugeuza umakini wa Hezbollah na kuilazimisha kuelekeza operesheni zake ndani ya ukanda huu mbali na kaskazini mwa Israel, lakini alisisitiza kuwa "hii haitazuia operesheni za Hezbollah dhidi ya maeneo ya kijeshi na miji ndani ya Israeli."

Je, uvamizi wa Lebanon utadumu kwa muda gani?

Awamu ya kwanza ya uvamizi wa mwaka 1982 ilidumu kwa miezi 3 na kumalizika kwa kuondoka kwa wapiganaji wa PLO kutoka mji mkuu wa Lebanon Beirut mwishoni mwa Agosti mwaka huo huo. Katika vita vya mwaka 2006, operesheni za ardhini zilidumu kwa siku 27.

Stern anaamini kuwa Israel imebadili mtazamo wake katika operesheni za kijeshi. Katika siku za nyuma, ilitegemea zaidi vita vifupi, vya haraka, lakini vita vinavyofuata vinaweza kuwa virefu.

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi