Je, ni washambuliaji gani hatari zaidi kwenye ligi ya Premier? Haland, Salah, Nunez, Ferguson

Wafungaji bora mara nyingi hupata nafasi nzuri kupitia uchezaji wao na uwezo nao, lawini wamalizaji wazuri pia hutumia vyema kile wanachopata.

Kwa kuangalia jinsi washambuliaji wakubwa wa Ligi ya Uingereza na mabao waliofunga tangu kuanza kwa msimu uliopita - ukiondoa penalti - tunaweza kuona ni nani amefunga magoli kwasababu alikua na fursa za juu zaidi na nani amekuwa mfungaji hatari.

Magoli yanayotarajiwa hupimwa kulingana na ubora wa fursa na uwezekano kwamba goli litafungwa kwa kutumia mashambulizi kama hayo katika siku zilizopita.

Takriban mashambulizi milioni moja kutoka hifadhidata ya kihistoria ya Opta hutumiwa kupima xG kwa mizani kati ya sifuri na moja, ambapo sifuri inawakilisha fursa isiowezekana kufungwa , na moja inawakilisha nafasi ambayo mchezaji angetarajiwa kufunga kila wakati.

Penalti hazijumuishwi katika hesabu hii kwa sababu ni rahisi sana kufunga. Mchezaji mmoja pekee kwa kila timu kwa kawaida hupata penalti na kushinda penalti si chini ya mpiga penalti pekee bali hutokana na wachezaji-wenza na mabeki machachari.

Washambuliaji wakuu tangu kuanza kwa msimu uliopita

Mshambulizi wa Liverpool Roberto Firmino aliondoka kwenye Ligi ya Uingereza akiwa na umaliziaji mzuri, akifunga mabao mara mbili zaidi ya ilivyotarajiwa. Alishinda mabao 11 chini ya idadi ya mabao 5.5 (xG) ambayo alitarajiwa kushinda.

Kiwango cha Taiwo Awoniyi mbele ya lango kwa sasa kinamweka miongoni mwa wamaliziaji bora, ingawa mshambuliaji huyo wa Nottingham Forest amecheza kwa wastani wa dakika 18 pekee kwa michezo yote.

Erling Haaland sio tu anapata nafasi nzuri, lakini bila shaka amekuwa mmaliziaji bora tangu ajiunge na Ligi Kuu msimu uliopita. Wakati Firmino na Awoniyi wamefanya vyema zaidi katika ubora wao, mshindi wa Kiatu cha Dhahabu cha Manchester City amedumisha umaliziaji wake bora kwa dakika nyingi zaidi za soka.

Harry Kane alikuwa na msimu wa mzuri zaidi katika maisha yake ya Ligi Kuu ya Uingereza kabla ya kuondoka Tottenham na kwenda Bayern Munich, akifunga mabao 50% zaidi ya ilivyotarajiwa msimu uliopita (mabao 25 yasiyo ya penalti kutoka mabao ya matarajio 16.6).

Evan Ferguson mchezaji mwenye ubora na namba zake tayari ziko juu. Ingawa bado ni mapema - mshambuliaji huyo wa Brighton mwenye umri wa miaka 18 amecheza zaidi ya dakika 1000 kwenye Ligi ya Uingereza.

Kwa upande mwingine, uwezo wa mshambuliaji wa Arsenal, Gabriel Jesus na Eddie Nketiah na wasaidizi wao umewafanya wote wawili kupata nafasi nzuri, lakini hakuna hata mmoja ambaye amekuwa mkali mbele ya lango.

Mchezaji nambari tisa wa Liverpool Darwin Nunez pia anapata nafasi nyingi lakini bado hajatenda vyema katika kuzitumia, nje ya umaliziaji wake wa hivi majuzi akiwa Newcastle.

Ikiwa tutarudi nyuma zaidi na kuona jinsi washambuliaji wakuu wa Ligi Kuu ya Uingereza walivyofanya katika mashindano tangu Septemba 2020, tunapata mtazamo sahihi zaidi na wa kujiamini katika uwezo wao wa kumaliza.

Jedwali la xG

Matokeo katika chati hii ni ya kina zaidi kuliko katika utafiti wa hivi majuzi kwani ni kweli kuwa kadiri muda unavyosonga, ndivyo idadi ya mabao ya mchezaji yanayovyokaribiana na magoli yake anayotarajiwa.

Mabao mengi ya ligi ya Premier tangu 2020-21 - takwimu zote isipokuwa penalti

Mabao xG Shoti mabao - xG

Harry Kane 57 49.4 386 +7.1

Mohamed Salah 53 52.8 387 +0.2

Son Heung-min 52 36.5 244 +15.5

Wachezaji kama Awoniyi, Ferguson, Nketiah na Nunez wako mapema sana katika maisha yao ya Ligi Kuu ya Uingereza kuonekana - tumeweka hitaji la chini la dakika 2700 za kucheza - kwa hivyo bado ni mapema sana kwetu kujua jinsi walivyofanikiwa.

Wakati idadi namba za Haaland ni sawa tangu ajiunge msimu uliopita wa joto, tayari amecheza mpira wa kutosha kuonyesha kuwa yeye ni bora. Akizidi nambari zake za xG kwa mabao 8 hadi sasa (mabao 34 yasiyo ya penalti kutoka xG ya 26.1).

Kando ya ujio wa hivi majuzi wa Haaland, Son Heung-min wa Tottenham bila shaka amekuwa mmaliziaji bora wa Ligi Kuu kwa misimu iliyopita.

Son amefunga karibu na kiwango cha Harry Kane na Mohamed Salah licha ya kupata nafasi chache sana, akifunga mabao 15 zaidi kuliko ilivyotarajiwa tangu kuanza kwa msimu wa 2020-21 - akiwashinda wachezaji wengine wote.