Je, ni kwanini Urusi inaboresha kwa siri uwezo wake wa nyuklia?

Chanzo cha picha, Wikimedia Commons/ISC Kosmotras
Kwa miaka kadhaa sasa, mamlaka za Urusi zimekuwa zikifanya kwa bidii na kwa siri uboreshaji mkubwa wa vifaa vyao vya nyuklia vya kijeshi, kulingana na gazeti la Ujerumani Spiegel.
Gazeti hilo lilichapisha matokeo ya uchunguzi uliofanywa na waandishi wa habari wa Spiegel pamoja na kituo cha utafiti huru cha Denmark Danwatch.
Kama ilivyoelezewa katika uchapishaji, wafanyikazi wa miundo hii yote miwili walipata ufikiaji wa mamia ya michoro ya kina na hati zingine za siri zinazoonyesha jinsi "Urusi inavyoimarisha uwezo wake wa nyuklia, kwa kutumia mfano wa msingi wa uzinduzi wa Yasny, ulioko katika mkoa wa Orenburg, kusini mwa Milima ya Ural.
Yasny ni mojawapo ya pointi 11 kwenye eneo la Urusi ambapo makombora ya masafa marefu ya ardhini, ikiwa ni pamoja na yale yenye vichwa vya nyuklia, yanaweza kurushwa.
Kulingana na waandishi wa uchapishaji huo wa kuvutia, kwa jumla, waandishi wa habari "walichambua hati zaidi ya milioni mbili zinazohusiana na ununuzi wa jeshi la Urusi, ambazo Danwatch ilitoa kwa utaratibu kutoka kwa hifadhidata ya umma kwa miezi mingi.
Hata hivyo, ukubwa wa kazi unaweza kutathminiwa kwa macho - kwa kulinganisha tu picha za satelaiti za eneo hili zilizochapishwa na waandishi wa habari, zilizochukuliwa kwa miaka kadhaa.

Wakati ambapo hapo awali juu ya uso wa dunia mtu angeweza tu kuona "kifuniko cha silo ya kombora na mijengo michache isio ya ajabu iliyozungukwa na uzio wa chini," majengo yote ya kijeshi sasa yamekua, yamezungukwa na mzunguko wa tatu wa umeme wa kiwango cha juu.
Kamera za uchunguzi zimewekwa kila mahali na hatua muhimu za ulinzi zimechukuliwa, ikiwa ni pamoja na sehemu za kurushia risasi zinazodhibitiwa kwa mbali, maguruneti ya waya tatu na mifumo ya kisasa ya ulinzi wa anga.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Katika baadhi ya picha, mtu anaweza kutambua majengo mahususi, kama vile minara ya uchunguzi iliyo katikati ya eneo lenye uzio.
"Kwa miongo kadhaa, watafiti wamekuwa wakifuatilia ukuzaji wa uwezo wa nyuklia wa Urusi kwa njia hii haswa, kwa kutumia picha za satelaiti," linaandika Danwatch, chapisho linalojulikana kwa uchunguzi wake juu ya mada muhimu, pamoja na matumizi mabaya ya madaraka, wizi, n.k.
"Hata hivyo, setilaiti haiwezi kuangalia chini ya paa, mbali na kupenya chini ya ardhi. Na hivyo hapo awali, ufuatiliaji wa kambi za nyuklia ulikuwa mdogo kwa hili," waandishi wa Danwatch wanaendelea. "Hadi hivi majuzi."
Na kutokana na "uvujaji mkubwa" wa hati za siri kutoka kwa vyombo vya usalama vya Urusi, waandishi wa habari wa uchunguzi wameweza kujifunza zaidi juu ya nini hasa iko katika eneo lililofungwa (rasmi kuwa na hadhi ya chombo kilichofungwa cha kiutawala-eneo), jinsi vitu hivi vimepangwa na jinsi vinavyolindwa.
Waandishi wa habari wamepata "mamia ya michoro ya kambi mpya za Putin," na kuifanya iwezekane "kwa mara ya kwanza kuondoa pazia la usiri unaozunguka mipango ya Vladimir Putin."
"Kwa michoro hii tunaweza kuangalia ndani ya majengo na hata kwenda chini ya ardhi kwa mara ya kwanza," anasema mwanzilishi mwenza wa Danwatch na mmoja wa wataalam wa ulimwengu wa silaha za nyuklia, Hans Christensen. "Hii haijawahi kutokea kabisa."
Vitisho vya Putin vinazidi kudhihirika
Kama uchunguzi unavyokumbuka, mnamo Machi 1, 2018, Rais wa Urusi Vladimir Putin alitoa hotuba ya kufurahisha huko Moscow, akitangaza kuundwa kwa safu nzima ya mifumo mipya ya silaha za nyuklia ambayo ingeipeleka nchi hiyo hatua moja mbele katika ushindani wa silaha na nchi za Magharibi.
"Hakuna mtu alitaka kutusikiliza wakati huo, "Kwa hiyo sikilizeni sasa."
Kile ambacho rais wa Urusi alinyamaza nacho wakati huo ni uboreshaji mkubwa wa kisasa na tata wa silaha za nyuklia za Urusi.
Ilichukua zaidi ya miaka 10 kuunda mpango wa kisasa, lakini wakati Putin alipotoa hotuba yake ya Moscow, kazi hii (pamoja na ile ya Yasny) ilikuwa tayari imeshafanyika.
Mamia ya maelfu ya hati zilizochunguzwa na waandishi wa habari zinaonyesha kuwa vituo vipya vya kijeshi vimejengwa katika miaka ya hivi karibuni kote Urusi.

Chanzo cha picha, Danwatch
Nyaraka zilizochapishwa na Spiegel na Danwatch zina michoro ya moja ya majengo kwenye eneo la kituo cha kijeshi cha Urusi. Madhumuni ya jengo ni vigumu kubaini hasa, lakini mpangilio wake unaonyesha "chumba cha kudhibiti" na vyumba vya walinzi.
Hii ni mojawapo tu ya miundo mingi iliyo kwenye idadi ya mitambo ya kijeshi iliyotajwa kwenye chapisho. Haijulikani ni ipi kati ya mipango hii ilitolewa kwa waandishi wa habari.
Hata hivyo, ukweli wenyewe kwamba nchi ya kigeni ina mipango yoyote kama hiyo inaleta tishio kubwa kwa usalama wa kambi za Kikosi cha Makombora cha Kimkakati (SMF).
Nyenzo za nyuklia zisizosimama, kama vile vizindua vya silo au vifaa vya kuhifadhia vichwa vya vita, kwa kawaida zinalindwa vyema dhidi ya mashambulio ya anga.

Chanzo cha picha, DANWATCH
Hii ndiyo sababu vitu kama hivyo vinalindwa na vitengo vilivyo na mafunzo maalum, vikiwemo vile vya Kikosi cha Makombora cha Kimkakati na mashirika mengine ya usalama.
Ikiwa michoro ya vitu kama hivyo itatolewa kwa umma, hii inaweza kinadharia kuwezesha maandalizi ya jaribio la kuvamia eneo lao.
Moja ya vitu, mchoro ambao, kulingana na ripoti za vyombo vya habari, uliishia mikononi mwa waandishi wa habari wa Magharibi, iko kilomita 30 tu kutoka mpaka wa Urusi-Kazakh.
Jimbo hili lina uhusiano mzuri na Urusi, na ni ngumu kufikiria kuwa vifaa vya nyuklia vitashambuliwa kutoka kwa eneo lake.
Imetafsiriwa na Seif Abdalla












