Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kuishi katika maeno ya uhasama wa kivita kati ya Marekani na China
Mazoezi makubwa zaidi ya kijeshi kati ya Marekani na Ufilipino yanakaribia kukamilika. Yalianza siku chache tu `baada ya jeshi la China kufanya mazoezi ya kutuma manoari na meli za kuzuia usafiri wowote wa majini kuingia au kutoka Taiwan – jambo ambalo Marekani lilisoluwa na uwiano. Huku hali ya wasi wasi ikiendelea kutokota katika kanda hiyo, watu wachache wanaoishi katika visiwa vidogo wamejipata katikati ya mvutano wa mataifa yenye nguvu zaidi.
Hali ya maisha ni tete katika eneo la Itbayat.
Ni miamba mirefu na vilima vyeye miteremko vinanavyounda kisiwa hiki kidogo sana kilichopo ukingoni kabisa mwa Ufilipino cha Luzon Strait.
Hata katika siku nzuri ya hali ya hewa, mawimbi makali hupiga kwenye maboti ya wavuvi wenye matumaini ya kuwanasa samaki wawapendao ambao huruka kwenye mawimbi.
Karibu, watu 3,000 wa jamii ya wazawa inayoitwaIvatans, ambao ni wavuvi na wakulima, wamenusurika na matetemeko ya ardhi, vimbunga na ukame. Lakini sasa wanakabiliwa na tisho tofauti na jipya.
Kisiwa chao cha nyumbani kinakabiliwa na hatari za kujipata katikati ya mzozo wa Marekani na China kwani shughuli za kijeshi za nchi hizi zinakaribiana kabisa ili kuweza kupata udhibiti wa Bahari ya China.
Wachambuzi mara kwa mara wamekuwa wakizungumzia kuongezeka kwa hali ya wasi wasi baina ya mataifa hayo yenye nguvu zaidi, lakini je inakuwaje kuishi katika eneo kubwa zaidi la mzozo baina ya Beijing na Washington?.
Itbayat mara kwa mara hukosa mawasiliano kwa wiki kadhaa. Huonekana kama eneo lisiloweza kuingilika. Bandari ndogo zimezingirwa na maporomoko na kuingia ndani ya boti ni lazima utelemke kwenye mteremko mkali chini ukipitia kwenye mwamba.
Ni watu wachache hapa wanaotazma televisheni. Kuna mtandao unaofikisha ujumbe kutoka nyumba hadi nyumba, ingawa kongamano la kanisa, mara nyingi huwa la kuaminika zaidi kuliko mtandao wa simu.
Ni nani anayetawala mawimbi?
Wanajeshi wa Marekani, wamekita kambi hapa , macho yao wakiyaelekeza kwenye darubini zao za kuona mbali. Ni wanajeshi wa kikosi cha silaha cha Marekani – Kitengo cha 25 wanaofanya mazoezi katika kisiwa cha Basco.
Wanafanya mazoezi ya kulinda kisiwa dhidi ya uchokozi au mashambulio yanayoweza kutokea. Mazoezi hay ani sehemu ya mazoezi makubwa zaidi ya mapigano kuwahi kufanyika kati ya Marekani na Ufilipino.
Kando ya bahari, shughuli hii ya mazoezi ilikuwa inadhibitiwa na meli ya - USS Miguel Keith, huku meli yndege ya V-22 Osprey ikizunguka juu ya kisiwa.
Lakini anakiri kuwa vikosi viwili vinatuma ujumbe.
"Ujumbe uliotumwa ni kwamba tupo hapa. tuna uwezo. tuna ushirikiano bora hapa. Na tumekuja kufanya kazi."
Pande mbili katika mzozo huu zinajihami, sawa na Asia nzima.
Kwa Washington haya sio maonyesho tu ya jeshi jipya linalong’ara.
"Hali inachemka," alikiri rais wa Ufilipino Ferdinand Marcos katika mahojiano ya hivi karibuni na redio nchini humo wakati alipokuwa akielekea kwenye ziara mjini Washington wiki hii.
Ameamua kuchukua msimamo wa wazi zaidi kwa Uchina kuliko mtangulizi wake na hilo linajumuisha kuagiza doria zaidi ya vikosi vya majini na walinzi wa mwambao.
Wavuvi kwenye viwanja vya mapambano
Beijing inadai umilikiwa karibu Bahari yote ya Kusini ya China – eneo la maji la kimkakati ambalo biashara za thamani ya mamilioni kuhipia kila mwaka – licha ya uamuzi wa mahakama ya kimataifa kwamba madai hayo hayana msingi wa kisheria.
"Wavuvi wa Kichina walikuwa wanatunyanyasa ," anasema Cyrus Malupa, mwenye umri wa miaka 59, huku akirusha waya mmoja wa kunasia Samaki ndani ya bahari na kuongeza kuwa lakini kwa sasa hawatunynyasi tena.
Mamia ya Wafilipino wameripoti matukio ya kufurushwa kutoka kwenye maeneo yao asilia ya uvuvi katika Bahari ya Kusini ya China kwa zaidi ya muongo – hususan katika maeneo ya bahari yanayozozaniwa yaliyopo karibu na Visiwa vya Spratly.
Manila iliwasilisha karibu pingamizi 200 za kidiploamasia dhidi yah atua za Beijing katika bahari ya Kusini ya China – ambako Vietnam, Malaysia, Taiwan na Brunei pia zimeanzisha madai ya kieneo.
Ni kawaida kuwa na hifu kwasababu mzozo wowowte utaathiri maisha yetu," alisema Victor Gonzales, mwenye umri wa miaka 51.
"Kwanza, tuna hofu kwa ajili ya maisha yetu na pia kuna uwezekano wa kuja kwa watu kutoka Taiwan wakati tuna raslimali chache."
"Tunahitaji kulinda raslimali zetu kwasababu ndio jinsi tunavyoishi, na hatuna maisha mengine mbadala . Tunataka kuwa na kitu cha kurithisha kizazi kijacho," anasema Victor.
Majeshi na washirika
Santa Ana ni mji uliopo kaskazini mwa kisiwa kikuu cha Luzon. Kuna shughuli chache katika ngome ndogo ya jeshi la wanamaji la Ufilipino iliyoko kwenye kona kabisa ya ufukwe ambayo ni vigumu kujua kuwa ilikuwa pale - isipokuwa unapogundua kuwa kuna ishara za eneo la ‘’vikwazo’’
La muhimu ina uwanja wa ndege ambao utaiwezesha Marekani kuifikia Taiwan moja kwa moja.
"Kiukweli sio ngome . Ninaweza kusema ni kama Kambi ya Maskauti wa Kiume," anadai Gavana wa Cagayan-Manuel Mamba.
Hii ni moja ya kambi nne mpya nchini Ufilipino ambazo majeshi ya Marekani yanaweza kuzitumia kufikia huku nchi hizi mbili zikiimarisha ushirika wao wa kijeshi. Maeneo yao mawili mapya yako katika jimbo la kaskazini la Cagayan na ambalo linatizamana na Taiwan.
"Huu sio wito wangu au wito wa watu wetu. Ni wito kwa viongozi wetu wa kitaifa. Tutauheshimu. Huenda tusikubaline nao, lakini kusema kweli hatutaki vita ," anasema Mamba.
"Tuko masikini na tuna matatizo yetu ya hapa pia. Ndio maana sababu yoyote itakayosababisha hofu itakuwa ni tatizo kubwa kwetu sote."
Bw Mamba anahofu kwamba kuwa na ngome mbili za Marekani katika jimbo kutalifanya lilengwe.
Kauli ya gavana Mamba inaonyesha kuongezeka kwa hali ya wasi wasi inayoendelea kuongezeka katika maeneo mbali mbali ya Asia.
Je watalazimika kuchagua kati ya mshirika wa muda mrefu, Marekani, na mshirika wake mkubwa wa kibiashara, China?.
"Sidhani Marekani itasababisha vita kwa mazoezi haya ya kijeshi. Ni Marekani tu inajaribu kusaidia jeshi la Ufilipino kukilinda kisiwa hiki na kuhakikisha mchina anafahamu kuwa eneo hili limelindwa," anasema Ave Marie Garcia, akiwa ufukweni.
Nyumba yao ya mababu , ambayo imejengwa kwa mawe na kudumu kwa karne na karne, imebaki kwenye magofu baada ya tetemeko la ardhi la mwaka 2019 – jamb linalokumbusha kuwa maisha ni ya wasi wasi hapa.
Watu hapa wanahisi kuwa mbali sana na siasa, na wanajaribu kutoingia sana katika kile kinachoweza kutokea, na kufurahia kile walichonacho.
"Maisha ya kisiwa ni rahisi," Ave anasema. Kila siku, yeye na familia yake wanomba hali itaendelea kuwa hivyo.