Kugongana kwa ndege ya Marekani na Urusi: Je, ni ajali?

Tukio lililohusisha ndege za kijeshi za Urusi na ndege ya Marekani ya kijasusi isiyoendeshwa na rubani katika Bahari Nyeusi inaonekana kuwa mkwaruzano mkubwa zaidi kati ya nchi hizo mbili tangu Urusi kuanzisha vita Ukraine zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

Tukio hilo la Jumanne lililoishia na ndege hiyo ya Marekani kuanguka baharini, linazua maswali na kuibua wasiwasi wa hatari kunukia licha ya Urusi kukanusha kuwa ndege zake ziliishambulia moja kwa moja ndge hiyo ya kijasusi ya Marekani.

Msemaji wa Barala la usalama wa taifa Marekani John Kirby amesema kumekuwa na matukio mengine yanayohusisha ndege za Urusi katika majuma ya hivi karibuni lakini hili ni tofauti na kuongeza operesheni imeanzishwa kuipata ndege hiyo ili kuepuka kile alichokitaja kuwepo katika mikono hatari

Je,ilikuwa ni ajali?

''Kutokana na vitendo vya marubani wa Urusi ni bayana ilikuwa hatari na kinyume na taratibu'' Anasema msemaji wa wizara ya ulinzi Marekani Jenerali Pat Ryder na kuongeza kuwa vitendo hivyo vilikuwa dhahiri kuonesha nia na makusudi.

Vitendo vya marubani wa Urusi vya kumwaga mafuta katika njia ya Droni kisha kugongana nayo ishara ya uhasama kuongezeka?

Kulingana na wizara ya ulinzi ya Marekani,tukio hilo lilidumu kwa muda wa kati ya dakika thelathini na arobaini. Jenerali Ryder anasema wakati huo hakukuwa na mawasiliano ya moja kwa moja kati ya wanajeshi wa Urusi na Marekani.

Maafisa wa Marekani wanaamini kuwa ndege za kijeshi za Urusi aina ya Su-27 zilizohusika katika kisa hicho huenda zilipata uharibifu fulani ikidokeza kuwa huenda mgongano huo haukuwa wa makusudi.

"Najua kuwa wizara ya mambo ya kigeni inawasilisha wasiwasi wetu kuhusu tukio hili moja kwa moja na serikali ya Urusi" Ryder ameripoti.

Tukio hili linamaanisha nini kwa operesheni zijazo za droni katika Bahari Nyesu na taarifa muhimu za kijasusi zinazotolewa kwa Ukraine?

"Iwapo ujumbe ni kutuzuia kutopaa au kufanya operesheni kwenye anga za kimataifa juu ya Bahari Nyesi," Kirby ameiambia shirika la habari la VOA, "basi ujumbe huo umefeli kwani hilo halitafanyika.

Litakuwa jambo la kushangaza iwapo Urusi inataka kufanya hali kuwa ngumu kwa washirika wa Ukraine kufanya operesheni za aina hiyo.

Marekani kwa sasa ikisalia kimya au kutoa taarifa kidogo kuhusu kilichoisibu droni yake. Ni wazi Washington haingetaka vifaa vyake muhimu kama cha kukusanya taarifa za kijasusi kuangukia mikononi mwa Warusi.

Ndege za kijasusi za Marekani zimekuwa zikishika doria katika bahari nyeusi kufuatilia muenendo wa vita hivyo vya Ukraine.