England wambeba paka baada ya kukosa Kombe la Dunia

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Paka kwa jina Dave

Three Lions hawakunguruma kwa ushindi wa Kombe la Dunia, lakini kiungo mpya wa kikosi hicho atarejea nao nyumbani.

Dave the Cat anayecheza kwa miguu atabadilisha joto la Qatar na kuituliza England - na kwa wakati muafaka wa dirisha la usajili la Januari.

Mnyama huyo amegusa mioyo kama kinyago kisicho rasmi cha wachezaji.

Hapo awali walisema watamrudisha Dave aliyepotea ikiwa wangeshinda kombe hilo, lakini waliamua kusafiri naye nyumbani licha ya huzuni yao ya robo fainali.

Wachezaji wawili wa Manchester City John Stones na Kyle Walker wamekuwa mashabiki wakubwa wa Dave, wakichapisha habari za mara kwa mara na picha za paka huyo.

"Siku ya kwanza tulipofika ... Tulimuona Dave," Stones alisema.

"Kila usiku amekaa pale akisubiri chakula chake."

"Alikuwa pale siku moja kwa hivyo tumemkubali yeye, mimi na Stonesy," Walker alikiambia kituo rasmi cha habari cha FA.

.

Chanzo cha picha, PA Wire

Maelezo ya picha, Paka Dave

Dave alikua mshiriki wa kawaida kwenye meza ya chakula cha jioni ya timu, ambapo Walker anasema "alikaribishwa" - lakini sio kila mtu alikubali.

"Watu wengine hawapendi paka, lakini ninampenda."

Mmoja wa waliotajwa kuruka juu Dave alipowasili ni Bukayo Saka.

John Stones anadai kumpatia jina zuri paka huyo

Na alianza kumwita "Big Dave" baada ya mgeni huyo wa chakula cha jioni mwenye miguu minne kuanza kuwa "mchoyo".

Ruka Instagram ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Mwisho wa Instagram ujumbe

Paka waliopotea ni jambo la kawaida katika mikahawa na hoteli katika taifa la Qatar.

Dave amevutia sio tu mioyo ya wachezaji wa England, lakini pia umakini wa vyombo vya habari vya ulimwengu - na maswali juu yake katika wiki ya kuelekea robo fainali dhidi ya Ufaransa.

Na, labda kwa kushinikizwa na mchezo dhidi ya Ufransa, Dave hivi majuzi aliingia kwenye "vita kidogo na paka mwingine", kulingana na Walker.

"Kupigania eneo na chakula. Lakini anaendelea vyema."

Dave anajiunga na orodha ya wanyama maarufu ambao wamegusa mahali maalum katika mioyo ya umma wa England.

Mmoja wao tayari ameandika furaha yake katika ujio wake

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Mwisho wa X ujumbe

Dave aliondoka Al Wakrah saa mbili tu baada ya kikosi cha England kuondoka na kwanza ataelekea kwa daktari wa mifugo.

Huko atapimwa damu na kupokea chanjo, akitumia miezi minne katika karantini kabla ya kuelekea kwenye nyumba yake mpya.

Hivyobasi wakati kombe la Dunia limewaponyoka England wanarudi nyumbani na paka Dave