Wasira: Martha Karua kawaponza wanaharakati wengine

Maelezo ya sauti, Wasira: Martha Karua kawaponza wanaharakati wengine
Muda wa kusoma: Dakika 1

Chama tawala nchini Tanzania CCM kimesema suala la mwanasiasa wa Kenya Martha Karua kuingilia maamuzi ya mahakama ya nchi hiyo ndio lililosababisha kuzuiliwa kwa wanaharakati wengine waliotaka kuja kushuhudia kesi ya mwanasiasa wa upinzani Tundu Lissu.

Katika mahojiano maalum na BBC, Makamu mwenyekiti wa chama hicho, Stephen Wasira amesema hatua hiyo ilikua ni kama kuingilia maamuzi ya ndani ya nchi kitu ambacho hakikubaliki.

Ameanza kwa kumuelezea mwandishi wa BBC David Nkya malalamiko ya kwamba vyombo vya dola nchini humo vinatumika kuukandamiza upinzani.