Liz Truss: Matukio sita ya kukumbukwa ndani ya wiki sita alizohudumu kama Waziri Mkuu

Liz Truss amejiuzulu kama waziri mkuu wa Uingereza baada ya kukaa madarakani kwa chini ya miezi miwili.

Kuanzia mkutano wake wa kwanza na Malkia, hadi machafuko ya bajeti yake ndogo, wiki zake sita madarakani zimekuwa mchanganyiko wa nyakati za kihistoria na migogoro ya kisiasa aliyojiletea mwenyewe.

Hapa kuna matukio sita ya kukumbukwa kwa muda wake mfupi aliyohudumu.

Mkutano wa kwanza na wa mwisho na Malkia

Ingawa ataingia kwenye historia kama waziri mkuu aliyekaa muda mfupi zaidi nchini Uingereza, Bi Truss alipigwa picha kwenye picha ya mwisho ya hadhara na mfalme aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi nchini humo.

Siku mbili kabla ya kifo chake, Malkia alimwalika rasmi Bi Truss - waziri wake mkuu wa 15 - kuunda serikali.

Picha ya wanandoa hao wakipeana mikono katika Kasri la Balmoral ilizua wasiwasi kuhusu afya ya Malkia, kwa sababu ya sura yake dhaifu.

Bi Truss alielezea kujisikia ‘’kuheshimiwa sana’’ kukutana na Malkia ‘’katika moja ya matendo yake ya mwisho’’

Kuporomoka kwa bajeti ndogo

Bi Truss alifanya kampeni juu ya mpango wa kupunguza ushuru na wiki kadhaa za muhula wake kama waziri mkuu, Kansela wake, Kwasi Kwarteng, alizindua mpango wa kupunguzwa kwa ushuru wenye thamani ya £45bn ($51bn).

Lakini Bw Kwarteng hakueleza jinsi punguzo hilo lingelipwa.

Bajeti ndogo ilitangazwa siku ya Ijumaa - lakini masoko ya hisa yalipofunguliwa tena Jumatatu iliyofuata asubuhi, pauni ilishuka hadi kufikia viwango vya chini dhidi ya dola.

Bajeti ndogo ambayo haikuwa ndogo ilizua msukosuko wa soko, huku Benki ya Uingereza ikilazimika kuchukua makumi ya mabilioni ya pauni ili kuleta uthabiti wa mifuko ya fedha za malipo ya uzeeni, na viwango vya mikopo viliongezeka.

Kansela alibatilisha baadhi ya mpango huu, lakini haikusaidia sana kuwatuliza wanasiasa katika chama cha Bi Truss cha Conservative Party.

Ingekuwa mpango wa kwanza wa kiuchumi kutangazwa na punde tu kuanza kubadilishwa, na kuwafanya wachambuzi wa uchumi kusema kwamba ‘ulikuwa umekufa.’’

Mkutano mfupi na wa kikatili na waandishi wa habari

Huku serikali ikiwa imetatizwa na mwitikio wa soko la hisa na uvumi mabadiliko makubwa, Bw Kwarteng aliitwa kutoka kwenye mkutano wa kimataifa huko Washington DC siku moja kabla ya kukamilika, na akafutwa kazi.

Saa chache baada ya kufutwa kazi, Bi Truss alikuwa na mkutano mfupi na waandishi wa habari ambapo aliulizwa mara kwa mara kuhusu uaminifu wake kama waziri mkuu.

Vipi mbona bado upo?, aliuliza mwandishi mmoja wa habari.

Ingawa alijibu maswali manne pekee, alijikwaa na majibu yake, akisisitiza kwamba alikuwa amechukua hatua ya ‘’kutuliza kuyumba kwa uchumi’’.

Utendaji wake usio wa kawaida wa dakika nane na waandishi habari haukuwashawishi Wabunge katika chama chake kwamba angeweza kuendelea kuwa kiongozi.

‘Mpendwa au mpenzi’’

Kanda za video kutoka ndani ya hadhira ya kila wiki kati ya mfalme wa Uingereza na waziri mkuu wao ni nadra.

Lakini picha zilipotolewa za Mfalme Charles wa Tatu akikutana na Bi Truss kwa mara ya kwanza katika kasri la Buckingham, hazikusaidia sana kurejesha sifa yake kwa watu.

Alipokabiliwa na shinikizo kubwa kutoka kwa wabunge wenzake waliokasirika kwenye chama, Mfalme alituma mitandao ya kijamii kukasirika baada ya kunung’unika ‘mpendwa au mpenzi’’ wakati wa wanazungumza na Bi Truss.

Ingawa msemo huo unasemekana kuwa kama ishara ya maneno ya Mfalme, ubadilishanaji huo wa maneno wa sekunde 15 ulianza kuenea haraka.

Hivi karibuni baadhi walidhani kwamba mfalme alikuwa akitoa ufafanuzi kuhusu uongozi wa Bi Truss, lakini vyanzo baadaye vilimwambia Mhariri wa Siasa wa BBC Chris Mason kwamba alikuwa akionyesha tu kusikitikia ratiba ya waziri mkuu, ambayo ilimwona akitembelea ikulu mara mbili katika kipindi cha masaa.

Barua ya maudhi ya Braverman

Siku moja kabla ya kuwasilisha barua yake ya kujiuzulu, Bi Truss alikuwa akipokea barua moja - kutoka kwa Waziri wake wa Mambo ya Ndani, Suella Braverman.

Aliyekuwa mpinzani wa waziri mkuu, Bi Braverman alijiuzulu kutokana na ukiukaji wa data mara mbili.

Na yeye hakuenda kimya kimya.

Katika barua yake ya kujiuzulu, alisema alikuwa amefanya ‘’ukiukaji wa kiufundi’’ kwa kutuma hati rasmi kutoka kwa barua pepe ya kibinafsi, na kwamba sasa anawajibika.

‘’Kujifanya kuwa hatujafanya makosa, kuendelea kana kwamba kila mtu haoni kuwa tumeyafanya, na kutumaini kwamba mambo yatakwenda sawa sio siasa kali,’’ aliandika.

‘’Nimefanya makosa; nakubali kuwajibika; najiuzulu.’’

Ujumbe huo ulichukuliwa kama kumshambulia waziri mkuu mbele ya umma, ukimkosoa Bi Truss na uongozi wake isipokuwa kwa jina.

Bi Braverman pia aliibua ‘’wasiwasi mkubwa kuhusu dhamira ya serikali hii ya kuheshimu ahadi za ilani’’ kuhusu masuala kama vile uhamiaji - hatua inayoonekana na watoa maoni wengi kama ombi la kuungwa mkono kwa watu wenye msimamo mkali wa chama katika kinyang’anyiro chochote cha uongozi siku zijazo.

Letusi lilikuwa na maisha marefu

Wakati mchambuzi wa masuala ya kisiasa alitania kwamba Bi Truss alikuwa na takriban maisha sawa na letusi’’ kwa maana ya muda wa kuhudumu, gazeti la Uingereza la Daily Star lilijibu kwa kujaribu nadharia hiyo moja kwa moja kwa wavuti wao.

Maelfu ya watu walitazama kutazama ‘letusi’, kando ya picha iliyowekwa kwenye fremu ya waziri mkuu.

Mboga iliponyauka taratibu mbele ya macho yao, ndivyo Bi Truss naye alivyoendelea madarakani.

Na wakati Waziri Mkuu alipotangaza kujiuzulu, karibu watu 20,000 walianza kupongeza letusi kwa kuwa katika ubora wake kwa muda mrefu ikilinganishwa na muda ambao Bi. Truss amekuwa madarakani.

Wimbo wa taifa ulichezwa, pamoja na remix ya Kool na Gang, wimbo ukiwa ni wa ‘’Sherehe’’.

‘’Letusi lafurahi,’’ ndivyo ulivyokuwa ukurasa wa mbele wa magazeti siku iliyofuata.

Na siku yenye misukosuko katika siasa za Uingereza ilipokaribia mwisho, magazeti yalikuwa na mbinu moja ya mwisho iliyotumia.

Giza lilipotanda jijini London, ilikadiria picha kubwa ya boga hiyo kwenye sehemu ya nje ya Westminster, kabla ya kutangaza kwenye Twitter kwamba ‘’letusi’’ imefika bungeni.