Kwanini vizazi vya watumwa vinataka Shaba za Benin zibaki Marekani?

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Katika msururu wa barua kutoka kwa waandishi wa habari wa Afrika, Mwandishi wa Mnigeria Adaobi Tricia Nwaubani anaangalia jinsi vizazi vya watumwa nchini Marekani vilivyoingia katika vuta nikuvute kuhusu kazi maarufu za sanaa ambazo ziliibiwa wakati wa enzi ya ukoloni na kuishia hususan katika majumba ya makumbusho ya nchi za Magharibi.

Kikundi cha Wamarekani wenye asili ya Afrika kimewasilisha kesi mahakamani kutaka kusitisha urejeshwaji wa baadhi ya Shaba za Benin kutoka katika makumbusho ya Smithsonian ya Washington DC.

 Wanadai kwamba shaba – zilizoporwa na wakoloni wa Kiingereza katika karne ya 19 kutoka katika ufalme wa benin katika kile ambacho sasa ni Nigeria – pia ni sehemu ya urithi wa vizazi vya watumwa nchini Marekani, na kwamba kuzirejesha ni kuwanyima fursa ya uzoefu wa utamaduni na historia yao.

'' Ni madai ya kushangaza," anasema David Edebiri mwenye umri wa miaka 93, baada ya kucheka kwa takriban sekundę 15.

Ni sehemu ya baraza la sasa la Oba wa Benin – mfalme au mtawala wa kitamaduni katika jimbo la kusini mwa Nigeria la Ido.

"Lakini vinyago hivyo vya shaba sio vya Oba pekee. Ni vya watu wote wa Benin, wawe Benin au katika mataifa ya kigeni."

Wengi wa Wanigeria ambao nilizungumza nao kuhusu kesi hii ya Marekani wameangua kicheko.

G
Maelezo ya picha, Deadria Farmer-Paellmann, muasisi na mkurugenzi mtendaji wa Restitution Study Group (RSG)

Lakini Deadria Farmer-Paellmann, muasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa Restitution Study Group (RSG) ambacho kilifungua kesi hii, yuko makini sana na kesi hii.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

 Bi Farmer-Paellmann mwenye umri wa miaka 56 alianzisha RSG, taasisi yenye makao yake New York, katika mwaka 2000 "kuchunguza na kutekeleza mbinu za uvumbuzi za kuponya majeraha ya unyonyaji na ukandamizaji wa watu".

Watumwa wapatao 100,000 walioletwa Marekani walikuwa kutoka kwenye bandari ambazo wakati mmoja zilidhibitiwa na wafanyabiashara kutoka ufalme wa Benin, kama vile Warri, anasema Bi Farmer.

Ananukuu rekodi kutoka kwenye kanzidata (Database) ya biashara ya watumwa kupitia bahari ya Atlantic iliyohifadhiwa na Chuo kikuu cha Rice cha Texas na vipimo vya hivi karibuni vilionesha kuwa 23% ya vipimo vyake vya vinasaba DNA vilimhusisha na watu hawa.

Hii, anaamini, inampa yeye na mamilioni wengine ambao wana mababu saw ana yeye haki ya kudai sanamu hizo za shaba.

Hoja zake ziko katika karatasi za manila, vipuri vilivyoanzishwa kama aina ya sarafu na wachuuzi wa Kireno, ambao kuanzia karne ya 16 hadi ya 19 walinunua mazao mbali mbali ya kilimo na bidhaa kutoka Afrika na pia binadamu.

Maelfu ya sanamu yanayofahamika kwa ujumla kama (Shaba za Benin) Benin Bronzes ambayo yaliporwa baada ya shambulio baya kwenye kasri ya Oba Ovonramwen Nogbaisi mwaka1897 yalitengenezwa kwa mchanganyiko wa vyuma vilevile shaba.

G

Chanzo cha picha, Alamy

Maelezo ya picha, Takriban manila 50 zililipwa kumnunua mtumwa vipuri vya mkononi mara nyingi vilikuwa vinayeyushwa ili kutengeneza vinyago.

Ufalme wenyewe haukutengeneza chuma cha kutosha kwa ajili ya kutengeneza vinyago hivyo, kwa hiyo ulitehgemea vyuma vinavyoagizwa kutoka nje- ikiwa ni pamoja na chuma cha shaba kutoka kwa vipuli hivi vya mikono, ambavyo viliyeyushwa ili kutengeneza vinyago.

"Manila 50 zilimnunua mtumwa mwanamke , 57 zilimnunua mtumwa mwaume," anasema Bi Farmer.

"Tunachosema ni kwamba vizazi vya watu waliochuuzwa kwa ajili ya hizi manila wana haki ya kuona hizi shaba kule wanakoishi," anasema.

"Hakuna sababu ni kwanini tulazimike kusafiri hadi Nigeria kuziona," alisema, akielezea tahahadhari za Marekani za kusafiri Nigeria. "Sitaki kutekwa nyara ."

'Tamaa ya Afrika'

Wakosoaji wa kesi hiyo, kama Bw Edebiri, wanadai kuwa sio manila zote zilitumiwa katika Benin zilitokana na biashara ya watumwa.

Ameandika kitabu kuhusu babu yake mzaa babu Iyase Ohenmwen, ambaye alikuwa Waziri mkuu wa Oba katika karne ya 19, akielezea kwa undani jinsi alivyofanya bishara ya pembe za ndovu na nguo za Ulaya.

G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Msanii maarufu wa Nigeria Victor Ehikhamenor anaamini shaba zinapaswa kurejeshwa mahali zilipotengenezwa.

"Alikuwa anazichukua manila hizi hadi Igun-Eronmwon, kijiji kilichopo Benin ambacho kilitengeneza kazi zote hizi za Sanaa. Walikuwa wanazitengeneza kuwa sahaba na vitu vingine vya kupendeza."

Msanii maarufu Mmarekani mwenye asili ya Nigeria Victor Ehikhamenor, ambaye anatoka katika jimbo la Edo, anadai kwamba huku historia ikiwa ngumu, suala moja ni rahisi: "Ardhi halisi ambako vitu hivi vilichukuliwa haijahama."

Kwa mwanahistoria wa masuala ya sanaa Mnigeria Chika Okeke Agulu, Profesa katika Chuo Kikuu cha Princeton na mwanaharakati aliye mstari wa mbele katikakampeni ya kurejea kwa kazi za usanii zilizoporwa, kauli za Bi Farmer Paellmann " zinasikika kama madai ya wazungu wasiotaka zirejeshwe walipozitoa".

"Ukosefu wa usalama ulinigusa kama aina nyingine ya tamaa ya Afrika ambayo tumeisikia kwa muda mrefu," alisema, akielezea kuhusu maelfu ya Wamarekani wenye asili ya Afrika ambao kwa sasa wanasafiri kusini magharibi mwa Nigeria kila mwaka kwa ajili ya tamasha la kila mwaka la Yoruba Osun Osogbo. Kukasirishwa na kurejeshwa kwa shaba Nigeria kumekuwa kukiendelea tangu miaka ya1930.

"Kuwepo kwake katika makumbusho ya Uingereza, ambayo ni mojawapo ya maeneo ya urithi, kunawaruhusu watu kuziona," alisema Oliver Dowden, waziri wa zamani wa Uingereza wa utamaduni, mwaka jana.

Lakini tangu wakati huo taasisi katika nchi za magharibi zimeanza hatimaye kuzirejesha sanamu hizo Afrika.

G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Sherehe ya Smithsonian ilikuwa ni mojawapo ya sherehe zilizofanyika mwaka huu kuadhimisha mabadiliko ya bahari katika mtazamo wa kurejesha hazina za thamani zilizoporwa

Sherehe ya Smithsonian ilikuwa ni mojawapo ya sherehe zilizofanyika mwaka huu kuadhimisha mabadiliko ya bahari katika mtazamo wa kurejesha hazina za thamani zilizoporwa.

Makumbusho ya Sanaa za kiafrika ya Smithsonian Museum of African Art, katika sherehe ya tarehe 11 oktoba, yalihamishia umiliki wa Sanaa 20 kwa Nigeria, wakati tisa zaidi zitaendelea kubakia kwenye makumbusho hayo kwa mkopo.

Kazi nyingine 20 za Sanaa ziko katika makumbusho ya taifa ya Kihistoria ya Smithsonian, na mchakato ambao unaweza kusababisha kuhamishwa kwake umeanza. Kesi ya Restitution Study Group inatumai kusitisha hilo.

'Tunaumizwa na aibu'

Bi Farmer-Paellmann amekuwa akipambana kwa muda mrefu na ajili ya kupatikana kwa vizazi vya watumwa nchini Marekani.

Katika miaka ya 1990, alianza kukusanya ushahidi wa kuonesha jinsi makampuni 17 yalivyojikusanyia utajiri mkubwa kutokana na utumwa, kama vile kampuni ya bima ya Lloyd ya London.

Mchakato wa kisheria uliishia miaka ya 2000 na zaidi baada ya RSG kuishiwa pesa.

Hatahivyo, baada ya maandamano ya Black Lives Matter ya mwaka 2020. Lloyd ya London iliomba msamaha kwa uhusiano wake wa zamani na biashara ya utumwa na ikajitolea kuwekeza kifedha katika kuinua maisha bora ya Weusi, Waasia na makundi ya watu wachache. 

Kila mara nilipowaandikia kuhusu urithi wa utumwa katika Afrika, nilipokea mamia ya ujumbe kutoka kwa Wamarekani wenye asili ya Afrika wakielezea hofu yao kwamba hadithi yangu inaweza kuathiri haja yao ya kupata fidia kutoka kwa vizazi vya wamiliki wa watumwa ambao wanaweza kutumia ushahidi uliopo wa uhusika wa Waafrika katika usafirishaji wa watumwa kupitia bahari ya Atlantic kama sababu ya kujiondoa katika lawama za maafa yaliyotekelezwa na mababu zao.

Kwahivyo, nilishangaa kuwa kikundi kama cha Bi Farmer-Paellmann kiliweza kuongea wazi kuhusu suala hili.

"Kuna aibu kubwa," anakiri. " Ni karibu na sawa na mtoto kumripoti mama yake kwa unyanyasaji wa watoto. Hilo ni jambo gumu kufanya."

"Lakini tunaumia kutokana na aibu huku warithi wa biashara ya utumwa wanaondoka na vito’’

Anatoa wito kwa kuwepo kwa mtazamo wa uelewa zaidi : "Hii ni fursa ya Nigeria kuchukua msimamo, mojawapo ya maeneo makubwa zaidi ambako vizazi vya watumwa walitoka – takriban milioni 3.6 yetu na akasema kuwa kitu cha heshima zaidi hadi leo ni kushirikishana hizi shaba

"Nigeria itasherehekewa kwa kufanya kitu kama hicho."