Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 14.10.2024

Muda wa kusoma: Dakika 2

Arsenal wana imani kuwa mlinzi wa Ufaransa William Saliba, 23, atasalia katika uwanja wa Emirates licha ya Real Madrid kumtaka (Express),

Juventus wanaweza kumnunua mshambuliaji wa Everton Mwingereza Dominic Calvert-Lewin, 27, ambaye mkataba wake utamalizika msimu wa joto. (Corriere dello Sport – In Itali)

Manchester United walimtafuta meneja wa Stuttgart Sebastian Hoeness, 42, kuchukua nafasi ya Erik ten Hag msimu uliopita lakini akawakataa. (Bild – In Dutch)

Manchester United bado iko kwenye nafasi ya kumsajili mkufunzi wa zamani wa Chelsea na Bayern Munich Thomas Tuchel, licha ya kocha huyo mwenye umri wa miaka 51 kuhusishwa na kibarua cha Uingereza. (TeamTalks)

Chelsea walijiweka kifua mbele msimu uliopita walipoishinda Bayern Munich katika kuinasa saini ya mlinda lango wa Genk Mbelgiji Mike Penders, 19, ambaye atahamia Stamford Bridge Julai ijayo. (Fabrizio Romano),

Mshambulizi wa Arsenal Muingereza Nathan Butler-Oyedeji, 21, anawindwa na Borussia Monchengladbach. (Football Insider),

Beki wa kati wa Ujerumani Marvin Friedrich, 28, anaweza kuondoka Borussia Monchengladbach mwezi Januari. (Sky Sport Germany kupitia Frankfurter Rundschau – in Dutch,

Arsenal wameungana na Tottenham katika kinyang'anyiro cha kumsajili kiungo mshambuliaji wa Ukraine Georgi Sudakov, 22 kutoka Shakhtar Donetsk. (Caught Offside)

Barcelona, Arsenal, na Newcastle wote wana nia ya kumsajili winga wa Ujerumani Leroy Sane mwenye umri wa miaka 28 kutoka Bayern Munich. (Ekrem Konur)

imetafsiriwa na Seif Abdalla