Je, Israel ilifanikiwa kuzuia uwezo wa Iran kuzalisha makombora ya masafa marefu?

g

Chanzo cha picha, Fatemeh Bahrami/Anadolu via Getty Images)

Maelezo ya picha, Maonyesho ya uwezo wa kikosi cha wanaanga cha IRGC
Muda wa kusoma: Dakika 4

Mkuu wa majeshi ya Uingereza amesema katika shambulio lake la Oktoba 26 dhidi ya Iran, Israel ilizima karibu mfumo wote wa ulinzi wa anga wa Iran na ndege za kijeshi za kizazi cha tano mia moja na kuharibu uwezo wa Iran wa kutengeneza makombora ya masafa marefu kwa mwaka mmoja.

Ndege za kijeshi za kizazi cha tano pekee za Israel, zenye uwezo wa ndege hizo kulingana na Admiral Tony Redkin, ni ndege za kivita za F35.

Hii ni mara ya kwanza kwa afisa wa ngazi ya juu wa jeshi kuzungumzia hadharani kuhusu aina ya ndege zilizotumika katika shambulio la Israel dhidi ya Iran na matokeo ya shambulio hilo.

Wakati wa hotuba yake katika taasisi ya Urusi (RUSI) mjini London, Admiral Tony Redkin, ambaye ni afisa wa ngazi ya juu wa jeshi la Uingereza na mkuu wa majeshi ya ulinzi, alisema kuwa shambulio la Israel lilionyesha faida za vita vya kisasa, na kuongeza kuwa Israel wakati wa wimbi la kwanza la mashambulizi yake dhidi ya Iran bila hata kuingia ndani ya maili mia moja kutoka kwenye malengo yake iliharibu uwezo wa Iran wa kutengeneza makombora ya masafa marefu kwa mwaka mmoja na imeiacha Tehran katika mkanganyiko wa kimkakati katika kujibu shambulio hili.

Hii ni mara ya kwanza kwa afisa wa serikali kuthibitisha rasmi kuingia kwa ndege za kivita za Israel katika anga za Iran.

Hapo awali, baadhi ya vyombo vya habari viliibua suala hili bila kutaja majina, vikiwanukuu maafisa wa Israeli.

Wakati wa hotuba yake katika taasisi ya Urusi, Admiral Sir Tony Redkin aliliita shambulio hilo kuwa matokeo ya "nguvu ya ndege ya kivita ya kizazi cha tano pamoja na ujasusi bora na kulenga vyema malengo."

Shambulio la tano la Israel mwezi Novemba lilitekelezwa katika mawimbi matatu, na jeshi la Israeli lilitangaza kuwa yalimalizika saa nne baada ya ripoti za kwanza. Jeshi la Israel linasema wakati wa shambulio hilo, lililenga maeneo 20, ambayo yanajumuisha maeneo ya kijeshi ya Iran na mifumo ya ulinzi.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Iran bado haijajibu shambulio la moja kwa moja la Israel katika ardhi yake, ambalo lilitekelezwa asubuhi ya tarehe 5 Novemba, lakini imesisitiza mara kwa mara kwamba ina haki ya kujibu.

Maafisa wa Iran wametangaza kuwa watu watano waliuawa katika mashambulizi hayo ya Israel, wengi wao ni wanajeshi kutoka jeshi la Jamhuri ya Kiislamu.

Ndege hiyo ya kivita aina ya F-35, iliyotengenezwa na kampuni ya silaha ya Lockheed Martin, inafahamika kama ndege ya kivita ya hali ya juu zaidi duniani, na Israel ilitangaza mwaka 2018 kuwa imeitumia katika operesheni za kivita hata mapema kuliko Marekani.

Mnamo mwezi Juni 2017, afisa wa kijeshi wa Israeli Meja Jenerali Amikam Norkin alisema kuwa nchi yake ilisafirisha ndege hizi za siri kote Mashariki ya Kati na kuzitumia kushambulia maeneo mawili (maeneo yanayohusiana na Iran).

Israel ilikuwa mteja wa kwanza wa F-35 nje ya Marekani kusaini mkataba wa ununuzi wa ndege hizi za kivita mwaka 2010, na mwishoni mwa mwaka 2016, ilipokea ndege mbili aina ya F-35 kati ya Hamsini ilizokuwa imeagiza.

Unaweza pia kusoma:
v

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ndege ya kivita ya Israel F-35 wakati wa mazoezi ya kijeshi Chanzo cha

Serikali ya Iran inasema kuwa shambulio lake la kwanza la moja kwa moja dhidi ya Israel la mnamo tarehe 25, Aprili 25, 1403, lilikuwa ni jibu kwa moja ya mashambulizi ya Israeli kwenye ardhi ya Syria, ambapo jengo la kidiplomasia la Jamhuri ya Kiislamu huko Damascus lililengwa.

Katika shambulio hilo la Israel, wanachama saba wa Jeshi la walinzi wa mapinduzi ya Kiislamu, wakiwemo makamanda wawili wa ngazi ya juu wa kikosi cha Wakurdi, pamoja na raia sita wa Syria waliuawa.

IRGC iliishambulia Israel kwa makombora 300 ya masafa marefu na ndege zisizokuwa na rubani katika operesheni yake ya kulipiza kisasi, ambayo iliiita "Wadah Sadeq 1".

Israel ilirusha kombora katika kambi ya jeshi la anga la Isfahan siku tano baadaye.

Mohammad Ali Jafari, Amiri jeshi mkuu wa zamani wa Jeshi la walinzi wa mapinduzi ya Kiislamu na kamanda wa sasa wa kambi ya kitamaduni na kijamii ya Jeshi la mapinduzi ya Kiislamu, kwa mara ya kwanza baada ya miezi sita, alikiri shambulio la kombora la Israeli kwenye kambi ya kijeshi huko Isfahan.

Katika sherehe ya kumbukumbu ya Abbas Nilfroushan, mmoja wa makamanda wa kikosi cha Kikurdi aliyeuawa nchini Lebanon, Bw. Jafari alikiri mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Israel kujibu operesheni ya "Ahadi ya kweli" na kusema kuwa Israel ilitumia "ndege za kisasa za Marekani" kufyatua "kombora moja au mawili" katika kambi ya Isfahan.

Maelezo ya serikali ya Iran hapo awali yalikuwa kwamba ulinzi wa anga wa Isfahan ulilenga "ndege wadogo na vitu vinavyotiliwa shaka" karibu na Isfahan.

Katika shambulio la pili, "Operesheni Sadeq Promise 2," mnamo tarehe 1 Oktoba mwaka huu, Iran ilizindua wimbi la mashambulizi ya makombora kwa makombora zaidi ya 180, ikiwa ni pamoja na kombora la Fatah, ambalo IRGC inaliita "hypersonic," moja kwa moja kutoka Iran ikilenga maeneo mbalimbali ya Israeli. Nchini Israeli, ving'ora vilisikika na watu wakakimbilia kwenye makazi.

Katika baaadhi ya mashambulizi ya shambulio hilo ambapo Israel ililenga "pointi 20" nchini Iran na wapiganaji wake. Shambulio ambalo admiral wa Uingereza aliliita mfano wa mafanikio bila kutaja maelezo zaidi.

Admiral Redkin alisema katika hotuba yake kwamba "dunia iko kwenye awamu ya tatu ya nyuklia".

Alisema kuwa zama hizi hazielezewi kwa kuzuia au kunyang'anya silaha, bali kwa kuenea kwa silaha na teknolojia za mabadiliko.

Unaweza pia kusoma:

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi