'Kwanini mashambulizi ya Iran dhidi ya Israel yamegonga mwamba?'

Chanzo cha picha, Press Eye
Katika uchambuzi wa magazeti ya leo, tunaangalia migogoro katika Mashariki ya Kati, hasa Gaza, na katika muktadha huu tunajadili msimamo wa utawala wa Biden juu ya mateso ya raia katika ukanda huo.
Tunaanza kwanza na mgogoro kati ya Israel na Iran, kutoka gazeti la Jerusalem Post, ambalo limechapisha makala ya mwandishi Neville Taylor, kuhusu mashambulizi ya Iran dhidi ya Israel na matokeo yake kwa Tehran na eneo lote.
Tyler anaamini kwamba "viongozi wa Iran wanataka kuiangamiza dunia, kuitawala Mashariki ya Kati, kupindua mfumo wa demokrasia wa Magharibi ambao Marekani ni mwakilishi muhimu zaidi, kuifuta hali ya Israeli, na kulazimisha Imani ya Kishia katika Uislamu duniani."
Mwandishi anasema: "Ulimwengu wa Magharibi ukubali usikubali kwa kupigana na Iran, Israeli inapigania uhuru wa ulimwengu wote."
"Hakuna shaka kwamba Iran inataka kuiangamiza Israel, na sio njia nyingine," alisema Taylor, akimaanisha shambulio la Aprili 13 dhidi ya Israel kama "kosa kubwa la kimkakati na mabadiliko makubwa katika sera ya Iran."
Taylor anaamini kuwa shambulio hili la Iran lilikuwa na matokeo mabaya, na "yawezekana" kwa Tehran, kwani lilikuwa shambulio la kwanza la moja kwa moja la Iran dhidi ya Israel.
" Uelewa mbaya"

Chanzo cha picha, Reuters
Mwandishi anasema kwamba uamuzi wa kuanzisha shambulio hili huenda ulifanywa kwa kuzingatia uelewa mbaya kuhusu ukweli wa Israeli: "kwamba ni katika hali ya udhaifu ambayo haijawahi kuwa hapo awali, kwamba inajihusisha na vita huko Gaza, ambapo haijafanikiwa kuangamiza Hamas au kuwakomboa mateka, "Inallaniwa na pande zote kutokana na idadi kubwa ya vifo vya raia, na kwamba inapokea mashambulizi ya kila siku kutoka kwa Hezbollah nchini Lebanon kaskazini na kutoka kwa Wahouthi nchini Yemen kusini."
Washauri wa Khamenei lazima wamsadikishe, Taylor aliendelea, kwamba mamia ya ndege zisizo na rubani za kamikaze, makombora ya masafa marefu, na makombora ya balistiki yangeweza kuishinda Israel, na kwamba angalau asilimia 50 ya makombora hayo yangeshambulia maeneo yao.
"Lakini kilichotokea ni kinyume na matarajio ya Khamenei na washauri wake mjini Tehran, ambao wote walipuuza jukumu la washirika wa Israel kutoka ndani ya eneo hilo au nje ya eneo hilo," kwa mujibu wa mwandishi huyo.
Mwandishi anakumbuka nukuu iliyohusishwa na Albert Einstein kwamba "utulivu unarudia makosa sawa na matumaini ya matokeo tofauti," akimaanisha katika suala hili kwa shambulio la pili la Iran mnamo Oktoba 1, ambalo Israeli ilijibu mnamo Oktoba 25.
"Kwahiyo, hakuna shaka kwamba Israel na Iran zina mgogoro, hata kama hakuna hata mmoja wao aliyetangaza rasmi vita dhidi ya mwingine. Hii inaelezea ubatili wa kusaini makubaliano yoyote ya kusitisha mapigano," kwa mujibu wa mwandishi.
Ujumbe wa Biden wa "mwisho" kwa Israel
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Tukiendelea na gazeti la Washington Post, tunasoma makala ya David Ignatius kuhusu kuwalinda raia wa Gaza au "kuacha kuipatia Israel silaha katika vita hivi."
Ignatius amesema mateso ya raia katika Ukanda wa Gaza yamekuwa magumu zaidi baada ya Israel kupiga marufuku shughuli za Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada na Kazi kwa Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) mnamo Oktoba 28, na hivyo kusitisha jukumu la shirika la Umoja wa Mataifa katika kuwapa raia wa Palestina chakula, dawa na maji, pamoja na huduma za elimu.
Mwandishi huyo amebainisha kuwa uamuzi wa marufuku uliochukuliwa na bunge la Israel, Knesset, ulikuwa ni kukataa moja kwa moja ombi lililowasilishwa na utawala wa Marekani ulioongozwa na Rais anayeondoka Joe Biden.
Katika barua iliyotiwa saini na makatibu wa mambo ya nje na ulinzi wa Marekani Antony Blinken na Lloyd Austin, utawala wa Biden uliionya Israel dhidi ya kupiga marufuku shughuli za UNRWA, ikisema kuwa "itadhoofisha kazi ya kutoa misaada Gaza." Hata hivyo, Knesset ilipuuza onyo la Marekani na kupitisha sheria yake, kwa mujibu wa Ignatius.
Mwandishi huyo alisema kuwa Israel huenda ikalazimika kujibu barua kutoka kwa Blinken na Austin, ya tarehe 13 Oktoba, leo, Jumanne, akibainisha kwamba Ron Dermer, mshauri wa karibu wa Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu, alitakiwa kuzungumza na Blinken Jumatatu jioni kuhusu barua hii.
Ujumbe wa Marekani unajumuisha onyo la kukata misaada ya kijeshi kwa Israel ikiwa hatua hiyo haitajibu hali mbaya ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza, ambako watu milioni 1.7 wa Gaza wamefurika katika kambi za pwani, ambako malori yanayobeba misaada yamekwama katika vivuko, na ambapo mashirika ya misaada "hayawezi kutoa mahitaji muhimu, "Kwa mujibu wa mwandishi.
Ignatius anasema ujumbe huo wa Marekani pia ulikuwa na kipengele cha kulazimisha, kwa kuwa ulizingatia mkataba wa usalama wa taifa uliotolewa mwezi Februari ambao ulieleza kuwa nchi yoyote inayopokea silaha kutoka Marekani lazima iheshimu haki za binadamu.
Mwandishi anasema kuwa timu ya utawala wa Biden inachukulia ushirikiano kutoka kwa Israeli kama suala ambalo "haliwezekani" sawa na alivyosema afisa mmoja, akionyesha kushindwa kwa majaribio ya mara kwa mara ya Blinken tangu siku za kwanza za vita kuwashinikiza Waisraeli kushirikiana ili kupeleka misaada ya kibinadamu kwa raia huko Gaza.

Chanzo cha picha, Getty Images
Ignatius alisema kuwa waziri wa zamani wa ulinzi wa Israel Yoav Galant wakati mwingine aliingilia kati kujibu ombi la Blinken la kupeleka misaada kwa raia huko Gaza, na sasa Netanyahu anamfukuza Galant - ambaye utawala wa Marekani ulimtegemea zaidi ya mtu mwingine yeyote katika serikali ya Netanyahu katika suala hili.
Mwandishi alihitimisha kwa kusema, "Biden alitoa wito kwa Israeli kuchukua hatua, na kuweka muda kwa Netanyahu kuchukua hatua hii."
"Maneno hayana maana tena," Ignatius alihitimisha. "Huu ni mtihani wa mwisho kwa rais anayeondoka. Iwapo Israel haitachukua hatua za haraka kuwalinda raia katika Ukanda wa Gaza, Marekani inalazimika kisheria kuacha kuiuzia Israel silaha inazotumia katika vita ambavyo vilipaswa kumalizika miezi kadhaa iliyopita."
Je, kurudi kwa Trump kunamaanisha "kurejea kwa makubaliano ya karne"?

Chanzo cha picha, Getty Images
Tunahitimisha uchambuzi wetu wa magazeti na gazeti la Al-Quds Al-Arabi na makala kuhusu "Deal of the Century" au ( Mkataba wa Karne) na mwandishi wa Palestina Muhammad Ayesh.
Mwandishi huyo alisema kuwa kurejea kwa Rais Donald Trump katika Ikulu ya White House kunakuja "baada ya mwaka mzima wa upendeleo kamili wa Marekani kwa vita vya Israeli, na bila shaka kura za Waarabu na Waislamu alizoshinda katika uchaguzi huu zilikuwa adhabu kwa Rais Biden, ambaye alitoa nguvu kamili kwa uchokozi wa Israeli, alitoa msaada kamili kwa uvamizi huo, na kuendelea kuwapa Waisraeli silaha zilizotumika katika vita hivi.
Hata wakati mzozo ulipozuka kati yake na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, hakutumia njia yoyote kumshinikiza, na Netanyahu aliishia kupuuza madai ya Biden."
Ayesh anaamini kwamba "Biden alimpa Netanyahu kila kitu alichotaka ili kuanza kutekeleza mradi wake wa kmaangamizi katika eneo hilo, ambao unategemea kuharibu fursa yoyote ya kuanzisha taifa la Palestina, hata baada ya muda."
Mwandishi aliendelea kusema: "Katika ngazi ya Palestina, inaonekana kwamba tofauti kuu kati ya Biden na Trump inahusiana na mpango wa karne, ambao ni mradi wa makazi kati ya Wapalestina na Waisraeli ambao Trump alipendekeza wakati wa muhula wake wa kwanza."
Ayesh anaamini kuwa "kitu hatari zaidi kuhusu mradi huu ni kwamba ni mpango, sio makubaliano. Trump anataka kutekeleza makubaliano hayo bila ya kuwafikiria Wapalestina, kuzungumza nao au kuyazingatia. Badala yake, anataka kuilazimisha na kuitekeleza kwa mapenzi ya Marekani na Israeli."
Mwandishi huyo alidokeza kuwa "wakati wa muhula wa kwanza wa Trump, utawala wa Marekani kwa kweli ulianza kutekeleza makubaliano haya, ambayo yalipata idhini ya Israeli, na Netanyahu akaona ndani yake ni kutimiza matarajio yake, kwani utawala wa Marekani uliamua kuhamisha ubalozi wake kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem, na kuanza kushughulikia mji mtakatifu kama mji mkuu wa Jimbo la Israeli, kinyume na makubaliano ya awali ya makaz ya Camp David, Wadi Araba na Oslo, na kinyume na maazimio ya Umoja wa Mataifa na uhalali wa kimataifa.
Ayesh anaamini kwamba "kitu muhimu zaidi katika mpango wa karne, ambao utarudi kwa Trump katika White House, ni kwamba unahakikishia udhibiti wa Israeli juu ya ardhi nyingi za Ukingo wa Magharibi ambazo Israeli ilizichukua mnamo 1967. Pia ni pamoja na kutwaliwa kwa kambi kubwa za makazi zilizopo katika Ukingo wa Magharibi na taifa ;a Israeli, pamoja na kuweka mji wa Jerusalemu pamoja na chini ya uhuru wa Israeli, ikiwa ni pamoja na Jerusalem Mashariki.
Mwandishi alihitimisha kuwa "mpango wa kurasa 181 wa karne unazungumzia wakimbizi wa Kiyahudi badala ya wakimbizi wa Palestina, jambo ambalo ni fjipya na ambalo halijawahi kujadiliwa hapo awali, wala hata kupendekezwa katika mazungumzo yoyote. Hiki ndicho watu wengi walielewa kama mlango mpya wa kupata fedha kutoka nchi za Kiarabu, pamoja na jaribio la kufuta suala la wakimbizi wa Kipalestina," alisema.
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi na kuhaririwa na Seif Abdalla












