Kiongozi wa upinzani wa Rwanda Victoire Ingabire akamatwa - kulikoni?

.

Chanzo cha picha, Jean Claude Mwambutsa/BBC

Muda wa kusoma: Dakika 3

Idara ya Upelelezi ya Rwanda imemkamata kiongozi maarufu wa upinzani saa chache baada ya kufika mahakamani kutoa ushahidi wake katika kesi inayowakabili baadhi ya wafuasi wake wanaotuhumiwa kwa jaribio la kupindua mamlaka mjini Kigali.

Victoire Ingabire ametajwa katika kesi dhidi ya watu tisa ambao ni pamoja na mwandishi wa habari wa ndani, na baadhi ya wanachama wa chama chake - ambayo imekataliwa kujiandikisha kisheria, anasema.

Bi Ingabire aliiambia mahakama kuu mjini Kigali Alhamisi asubuhi kwamba hakuhusika kivyovyote katika mafunzo ya mtandaoni ya 2021 yaliyotolewa kwa washtakiwa kupindua kwa njia serikali kwa za amani, ambazo ni msingi wa mashtaka dhidi yao.

Jana jioni mahakama ilitangaza kuwa haikuridhika na ushahidi wake na kuamuru uchunguzi wa wiki mbili dhidi yake, kabla ya ofisi ya idara ya upelelezi kutangaza kukamatwa kwake katika taarifa ya X usiku wa manane.

Bi Ingabire aliachiliwa kwa msamaha wa rais mwaka 2018 baada ya miaka minane gerezani kwa kutishia usalama wa taifa na "kupuuza" mashtaka ya mauaji ya kimbari ya 1994.

Amesisitiza kuwa kesi yake ilichochewa kisiasa

Tangu kuachiliwa kwake amedai kuzuiliwa kuondoka nchini kwenda kujiunga na familia yake aliyoiacha Uholanzi mwaka 2010 kufanya kampeni za kuwania urais.

Watoto wake na wajukuu wamemtembelea nchini Rwanda tangu kuachiliwa kwake.

Novemba mwaka jana, mawakili wake walitoa onyo kwa kuhofia usalama wake baada ya matamshi ya Rais Kagame ambayo yalimlenga Bi Ingabire kama mkosoaji wake, walisema.

Victoire Ingabire ni nani?

Bi Ingabire alirudi kutoka jela nchini Uholanzi 2010 ili kushiriki katika uchaguzi wa urais.

Alikamatwa na kuzuiliwa kuwania urais na amekuwa akihudumia kifungo jela tangu wakati huo.

Bi Ingabire , ambaye ni mwanachama wa kabila la Hutu, alikuwa akihoji ni kwa nini makumbusho ya mauaji ya halaiki nchini Rwanda ya 1994 hayakuhusisha watu wa kabila la Hutu.

Wengi wa watu 800,000 waliouawa walikuwa watu wa Kabila la Tutsi lakini Wahutu wenye msimamo wa kadri pia waliuawa na Wahutu wenye msimamo mkali.

Chama cha Rwanda Patriotic Front cha Rais Kagame kinachotawaliwa na Watutsi wengi kilimaliza mauaji hayo.