Je India kuwa nchi yenye watu wengi zaidi duniani ni baraka au laana?

Chanzo cha picha, Getty Images
Katikati ya mwezi Aprili, India inatabiriwa kuipita China kuwa nchi yenye watu wengi zaidi duniani.
Mataifa makubwa ya Asia tayari yana zaidi ya watu bilioni 1.4 kila moja, na kwa zaidi ya miaka 70 wamechukua zaidi ya theluthi moja ya idadi ya watu duniani.
Idadi ya watu nchini China huenda ikaanza kupungua mwaka ujao. Mwaka jana, watu milioni 10.6 walizaliwa, ikiwa ni zaidi kidogo kuliko idadi ya vifo, kutokana na kushuka kwa kasi kwa kiwango cha uzazi.
Kiwango cha uzazi nchini India pia kimepungua kwa kiasi kikubwa katika miongo ya hivi karibuni - kutoka kwa uzazi 5.7 kwa kila mwanamke mwaka 1950 hadi watoto wawili kwa kila mwanamke kwa sasa - lakini kiwango cha kupungua kimekuwa polepole.
Lakini je, India kuipiku China kama nchi yenye watu wengi zaidi duniani ina maanisha nini?
China ilipunguza idadi ya watu haraka kuliko India
China ilipunguza kiwango cha ongezeko la watu kwa karibu nusu kutoka 2% mwaka 1973 hadi 1.1% mwaka 1983.
Wataalamu wa takwimu wanasema mengi ya haya yalifikiwa kwa kuminywa kwa haki za binadamu - kampeni mbili tofauti za kukuza mtoto mmoja tu na kisha ndoa za baadaye, pengo refu kati ya watoto na wachache wao - katika nchi ambayo ilikuwa na watu wengi vijijini wasio na elimu na maskini.

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
India iliona ukuaji wa haraka wa idadi ya watu - karibu 2% kila mwaka - kwa sehemu kubwa ya nusu ya pili ya karne iliyopita. Baada ya muda, viwango vya vifo vilipungua, umri wa kuishi uliongezeka na mapato yalipanda. Watu zaidi - hasa wale wanaoishi mijini - walipata maji safi ya kunywa na mifereji ya maji taka ya kisasa. "Bado kiwango cha kuzaliwa kiliendelea kuwa juu," anasema Tim Dyson, mtaalamu wa takwimu katika Shule ya London ya Uchumi.
India ilizindua mpango wa uzazi wa mwaka 1952 na iliweka sera ya kitaifa ya idadi ya watu kwa mara ya kwanza kwa mwaka1976, wakati ambapo China ilikuwa na shughuli nyingi za kupunguza kiwango cha kuzaliwa.
Lakini kulazimishwa kufunga uzazi kwa mamilioni ya watu maskini katika mpango wa upangaji uzazi wakati wa dharura ya 1975 - wakati uhuru wa kiraia ulipositishwa - ulisababisha upinzani wa kijamii dhidi ya upangaji uzazi.
"Kupungua kwa uzazi kungekuwa haraka zaidi kwa India ikiwa dharura haingetokea na kama wanasiasa wangekuwa makini zaidi. Ilimaanisha pia kwamba serikali zote zilizofuata utaratibu kwa uangalifu linapokuja suala la kupanga uzazi," Prof Dyson anasema.
Nchi za Mashariki mwa Asia kama vile Korea, Malaysia, Taiwan na Thailand, ambazo zilizindua programu za idadi ya watu baadaye zaidi kuliko India, zilipata viwango vya chini vya uzazi, walipunguza viwango vya vifo vya watoto wachanga na wajawazito, kuinua mapato na kuboresha maendeleo ya binadamu mapema kuliko India.
Bado India haijapitia changamoto ya idadi ya watu
India imeongeza zaidi ya watu bilioni moja tangu Uhuru mnamo 1947, na idadi ya watu inatarajiwa kuongezeka kwa miaka 40 zaidi. Lakini kiwango cha ukuaji wa idadi ya watu kimekuwa kikipungua kwa miongo kadhaa sasa, na nchi hiyo imekaidi utabiri mbaya kuhusu "janga la idadi ya watu".
Hivyo India kuwa na watu wengi kuliko China sio muhimu tena au kuwa na wasiwasi, wanasema wanademografia.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kupanda kwa mapato na kuboreshwa kwa upatikanaji wa afya na elimu kumesaidia wanawake wa India kuwa na watoto wachache kuliko hapo awali, na hivyo kubana kwa ukuaji.
Viwango vya uzazi vimepungua chini ya viwango vya uingizwaji - watoto wawili wanaozaliwa kwa kila mwanamke - katika majimbo 17 kati ya 22 na maeneo yanayosimamiwa na shirikisho.
Kupungua kwa viwango vya kuzaliwa kumekuwa kwa kasi zaidi kusini mwa India kuliko kaskazini ambako kuna watu wengi zaidi. "Inasikitisha kwamba sehemu kubwa ya India haijaweza kuwa kama India kusini," anasema Prof Dyson.
"Mambo yote yakiwa sawa, ukuaji wa haraka wa idadi ya watu katika sehemu za kaskazini mwa India umeshuka viwango vya maisha".
Ingawa kuipita China linaweza kuwa jambo muhimu
Inawezekana, kwa mfano, kuimarisha madai ya India ya kupata kiti cha kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambalo lina wanachama watano wa kudumu, ikiwa ni pamoja na China.
India ni mwanachama mwanzilishi wa Umoja wa Mataifa na daima imekuwa ikisisitiza kwamba madai yake ya kiti cha kudumu ni ya haki. "Nafikiri kuna madai fulani kuhusu kuwa nchi yenye idadi kubwa zaidi ya watu," asema John Wilmoth, mkurugenzi wa Idara ya Watu katika Idara ya Umoja wa Mataifa ya Masuala ya Kiuchumi na Kijamii.
Jinsi idadi ya India inavyobadilika pia ni muhimu, kulingana na KS James wa Taasisi ya Kimataifa ya Sayansi ya Idadi ya Watu yenye makao yake Mumbai.
Licha ya mapungufu, India inastahili pongezi kwa kusimamia "mabadiliko yenye afya ya idadi ya watu" kwa kutumia upangaji uzazi katika demokrasia ambayo ilikuwa duni na isiyo na elimu, asema Bw James. "Nchi nyingi zilifanya hivyo baada ya kufikia viwango vya juu vya kusoma na kuandika na kuishi maisha ya wastani."

Chanzo cha picha, Getty Images
Habari njema zaidi. Mmoja kati ya watu watano walio chini ya miaka 25 duniani anatoka India na 47% ya Wahindi wako chini ya umri wa miaka 25. Theluthi mbili ya Wahindi walizaliwa baada ya India kufanya uchumi huria mapema miaka ya 1990. Kundi hili la vijana Wahindi wana sifa fulani za kipekee, asema Shruti Rajagopalan, mwanauchumi. "Kizazi hiki cha vijana wa India kitakuwa chanzo kikubwa cha watumiaji na wafanyakazi katika maarifa na uchumi wa bidhaa za mtandao. Wahindi watakuwa kundi kubwa la talanta za ulimwengu," anasema.
Lakini kuna changamoto pia
India inahitaji kuunda nafasi za kazi za kutosha kwa idadi ya watu wa umri wa kufanya kazi ili kupata faida ya idadi ya watu. Lakini ni asilimia 40 pekee ya watu wenye umri wa kufanya kazi nchini India wanaofanya kazi au wanataka kufanya kazi, kulingana na Kituo cha Kufuatilia Uchumi wa India (CMIE).
Wanawake wengi zaidi wangehitaji kazi kwani wanatumia muda mchache katika umri wao wa kufanya kazi kuzaa na kutunza watoto. Taswira hapa ni mbaya zaidi: ni 10% tu ya wanawake wenye umri wa kufanya kazi walikuwa wakishiriki katika nguvu kazi mwezi Oktoba, kulingana na CMIE, ikilinganishwa na 69% nchini China.
Kisha kuna uhamiaji. Baadhi ya Wahindi milioni 200 wamehamia ndani ya nchi - kati ya majimbo na wilaya - na idadi yao itaongezeka. Wengi wao ni wafanyakazi ambao huondoka vijijini kwenda mijini kutafuta kazi. "Miji yetu itakua kadiri wahamaji wanavyoongezeka kwa sababu ya ukosefu wa ajira na mishahara duni katika vijiji.

Chanzo cha picha, Getty Images
Je, wanaweza kuwapa wahamiaji hali ya kuridhisha ya maisha? La sivyo, tutaishia kuwa na makazi duni na magonjwa," anasema S Irudaya Rajan, mtaalam wa uhamiaji. Kituo cha Mafunzo ya Maendeleo cha Kerala.
Wataalamu wa idadi ya watu wanasema India pia inahitaji kuzuia ndoa za utotoni na kusajili ipasavyo kuzaliwa na vifo. Uwiano wa jinsia potofu wakati wa kuzaliwa - ikimaanisha wavulana wengi huzaliwa kuliko wasichana - bado ni wasiwasi. Matamshi ya kisiasa kuhusu "udhibiti wa idadi ya watu" yanaonekana kulengwa kwa Waislamu, walio wachache zaidi nchini humo wakati, kwa kweli, "mapengo katika kuzaa watoto kati ya makundi ya kidini ya India kwa ujumla ni madogo sana kuliko yalivyokuwa", kulingana na utafiti kutoka Kituo cha Utafiti cha Pew.
Na pia kuna kuna suala la umri nchini India
Wataalamu wa idadi ya watu wanasema suala la umri wa watu nchini India unapata umakini mdogo.
Mnamo 1947, umri wa wastani wa India ulikuwa 21. Asilimia 5 ya watu walikuwa zaidi ya umri wa miaka 60. Leo, umri wa wastani ni zaidi ya 28, na zaidi ya 10% ya Wahindi wana zaidi ya miaka 60. Majimbo ya Kusini kama vile Kerala na Tamil Nadu yalipata viwango vya mbadala takribani miaka 20 iliyopita.
"Kadiri idadi ya watu wa umri wa kufanya kazi inavyopungua, kusaidia watu wazee kutakuwa mzigo unaoongezeka kwa rasilimali za serikali," anasema Rukmini S, mwandishi wa Nambari Nzima na Nusu Ukweli: Lakini je takwimu zinaweza kusema nini na haziwezi kutuambia kuhusu India ya sasa.
"Miundo ya familia itabidi ibadilishwe na watu wazee wanaoishi peke yao watakuwa chanzo cha wasiwasi," anasema.












