Tetemeko la ardhi la Morocco: Mwalimu aliyepoteza wanafunzi wake wote 32

Children study in a school classroom

Chanzo cha picha, Adaseel Schools

Maelezo ya picha, Nesreen anaelezea wanafunzi wake waliopotea - wanaoonekana hapa kabla ya tetemeko la ardhi - kama "malaika"
    • Author, Yassmin Farag
    • Nafasi, BBC World Service

"Nilifikiria kushika sajili ya mahudhurio ya darasa langu na kupiga mstari jina la mwanafunzi mmoja baada ya mwingine, hadi nilipofikisha majina 32; wote wamefariki."

Nesreen Abu ElFadel, mwalimu wa Kiarabu na Kifaransa huko Marrakesh, anasimulia siku ambayo alikimbia katika kijiji cha Adaseel katika Milima ya Atlas ya Juu nchini Morocco, akiwinda miongoni mwa vifusi vya wanafunzi wake baada ya tetemeko la nguvu la 6.8 kupiga.

Nesreen na mama yake walikuwa wakikesha usiku kucha mtaani kufuatia tetemeko la ardhi la Ijumaa iliyopita, aliposikia habari za athari mbaya ya tetemeko hilo kubwa kwenye vijiji vya milimani.

Nesreen Abu ElFadel, mwalimu wa Kiarabu na Kifaransa huko Marrakesh, anasimulia siku ambayo alikimbia katika kijiji cha Adaseel katika Milima ya Atlas ya Juu nchini Morocco, akitafuta kwenye vifusi wanafunzi wake baada ya tetemeko lililopiga lenye ukubwa wa 6.8.

Mara moja alifikiria shule ambayo alikuwa anafunza - shule kuu za Adaseel - na wanafunzi wake, au kama anavyowaita "watoto wake".

"Nilienda kijijini na kuanza kuuliza kuhusu watoto wangu: Somaya yuko wapi? Yusef yuko wapi? Yuko wapi msichana huyu? Yuko wapi mvulana huyu? Nilipata jibu saa kadhaa baadaye: 'Wote wamefariki.'

School bags and a chair in a school

Chanzo cha picha, Adaseel Schools

Tarehe 8 Septemba, Morocco ilikumbwa na tetemeko kubwa zaidi la ardhi kuwahi kurekodiwa nchini humo, na ambalo ni baya zaidi kuwahi kutokea katika miongo sita likisababisha takriban vifo 3,000 na maelfu wengine wakiwa hawajulikani walipo.

Maeneo yaliyoathirika zaidi ni yale ya kusini mwa Marrakesh, ambapo vijiji vingi vya milimani viliharibiwa kabisa.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Mmoja wa wanafunzi waliofariki ambaye alipatikana na Nesreen ni Khadija - waokoaji walimkuta msichana huyo wa miaka sita akiwa amelala karibu na kaka yake Mohamed na dada zake wawili Mena na Hanan, Wote walikuwa kwenye kitanda chao - labda walikuwa wamelala - wakati tetemeko linatokea na wote walikuwa shule ya Nesreen.

"Khadija alikuwa kipenzi changu. Alikuwa mzuri sana, mwerevu, mwenye bidii na alipenda kuimba. Alikuwa akija nyumbani kwangu, na nilipenda kusoma na kuzungumza naye".

Nesreen aliwakumbuka wanafunzi wake kama "malaika", watoto wenye heshima ambao waliokuwa na hamu ya kujifunza.

Licha ya kung'ang'ana na umaskini na shida kubwa ya gharama ya maisha, watoto na familia zao walifikiria kwenda shule kama "jambo muhimu zaidi ulimwenguni".

"Darasa letu la mwisho lilikuwa Ijumaa usiku, saa tano kamili kabla ya tetemeko hilo kutokea," Nesreen alikumbuka.

"Tulikuwa tukijifunza wimbo wa taifa wa Morocco, na tukapanga kuuimba mbele ya shule nzima Jumatatu asubuhi.

'Sipati usingizi'

Damaged school building
Maelezo ya picha, Shule ambayo Nesreen alifundisha iliharibiwa vibaya na tetemeko la ardhi

Licha ya sauti yake tulivu, Nesreen amepata mfadhaiko wa akili. Bado bado hajaamini kilichotokea wanafunzi wake na shule yake.

"Sipati usingizi; bado nina mshtuko," alisema.

"Watu wananiona kuwa mmoja wa wale waliobahatika, lakini sijui jinsi ya kuendelea kuishi maisha yangu."

Nesreen alipenda kuwafundisha watoto Kiarabu na Kifaransa huko Adaseel, kijiji ambacho wengi wao ni Amazigh, wenyeji wa Afrika Kaskazini, ambao walizungumza zaidi lugha yao wenyewe, Tamazight.

"Kiarabu na Kifaransa zilikuwa lugha ngumu sana kujifunza, lakini watoto walikuwa werevu sana, na walikuwa karibu kujua lugha zote mbili," anakumbuka.

Nesreen anapanga kuendeleza kazi yake ya kufundisha - anatumai watajenga upya shule ya Adaseel, ambayo iliporomoka wakati wa tetemeko hilo.

Jumla ya taasisi za elimu 530 zimeharibiwa kwa viwango tofauti, ikiwa ni pamoja na baadhi ambazo zimeanguka kabisa au kupata uharibifu mkubwa wa miundo, kulingana na taarifa rasmi.

Serikali ya Morocco imesitisha kwa muda madarasa katika maeneo yaliyoathirika zaidi ya Al-Houz, Chichaoua na Taroudant.

"Labda siku moja watakapojenga upya shule na madarasa yatakapojengwa, tunaweza kuwakumbuka wale watoto 32 na kusimulia hadithi yao," Nesreen alisema.