Gereza la Saydnaya: Jinsi jengo la 'kichinjio cha binadamu' la Assad lilivyo

Chanzo cha picha, White Helmets
- Author, Matt Murphy
- Nafasi, BBC News
- Muda wa kusoma: Dakika 5
Tangu kusambaratika kwa utawala wa Assad siku ya Jumapili, raia wa Syria walikusanyika karibu na gereza la siri la Saydnaya wakiwa na matumaini ya kuwapata wapendwa wao.
Saydnaya ni gereza ambalo familia ya Assad ilikuwa ikizuilia mahasimu wake wa kisiasa kwa miongo kadhaa. Lilianzishwa miaka 1980 katika mji mdogo ulioyo takriban kilomita 30 (maili 19) kaskazini mwa jiji ka Damascus.
Maelfu ya watu wanaaminika kushikilia hapo, wakidhulumiwa na kuuawa gerezani humo tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Syria kuanza mwaka 2011. Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu, wamelipatia jina la ''kichinjio cha binadamu''.
Mpangilio wa gereza la Saydnaya ulikuwa ni siri kubwa na picha za kunavyokana humo ndani hazijawahi kuonyeshwa hadharani.
Maelezo ya mpangilio wa gereza hilo yanaweza tu kuelezewa kupitia mahojiano na walinzi wa zamani na wafungwa waliobahatika kuachiliwa huru.
Lakini taarifa kutoka kwa makundi ya kutetea haki za binadamu na Idara ya Mambo ya Ndani ya Marekani zimebainisha kuhusu gereza hilo ambalo lilikuwa nembo ya ukatili na udhibiti wa utawala wa Assad.
Kubuniwa kwa 'kichinjio cha binadamu'
Gereza la Saydnaya kwa miongo kadhaa imekuwa chini ya ulinzi wa maafisa wa polisi wa Syria na wanajeshi, ujenzi wake ukianza miaka ya 1980.
Wafungwa wa kwanza walifikishwa katika gereza hili lenye ukubwa wa 1.4 km mraba mwaka 1987, miaka 16 tangu utawala wa rais Hafeez al-Assad, babake Bashir, uanze.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Baada ya kukamilika kujengwa gereza hilo lilikuwa na sehemu mbili za wafungwa.
Jengo hilo lenye rangi nyeupe, kulingana na wanaharakati wa haki za binadamu ,lilijengwa kushikilia maafisa wa kijeshi na wanajeshi walioaminika kutokubaliana na sera za serikali tawala. Ilikuwa imejengwa kwa umbo la 'L' upande wa kusini mashariki ya jengo hilo kubwa.
Jengo hilo lekundu -gereza kuu- lilikuwa linawashikilia wakosoaji wa utawala.
Awali likijumuisha waliodaiwa kuwa wanachama wa makundi ya itikadi kali. Hii ilikuwa sehemu yenye umbo la 'Y' na likiwa na ushoroba tatu ikienea kutoka upande wa katikati.
Inakadiriwa kati ya wafungwa 10,000 hadi 20,000 wangeshikiliwa katika majengo hayo mawili, kulingana na mashirika ya kijamii ambayo yamezungumza na baadhi ya wafungwa walioachiwa huru.
Video zinazosambaa mitandaoni tangu Jumapili- ambazo zimehakikiwa na BBC Verify- zimeonyesha chumba kikubwa cha uangalizi kilichojaa skrini za kamera za siri CCTV zikionyesha seli kadhaa za gereza.

Ripoti ya mwaka 2017 kutoka kwa shirika la kutetea haki za binadamu a Amnesty International ikinukuu walinzi wa zamani katika gereza hilo ilibaini kuwa baada ya vuta vya Syria kuanza 2011 ,wafungwa waliokuwa kwa jengo leupe walihamishwa ,na kufanyiwa ukarabati kisha kuzuiliwa kwa waandamanaji waliokuwa wakipinga utawala wa Bashar al-Assad.
Aliyekuwa afisa aliiambia shirika la Amnesty kuwa'' baada ya mwaka 2011,[Saydnaya] ilikuwa gereza kuu la lilizuia wapinzani wa kisiasa nchini Syria''.
Shirika hilo pia lilinukuu ushuhuda wa wafungwa wa zamani wakidai kwamba wale waliokuwa waiishi katika jengo lililokuwa jekundu walikuwa wakipitia madhila kila uchao, ikiwemo vipigo vikali,ubakaji na kunyimwa chakula na matibabu hitajika.
Chini ya jengo hilo kulikuwa na jengo jeupe ambalo wale waliozungumza na Amnesty walilitaja kama ''chumba cha kuuawa''ambapo wafungwa kutoka jengo jekundu wangehamishwa ili kunyongwa.
Mlinzi wa zamani anasema kuwa orodha ya ambao walikuwa wanatarajiwa kunyongwa ilikuwa ikisomwa saa saba mchana.Jeshi lingenyanyua wale waliotajwa kuuawa na kuwapeleka kizuizini -ambacho wakati mwingine kilikuwa na hadi watu 100 -ambapo wangepewa vipigo .
Wafungwa ambao walizungumza na Amnesty walieleza kwamba wafungwa kutok ajengo jekundu walikuwa wakihamishwa usiku wa manane-kati ya saa sita za usiku n asaa tisa.
Waliofungwa kwa macho wangepelekwa kwenye ngazi hadi ''chumba cha kuuawa''kilichokuwa kwenye sehemu ya kusini mashariki ya jengo jeupe kabla ya kupandishwa kwenye jukwaa la urefu wa mita moja yenye mnyororo 10 ambapo wangenyongwa.
Kwa mujibu wa Amnesty, mwaka 2012 chumba hicho kilipanuliwa, na jukwaa la pili liliongezwa na mnyororo 20 zaidi.
Katika picha zilizosambazwa na chombo cha habari kilichoegemea waasi baada ya kuanguka kwa utawala, wapiganaji walionyesha minyororo walioipata katika seli zilizoko katika gereza la Saydnaya.
Inakadiriwa na mashirika ya haki za binadamu kuwa zaidi ya wafungwa 30,000 waliuawa ama kufa kutokana na mateso, ukosefu wa matibabu au njaa kati ya mwaka 2011 na 2018.
Kwa kutoa mifano kutoka kwa wafungwa wachache waliokolewa, angalau wafungwa wengine 500 walinyongwa kati ya 2018 na 2021, kulingana na Shirika la Waliohusika na Waliopotea katika Gereza la Saydnaya (AMDSP) mnamo 2022.
Mwaka 2017, Idara ya Jimbo ya Marekani ilidai kuwa mamlaka zilijenga mahali pa kuchomea maiti kwenye eneo hilo ili kutpa miili ya wafungwa waliouawa.
Katika picha hizi ,inaonekana ushoroba mdogo ukiungana n ajengo jeupe.

Msemaji wa Idara ya mambo ya ndani alisema kuwa maafisa walijenga jengo hili kama sehemu ya "juhudi ya kuficha kiwango cha mauaji ya kimbari yaliyokuwa yakitokea katika gereza la Saydnaya".
Picha za satelaiti zilizochapishwa na wataalamu wa Marekani zilionyesha jengo ambalo walidai lilikuwa ni jumba ndogo lililobadilishwa kuwa chumba cha kuchomea maiti.
Mamlaka walisema kwamba mchanganyiko wa theluji iliyoyeyuka juu ya paa la jengo hilo ulithibitisha madai yao – wakiongeza kuwa angalau wafungwa 50 kwa siku walikuwa wakinyongwa kwenye jengo hili wakati huo.
Ulinzi mkali uliozunguka gereza
Kwa muda wote wa historia yake, gereza hili lilikuwa limezingirwa na ulinzi mkali, huku uimarishaji ukizunguka eneo hili.
Nje ya gereza ililindwa na kikosi cha wanajeshi 200, huku wanajeshi wengine 250 kutoka kitengo cha ujasusi na wanajeshi kutoka idara ya usalama wa ndani, kulingana na ripoti ya AMDSP ya 2022.
Wanajeshi kutoka Kikosi cha 21 cha Divisheni ya Tatu ya jeshi walichaguliwa kulinda gereza hili kwa sababu ya uaminifu wao mkubwa kwa utawala.
Wanajeshi waliongozwa na maafisa kutoka kwa jamii ya Alawite ya Rais Bashar al-Assad.
Tangu kuanguka kwa utawala wa Assad, raia wametahadharishwa kuepuka kukimbilia kupitia ukingo wa gereza hili.
Mashirika ya haki za binadamu wanasema kuwa nje ya gereza kuna milipuko mingi. kuna bunduki za kijeshi za vifaru zimetegwa nje ya gereza, huku vilipuzi vikitegwa hadi katikati mwa gereza hilo.


Picha zilizosambazwa na kikosi cha White Helmets- kundi la ulinzi wa kiraia la Syria – zilionyesha kuta za juu zilizozungukwa na seng'enge ya stima katika gereza hilo.
Walinzi wanaoshika doria wakiwa wamesimam juu ya minara ya gereza hilo wameonekana wamesimama kwenye sehemu kadhaa za gereza.
Utawala wa Assad kila wakati ulikataa mashtaka yaliyoletwa dhidi yao na mashirika ya kimataifa, na kuyaita kuwa "yasiokuwa na msingi" na "bila ukweli".
Amnesty inasema kuwa kwa familia zinazoshuku kuwa jamaa zao wameshikiliwa katika gereza la Saydnaya, kuanguka kwa utawala kunatoa matumaini kuwa hatimaye wataweza kupat ufumbuzi kuhusu hatma ya wapendwa wao waliopotea, baadhi yao baada ya miongo kadhaa.
Imetafsiriwa na Mariam mjahid na kuhaririwa na Ambia Hirsi












