Je, timu za Uingereza kuzoa mataji yote matatu ya Ulaya?

Uingereza ina timu katika mashindano yote matatu ya Ulaya tunapoingia hatua ya robo fainali.
Hakuna nchi iliyowahi kushinda makombe yote matatu katika msimu mmoja, ingawa Ligi kuu iko katika mzunguko wake wa nne.
Aston Villa na Arsenal zinawakilisha ligi kuu England katika Ligi ya Mabingwa, huku Manchester United na Tottenham ziko katika Ligi ya Europa na Chelsea kwenye Conference League.
Scotland pia ina timu bado kwenye mashindano ya Ulaya, ambayo ni Rangers iliyo katika robo ya Ligi ya Europa pia.
BBC Sport inaangalia uwezekano wa timu hizo kunyakua makombe hayo.
Timu gani zimeingia fainali?

Chanzo cha picha, Getty Images
Aston Villa itacheza na Paris St-Germain katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa, huku Arsenal ikimenyana na mabingwa wa kihistoria, Real Madrid.
PSG iliifunga Liverpool katika hatua ya 16 bora, timu pekee ya Uingereza iliyotoka katika mashindano katika hatua hiyo msimu huu.
Manchester City, ambayo ilichapwa na Real katika raundi ya awali, ndiyo timu pekee ya Ligi Kuu ya Uingereza iliyotupwa nje katika mashindano ya Ulaya msimu huu.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Manchester United itamenyana na Lyon ya Ufaransa katika robo ya Ligi ya Europa baada ya Bruno Fernandes kufunga mabao matatu (hat-trick) katika ushindi wao wa bao 4-1 (ushindi wa jumla wa abao 5-2) dhidi ya Real Sociedad.
Bosi Ruben Amorim alisema: "Tuna michezo mingi kwenye ligi kuu. Ninaamini tutatumia kila dakika kuboresha timu. "Dhidi ya Lyon itakuwa mchezo tofauti, shughuli ipo.
"Wanacheza katika ligi ambayo ni ya ushindani sana. Utakuwa ni mchezo tofauti."
Tottenham, ambayo iliICHAPA AZ Alkmaar kwa jumla ya mabao 3-2, itacheza na Eintracht Frankfurt.
"Kulikuwa na mazungumzo mengi baada ya wiki iliyopita [kupoteza 1-0 ugenini], tulijiambia ukweli wenyewe hatukufanya vizuri vya kutosha', alisema mfungaji mabao James Maddison.
"Ninajua kile tunachoweza kufanya hapa na tumekamilisha kazi.
Hatujafanikiwa chochote bado, tuko katika robo fainali na tunaendelea na matumaini''
Rangers, ambao waliwashinda Fenerbahce kwa mikwaju ya penalti, watacheza na Athletic Bilbao mechi ijayo.
Na katika Ligi ya Conference, Chelsea - ambayo iliiondoa Copenhagen - itacheza na Legia Warsaw ya Poland.
Je timu za uingereza pekee kutinga fainali?
Katika Ligi ya Mabingwa, haiwezekani, lakini katika Ligi ya Europa, hilo linawezekana.
Arsenal na Villa wapo katika droo moja, ambapo kama zote zitafuzu robo fainali mana yake zitakutana katika nusu fainali.
Lakini Manchester United na Tottenham watakutana katika fainali ikiwa watashinda mechi zao za robo fainali na nusu fainali.
"Usidharau jinsi ilivyo muhimu kama United watafika fainali. Itampa Ruben Amorim umaarufu mkubwa," alisema kocha wa zamani wa United, Rene Meulensteen, kwenye BBC Radio 5 Live.
Rangers na Manchester United wanaweza kukutana katika nusu fainali.
Chelsea ndio timu pekee ya Uingereza inayoshiriki Ligi ya Conference.
Timu gani kutwaa ubingwa ?
Wataalamu wa takwimu wa Opta wanawaweka Arsenal kama timu ya tatu kuwa na uwezekano mkubwa wa kushinda Ligi ya Mabingwa, ikiwa na asilimia 16.8.
Aston Villa ni timu ya saba kwa uwezekano (yaani ya pili kutoka chini) ikiwa na asilimia 2.8.
Barcelona (20.4%) na PSG (19.3%) wanaonekana kama timu mbili zenye uwezo mkubwa wa kutwaa ubingwa wa Ulaya msimu huu.
Mahasimu wa Arsenal, Real Madrid, mabingwa watetezi, wanapewa asilimia 13.6 ya kushinda.
Katika Ligi ya Europa, Manchester United na Tottenham zinashikilia nafasi mbili kati ya tatu bora za kushinda, pamoja na Lazio.
Hii ni licha ya kuwa zote ziko chini katika msimamo wa ligi kuu England.
Chelsea wamekuwa ni timu inayotajwa kuwa na uwezekano mkubwa wa kushinda Conference league kwa sehemu kubwa ya msimu.
Blues, ambao wangekuwa timu ya kwanza kushinda Ligi ya Mabingwa, Ligi ya Europa na Conference league, wanashika nafasi ya nane katika viwango vya vilabu vya UEFA - katika mashindano yote.
Kocha wa Chelsea, Enzo Maresca, aliiambia TNT Sports: "Ni muhimu kufika robo fainali. Sasa lengo ni hatua inayofuata, ambayo ni nusu fainali.
"Klabu hii kila wakati imeshinda mataji katika historia yake na tunahitaji kufanya kila jitihada kufikia lengo letu msimu huu. Tunahitaji kuwapa mashabiki na klabu taji."
Mfungaji mabao Kiernan-Dewsbury Hall aliongeza: "Chelsea wamejishindia Ligi ya Mabingwa, Ligi ya Europa, itakuwa ujinga kwetu kusema hatuwezi kushinda kombe hili.
"Sio majivuno kwetu, lakini tunajua tu ubora tulionao katika kikosi. Copenhagen ni timu nzuri, lakini tunafurahi kuwa tumefika hapa."
Je nchi gani imewahi kupiku zote tatu?
Hakuna nchi ambayo imeweza kushinda Ligi ya Mabingwa, Ligi ya Europa na Ligi ya Conference katika msimu mmoja.
Lakini Roma, West Ham na Olympiacos ndiyo timu tatu pekee zilizoshinda Conference league hadi sasa.
Kumekuwapo mara sita tangu 2000 ambapo Ligi ya Mabingwa na Ligi ya Europa zote zimetoka katika nchi moja - na tano kati yao ni Hispania.
Mnamo 2006, 2014, 2015 na 2016 Sevilla walishinda Kombe la UEFA/Ligi ya Europa.
Barcelona ilishinda Ligi ya Mabingwa mwaka 2006 na 2015, huku Real Madrid ikishinda miaka mingine miwili (zote dhidi ya Atletico Madrid).
Mnamo 2018, Real Madrid ilishinda Ligi ya Mabingwa na Atletico ilitwaa Ligi ya Europa.
Lakini mwaka 2019, Uingereza ilifanya hatua moja bora na fainali zote za Uingereza.
Liverpool ilishinda dhidi ya Tottenham katika Ligi ya Mabingwa, huku Chelsea ikishinda Arsenal na kutwaa Ligi ya Europa.
Ligi ya Mabingwa/Conference league zilifanyika mwaka 2023 kati ya Manchester City na West Ham.












