Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Man Utd kusubiri uamuzi wa Sancho - Tetesi za soka Ulaya Jumapili
Manchester United wanasubiri Jadon Sancho kufanya maamuzi, Everton wanatafute mbadala wa Tyler Dibling, na Galatasaray watoa ofa kwa Ederson.
Manchester United wako tayari kukubali ofa ya Roma ya mkopo na wajibu wa kumnunua winga wa Uingereza Jadon Sancho, lakini wanasubiri mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kufanya uamuzi wa mwisho. (Fabrizio Romano)
Everton wanatafuta mbadala wa Tyler Dibling, 19, baada ya kuwa na ofa tatu - ya mwisho ikiwa ni takriban pauni milioni 37 - iliyokataliwa na Southampton kwa ajili ya winga huyo wa chini ya miaka 21 wa Uingereza. (Liverpool Echo)
Galatasaray wametoa ofa ya kwanza ya takriban £8.6m kwa mlinda lango wa Manchester City na Brazil Ederson, 31. (Fabrizio Romano)
Chelsea itamsajili tu winga wa Argentina Alejandro Garnacho, 21, kutoka Manchester United na kiungo wa kati wa Uholanzi Xavi Simons, 23, kutoka RB Leipzig ikiwa wanaweza kuuuza washambuliaji wawili. (Sky Sports)
Arsenal, Manchester United na Napoli wote wanavutiwa na kiungo wa kati wa Paris St-Germain na Korea Kusini, Lee Kang-in, 24, ambaye anafikiria kuondoka katika klabu hiyo ya Ufaransa ili apate muda zaidi wa kucheza. (Caught Offside)
Roma wamekubali dili la kumsajili winga wa Aston Villa na Jamaica Leon Bailey, 28, kwa mkataba wa mkopo wenye thamani ya £1.7m na chaguo la kumnunua kwa pauni milioni 20. (La Gazzetta dello Sport)
Nottingham Forest wamekubaliana mkataba na Rennes kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa Arnaud Kalimuendo mwenye thamani ya hadi £25m. (Telegraph)
Crystal Palace wamezungumza na Leicester City kuhusu Bilal El Khannouss, 21, huku kiungo huyo wa kati wa Morocco akionekana kama mbadala wa Eberechi Eze. (Athletic - subscription required)
Manchester United itafufua juhudi zao za kumsajili kiungo wa kati wa Brighton na Cameroon Carlos Baleba mnamo mwaka 2026 baada ya Seagulls kusema hawako tayari kumuuza msimu huu wa joto. (Fabrizio Romano)
Chelsea wameanza mazungumzo na Bayern Munich kuhusu kuuzwa kwa mshambuliaji wa Ufaransa Christopher Nkunku, 27. (Mail)
Fenerbahce wanatazamiwa kumsajili beki wa pembeni wa Arsenal na Ukraine Oleksandr Zinchenko, 28. (Sporx - in Turkish)