Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Uchaguzi DRC 2023: Ni upi mustakabali wa Joseph Kabila na chama chake cha PPRD?
Na Ousmane Badiane na Pamela Bamanay
BBC Africa
Yeye ndiye mtu ambaye hayupo zaidi katika ulingo wa kisiasa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Tangu aondoke madarakani Januari 2019, Joseph Kabila amekuwa akiishi kwa kujitenga katika shamba lake huko Kingakati, kilomita 50 mashariki mwa Kinshasa, au kwenye shamba lake lingine la Kashamata Lubumbashi, kusini mwa nchi.
Rais huyo wa zamani, ambaye alijiondoa katika maisha ya umma na kisiasa tangu alipotengana na mrithi wake Félix Tshisekedi mwishoni mwa 2020, amekuwa akiishi maisha ya ukimya.
Matembezi yake ya hadharani ni nadra, mawasiliano yake yanasalia kudhibitiwa sawa na wakati alipokuwa mamlakani kwa miaka 18.
Mkakati wa ukimya wake unazua fitina na maswali hasa katika muktadha wa uchaguzi mkuu huku chama chake cha kisiasa - Parti du Peuple pour la Reconstruction et la Démocratie (PPRD) kikikumbwa na changamoto nyingi tangu kilipoanzishwa.
Juni mwaka jana, Kabila alitoka katika hali yake ya kujificha kwa muda mrefu kwa kuitaka familia yake ya kisiasa "kupinga" ujanja wa kisiasa.
Mtangulizi wa Tshsekedi , pia alitumia fursa hiyo kuhoji "uaminifu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi huru (Ceni) na Mahakama ya Katiba ”, inayowajibika miongoni mwa mambo mengine kutatua migogoro ya uchaguzi.
Kabila, ambaye bado ana nguvu ndani ya taasisi za kisiasa, kiuchumi na kijeshi za DRC, ana mitandao imara iliyoendelezwa katika kipindi cha miaka 18 madarakani.
Siku chache kabla ya uchaguzi mkuu, BBC ilizungumza na Ferdinand Kambere, rafiki wa karibu wa Joseph Kabila na ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa PPRD, ambaye aliamua kuususia uchaguzi wa Desemba 20.
Kabila na chama chako kimeamua kutokwenda kwenye uchaguzi wa Desemba 2023. Kwa nini?
Ferdinand Kambere: Ndiyo, kama unavyojua, Joseph Desiré Kabila bado ni hakikisho la demokrasia katika nchi hii. Alitangaza Katiba, aliiheshimu na alihakikisha makabidhiano ya amani ya kidemokrasia nchini Congo, kwa ikiwa ni mara ya kwanza tangu uhuru. Na hivyo hatimaye, tunapofikia wakati ambapo ni lazima tuandae mchakato wa uchaguzi na kuna vyombo ambavyo vinapaswa kuamuliwa kwa maafikiano, tumeshuhudia ukiukwaji wa Katiba wa Mheshimiwa Félix Thisekedi, kwa kuanzishwa kwa mahakama ya kikatiba, lakini kikubwa zaidi tumeshuhudia ukiukwaji wa sheria ya utungaji wa Tume ya Uchaguzi (Ceni), huku hili likijadiliwa na kukubalika baina ya washirika, hasa wakati huu.
Tulishangaa kuwateua wajumbe wa Ceni hata hii sheria ilikiukwa hasa ibara ya 10 na 15 maana inasemwa wazi kwenye sheria kuwa wanachama wanateuliwa na vyama vya siasa na wanafanya uteuzi ambao wanaupeleka kwenye ofisi ya Bunge, hata ikiwa ni juu ya Bunge sasa, baada ya tume, kuthibitisha wagombea hao.
Utaratibu huu ulikiukwa na hii ilikuwa hatua ya tuliyokubaliana sote. Baadaye, hatukujali tena chochote kilichotokea na tuliweka wazi kwamba katika mchakato wa uchaguzi unaohusu uchaguzi ujao, washiriki wote wanapaswa kuhusishwa katika hatua zote. Hii ndiyo sababu hatukushiriki tena katika mchakato huu ili kukemea jambo hili.
BBC: Lakini wakati huo huo, chama chako kinakataa kwenda kwenye uchaguzi wa rais kama unavyosema. Je, hiyo si ni sawa na kujipiga risasi kwenye mguu?
FK: Hapana kwa uhakika, kwa sababu mwanzilishi wa chama hiki au bosi wa familia hii ya kisiasa aliona watu wamenaswa. Maana huko mnawatega wananchi mnasema mnaandaa uchaguzi kumbe mnaleta hali ya sintofahamu maeneo yenu. Lakini ukosefu huu wa usalama haukuishia tu Mashariki. Tumeshuhudia vikundi vyenye silaha hapa pia, ikiwa mambo yametulia huko Kasai ni bora zaidi.
Lakini wakati huo huo, katika ngazi ya kijamii, tumeona kwamba umaskini uliopo pia katika majimbo haya umesababisha watu kutoka vijijini, watu wamehama vijiji vyao kwenda majimbo mengine. Hili lina athari kubwa kwa watu, mtego na demokrasia.
Wanapokuwa wameiteka demokrasia kwa njia hii kwa kujenga ukosefu wa usalama, utulivu, uwepo wa majeshi ya kigeni, uanzishaji au uhamasishaji wa makundi yenye silaha ambapo wananchi hawataweza kufanya uchaguzi wa busara wakati kutakuwa na wagombea, hata kama kutakuwa na uchaguzi, upinzani hauwezi kuwa na uhuru kwenda wanapotaka , je, sisi hapa tunaoukosoa utawala huu xtutakwendaje pale wanaposifu makundi yenye silaha? Kwa masharti haya, mpinzani wa kweli wa serikali anaweza kwenda na kufanya mkutano katika eneo hili? Hapana.
Je, Kabila katika muktadha huu, kwake au kwa familia yake ya kisiasa, tayari mwaka 2018, ilikuwa vigumu katika eneo hili kumpigia kampeni Shadary, kwa sababu ya makundi yenye silaha yaliyokuwa upande wa Lamuka, ambayo yalibadilisha jina na kuwa Muungano mtakatifu leo. Hatukuweza kufanya kampeni tulivyotaka tukiwa madarakani. Sasa hebu fikiria mazingira ambayo leo wao ndio wako madarakani, tutafanyaje kampeni katika mazingira haya? Kwa hiyo huu sio uchaguzi huru, huu sio uchaguzi wa kidemokrasia, mchakato wenyewe ni wa kuegemea upande mmoja.
BBC: Hebu tuzungumzie chama chako cha siasa, PPRD, ni nini kimesalia cha chama chako leo, unafanyaje?
FK: Rais wa taifa ambaye ni kamanda yupo, tunafuata maagizo yake. Katibu Mkuu Comrade Emmanuel Ramazani Shadary yupo, anaendelea vizuri sana, sisi tupo kama manaibu wake. Kamati inafanya kazi, pia hukutana mara kwa mara. Na hata shughuli, unajua hilo. Na ukifuatilia kwenye mitandao ya kijamii, utaona kwamba mikoani, karibu kila mahali, hata katika majimbo yasiyo na utulivu, Kivu Kaskazini, Ituri, jimbo la mashariki, unaona bendera za PPRD. Kwa hiyo chama kinafanya vizuri.
Kamati ya taifa ipo, kuna shughuli katika ngazi ya kila mkoa. Chama kipo, katika ngazi ya eneo, kwa umakini na hata chini zaidi ya hapo.
BBC: Je, umesajili rasmi wanachama wapya? Je, unaweza kutupa takwimu sahihi kuhusu wanachama hai au hata wasioshiriki, lakini ambao wanabaki ndani ya chama baada ya kuondoka kwako?
FK: Naam, kama ningeangalia sajiri hapo awali, ningeweza kukupa takwimu kamili. Lakini ni hakika, ninaweza kukuhakikishia kwamba wanachama wapo. Hawa ni watendaji ambao kila mmoja aliondoka kwa sababu zake.
Sisi ni chama ambacho kilikuwa kimesimamia nchi kwa miaka kumi na minane. Kila mtu alikuwa na sababu za kuondoka, lakini wanaharakati wapo, watendaji wamebaki, watendaji wanaoendelea kukiongoza chama wapo.
Walioondoka walikuwa ni manaibu zaidi, kwa sababu unajua nini kilitokea jinsi walivyolaighaiwa na mamlaka, kwamba Bunge linakwenda kuvunjwa, hii bado iliwafanya baadhi ya watu kutetemeka ambao walidhani kwamba ili kuhifadhi viti vyao vya Bunge ni afadhali wawe wabunge upande wa serikali.
Lakini waliobaki, wapo, hawajaenda popote, kinyume chake uanachama nao unaongezeka katika mikoa yote.
BBC: Umezungumza tu kuhusu shughuli, je, unazifanya mara kwa mara?
FK : Ndiyo, ndiyo, angalau kila wiki kunakuwa na mikutano. Katika ngazi ya mkoa pia, kila mkoa hujipanga kwa njia yake. PPRD ni chama ambacho kina mizizi ya kijami.
Ni chama cha watu wengi, si chama cha makada. Kulikuwa na watendaji ishirini, arobaini au hamsini ambao labda walijulikana zaidi wakati huo katika msafara wa viongozi ambao watu waliwaona wakiondoka, lakini hawakuondoka na watu wengi.
BBC: Bwana Kambere, umesema, haushiriki uchaguzi. Kwa hivyo ni nini mipango yako katika kipindi hiki?
FK: Tunaendelea kumpigia kampeni ya kutaka Felix Thisekedi, aliyehudumu kwa muhula mmoja, kujiuzulu. Na sio mimi ninayesema bali ni Katiba. Kwa vyovyote vile kama CENI yake mwenyewe haijui hata jinsi ya kuandaa chaguzi wa ghasia ambao alitaka kuuandaa, kilichobaki kwake ni kujiuzulu.
BBC: Na iwapo uchaguzi utafanyika, na yeye au mtu mwingine kushinda utafanya nini?
FK: Kwetu sisi, uchaguzi, katika hali hizi, si uchaguzi unaowafurahisha watu wa Congo. Huu ni uchaguzi kwa ajili ya majeshi haya ambayo yeye mwenyewe aliyaalika katika ardhi ya Congo. Maana yake anataka kuandaa uchaguzi wakati kuna majeshi ya kigeni katika ardhi ya Congo, kuna hata makundi yenye silaha ambayo yanaungwa mkono. Kwa hivyo huwezi kuniambia, kama nilivyosema hapo awali, kwamba katika hali hizi, tunaweza kukubali kwamba kutakuwa na uchaguzi.
Kwa hiyo uchaguzi, wakitaka kuwa nao, ni kwa ajili yake huko Kasai, na pengine kwingineko, na katika sehemu ya Jamhuri. Kwa wakati huo haiwezekani tena, hatutakuwa tunazungumzia jamhuri moja, kwa hiyo tunaendelea kupinga kuonyesha kuwa uchaguzi utakaofanyika sio mafanikio.
BBC: Lakini una mipango gani kwa 2028? Je, chama kinakusudia kujipanga vipi ili kiwepo kisiasa hadi 2028?
Ni chama cha siasa, unajua, kazi ya chama cha siasa, ni nini? Alipopoteza nguvu, ilikuwa ni kurejesha nguvu. Tuko hapa kurudisha madaraka na ni haki ya kikatiba, ni haki yetu. Tunaweza kupoteza huko kupigana dhidi ya haya yote na kupata tena mamlaka, kwa mara nyingine tena, kuwapa watu hawa uhuru, kwa nchi hii, kurejesha uadilifu wa eneo hilo.
Congo haiko tena katika uadilifu wa eneo lake. Kwa hivyo, PPRD inalenga kuleta amani Mashariki, kuwarudisha Wacongo kazini. Hivyo ndivyo inavyopaswa kuwa , hatuna chaguo.
Lazima tuirudishe amani, uadilifu wa eneo hilo, amani na kuwarudisha Wacongo kazini ili kuwarudishia tabasamu ambalo hawana tena tangu Felix Thisekedi ingie madarakani.
BBC: Na kama ungepigiwa simu na serikali kujaribu kuketi kwenye meza ili kuona jinsi ya kuleta amani nchini DRC, je, utakubali?
FK: Hapana, serikali hii haina tena chaguo ila kujiuzulu kwa sababu si halali tena. Nilikuambia kuwa amebakiza siku chache tu kwa hivyo hakuna cha kuelezea zaidi. Pengine tunaweza kuchagua mtu mwingine lakini serikali hii tayari imetimiza wajibu wake. Hana chochote zaidi cha kutuelezea.
BBC: Ulisema kwamba dhamira yako ni kuiteka tena DRC, unapanga kufanya hivi kivitendo Bw. Kambere?
FK: Hili lazima lifanywe kwa njia za kidemokrasia. Hii ina maana kwamba kwa vile wameshindwa kuandaa uchaguzi mzuri kwa tarehe iliyopangwa, ni lazima waondoke na kutupisha njia. Ni juu ya Wacongo wenyewe kuamua hatima yao, kwa kuandaa uchaguzi mpya na uchaguzi mzuri wa kidemokrasia ambao utawafaa Wacongo, kwa faida ya watu wa Congo. Hatuwezi kurejea kila mara kwa kile kilichoelezwa mwaka miaka ya 1960, 61, 64 kwa sababu hapo ndipo Bw. Thisekedi aliturudisha.
BBC: Lakini unaposema wacongo, hawa Wacongo ni akina nani?
FK: Ndiyo watu wa Kongo, ambao wameelezewa katika kifungu cha 5 cha Katiba, ambao ni watawala, ndio pekee wanaoweza kumpa mtu mamlaka.
Mahojiano yaliyofanywa na Pamela Bamanay mjini Kinshasa
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi