Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 16.01.2024

Chanzo cha picha, getty images
Manchester United wamejadili uwezekano wa kumnunua winga wa Uingereza Michael Olise, 22, msimu wa joto na watakuwa tayari kumruhusu mlinzi wa Uingereza Aaron Wan-Bissaka, 26, kuhamia Crystal Palace . (ESPN)
Paris St-Germain wanafikiria kumnunua kiungo wa kati wa Newcastle Brazil Bruno Guimaraes, 26, ambaye ana kipengele cha kuachiliwa cha pauni milioni 100(Talksport)
Sir Jim Ratcliffe anataka kumsajili mshambuliaji wa kati wa daraja ya juu, ambaye yuko katika kiwango sawa na mshambuliaji wa Bayern Munich , Harry Kane, 30, mara tu mkataba wake wa kununua 25% ya Manchester United utakapoidhinishwa na Ligi Kuu(Standard)

Chanzo cha picha, Getty Images
Newcastle wamesitisha harakati zao za kumnunua kiungo wa kati wa Uingereza Kalvin Phillips, 28, kwa sababu ya madai ya Manchester City ya kutaka ada ya mkopo. (Telegraph - usajili unahitajika)
Kando na Magpies, Crystal Palace , Everton , West Ham na Juventus wana nia ya kumsajili Phillips. (Sky Sports)

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United wamejadili uwezekano wa kumnunua winga wa Uingereza Michael Olise, 22, msimu wa joto na watakuwa tayari kumruhusu mlinzi wa Uingereza Aaron Wan-Bissaka, 26, kuhamia Crystal Palace . (ESPN)
The Red Devils pia wameungana na Bayern Munich katika harakati za kumsajili beki wa Barcelona mwenye umri wa miaka 23 kutoka Uruguay Ronald Araujo. (Florian Plettenberg)
Kiungo wa kati wa Ureno Renato Sanches huenda akahama mwezi huu kwani Paris St-Germain hawataki beki huyo mwenye umri wa miaka 26 na klabu ya sasa ya mkopo Roma inamtaka atafute klabu nyingine. (Fabrizio Romano)
Mchezaji huru Jesse Lingard, 31, yuko tayari kuhamia Ligi Kuu ya Soka (MLS) na maajenti wake wapya katika mazungumzo na Portland Timbers huku kiungo huyo wa kati wa Uingereza akijaribu kurejesha hali yake ya mchezo katika hali nzuri (Mail)
Chelsea inaweza kuvutiwa na mkataba wa mkopo wa muda mfupi na Aston Villa kwa mshambuliaji wa Colombia Jhon Duran, 20. (Nathan Gissing, kupitia Metro)

Chanzo cha picha, Getty Images
Chelsea pia wanafuatilia Ligi ya Saudia na wanaweza kumnunua mshambuliaji wa Al-Ittihad na Ufaransa Karim Benzema, 36, au fowadi wa Brazil Roberto Firmino, 32, ambaye alijiunga na Al-Ahli msimu wa joto. (Goal)
Chelsea wanatarajiwa kuitisha utekelezaji wa kifungu kamili cha pauni milioni 35 kwa mkataba wowote unaohusu uhamisho wa kudumu wa beki wa kushoto wa Uholanzi Ian Maatsen, 21, ambaye yuko kwa mkopo Borussia Dortmund . (Telegraph - usajili unahitajika)
Celtic wanavutiwa na mlinda lango wa Liverpool Caoimhin Kelleher, 25, lakini wanaweza kukabiliana na ushindani kutoka kwa Brentford , Brighton na Wolves kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Jamhuri ya Ireland. (Mail)
Imetafsiriwa na Yusuf Jumah












