Tetesi za soka Ulaya Jumamosi: Man City, Chelsea na Bayern wanamtaka Thiago

Brentford striker Igor Thiago

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 3

Man City, Chelsea na Bayern Munich wana nia ya kumsajili Igor Thiago, beki Dayot Upamecano amekatisha matumaini ya Real Madrid na Liverpool, huku Real Madrid ikitaka kumbakisha Endrick klabuni msimu ujao.

Manchester City, Chelsea na Bayern Munich bado wanamtaka mshambuliaji wa Brazil Igor Thiago, 24, licha ya kusaini mkataba mpya na Brentford. (Teamtalk)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Beki wa Ufaransa Dayot Upamecano, 27, amekatisha matumaini ya Liverpool na Real Madrid kumsajili msimu huu wa joto baada ya kusaini mkataba mpya na Bayern Munich. (Sports Illustrated)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Arsenal, Chelsea na Tottenham wameambiwa mshambuliaji wa Brazil Endrick hatapatikana msimu huu wa joto. Real Madrid wanasema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19, ambaye yuko kwa mkopo kwa msimu mzima na Lyon, atarudi Bernabeu kama sehemu ya kikosi chao cha kwanza msimu ujao. (Teamtalk)

Manchester United itataka kumuuza kipa Andre Onana msimu huu wa joto. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon mwenye umri wa miaka 29 yuko kwa mkopo Trabzonspor baada ya kupoteza nafasi yake Old Trafford. (Sun)

.

Inter Milan wanapanga kutumia kifungu cha kumnunua tena ili kupata huduma za kiungo Aleksandar Stankovic, licha ya kukabiliwa na ushindani kutoka Manchester United, Arsenal, Chelsea na Tottenham. Walimuuza Mserbia huyo, 20, kwa Club Brugge msimu uliopita wa joto lakini wanaweza kumrudisha kwa euro milioni 23 (pauni milioni 20). (Fabrizio Romano)

Real Madrid itaanzisha kipengele chao cha kumnunua tena kiungo wa kati wa Argentina Nico Paz, 21, kutoka Como msimu huu wa joto (Fichajes - in Spanish)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Tottenham wameacha mlango wazi kwa kocha wa Marekani Mauricio Pochettino, 53, kurudi klabuni msimu huu wa joto, huku Muargentina huyo akiwa ameiongoza klabu hiyo hadi fainali ya Ligi ya Mabingwa. (Telegraph - subscription required)

Manchester City wako tayari kutoa takriban euro milioni 50 (£43.4m) kumsajili beki wa kulia wa Brazil Wesley Franca, 22, kutoka Roma msimu wa joto. (Fichajes - in Spanish)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Newcastle, Tottenham, na Aston Villa wamejiunga na Arsenal, Chelsea, Liverpool, Manchester City na Manchester United katika kumfuatilia mshambuliaji wa Bournemouth, Eli Junior Kroupi, 19. (Teamtalk)

Manchester United wamefanya mazungumzo ya kumsajili beki wa Manchester City mwenye umri wa miaka 16 kutoka Uingereza, Kasen Brown. (Football Insider)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Barcelona wanataka kupunguza kima cha pauni milioni 26 katika chaguo la uhamisho ambalo awali lilikubaliwa kwa mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford, 28, ambaye kwa sasa yuko huko kwa mkopo, lakini Manchester United wanashikilia msimamo. (Express)

Barcelona wamembaini beki wa kati wa Sporting, Ureno, Gonçalo Inacio, 24, kama wanaye mlenga ili kuimarisha ulinzi wao, lakini watahitaji kulipa euro milioni 70 (pauni milioni 60). (Fichajes - in Spanish)

Imefasiriwa na Asha Juma