Moja kwa moja, Wanafunzi wa Iran wafanya maandamano makubwa ya kwanza tangu ukandamizaji mbaya wa serikali uliosababisha vifo

Wanafunzi katika vyuo vikuu kadhaa nchini Iran wamefanya maandamano ya kupinga serikali, maandamano ya kwanza ya aina hiyo kwa kiwango hiki tangu ukandamizaji mbaya wa mwezi uliopita.

Moja kwa moja

Na Lizzy Masinga

  1. Familia Mpalestina mwenye asili ya Marekani aliyeuawa Ukingo wa Magharibi yadai uwajibikaji

    Mama wa Nasrallah Abu Siyam, mwenye umri wa miaka 19, anaomboleza kwenye mazishi yake siku ya Alhamisi.

    Chanzo cha picha, Ammar Awad via Reuters

    Familia ya kijana Mpalestina mwenye umri wa miaka 19 ambaye wanasema alipigwa risasi na mlowezi wa Kiisraeli katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu wametaka kuwajibika kuhusu mauaji yake.

    Nasrallah Abu Siyam alipigwa risasi karibu na mji wa Ramallah katika Ukingo wa Magharibi na kuwa takribani raia wa sita wa Marekani waliuawa na walowezi wa Kiisraeli au wanajeshi katika eneo hilo katika miaka miwili iliyopita.

    Utawala wa Trump ulisema uko tayari kutoa msaada wa kibalozi, lakini haukujibu madai kwamba sera zake zilishindwa kuzuia kuongezeka kwa ghasia za walowezi.

    Ubalozi wa Israeli huko Washington ulisema tukio hilo linapitiwa na "uchunguzi wa kiutendaji... lazima ukamilike haraka iwezekanavyo".

    Abu Siyam alikuwa raia wa Marekani aliyezaliwa Philadelphia.

    Familia yake ilisema alikuwa miongoni mwa takribani wakazi 30 wa kijiji cha Mukhmas ambao walikuwa wakijaribu kuwazuia walowezi wenye silaha kuiba mbuzi wao siku ya Jumatano.

    Wakati wakazi na walowezi wote wakirusha mawe, shahidi mmoja alisema, walowezi waliwapiga risasi takribani wanakijiji watatu, akiwemo Abu Siyam, ambaye alipigwa risasi na kuuawa.

    Abdulhamid Siyam, binamu wa Abu Siyam, aliiambia BBC kwamba kifo cha kijana huyo wa miaka 19 kilikuwa "hasara kubwa" na vitendo vya walowezi katika Ukingo wa Magharibi havikuwa vimedhibitiwa.

  2. Wanafunzi wa Iran wafanya maandamano makubwa ya kwanza tangu ukandamizaji mbaya wa serikali uliosababisha vifo

    Maandamano

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Wanafunzi katika vyuo vikuu kadhaa nchini Iran wamefanya maandamano ya kupinga serikali, maandamano ya kwanza ya aina hii kwa kiwango hiki tangu msako mbaya wa mwezi uliopita uliofanywa na mamlaka.

    BBC imethibitisha picha za waandamanaji wakiandamana kwenye chuo kikuu cha Sharif katika mji mkuu Tehran siku ya Jumamosi.

    Mapigano yalionekana baadaye yakitokea kati yao na wafuasi wa serikali.

    Maandamano yalifanyika katika chuo kikuu kingine cha Tehran, na mengine yaliripotiwa kaskazini-mashariki.

    Wanafunzi walikuwa wakiwaenzi maelfu ya wale waliouawa katika maandamano makubwa mwezi Januari.

    Marekani imekuwa ikijenga uwepo wake wa kijeshi karibu na Iran, na Rais Donald Trump amesema anafikiria kufanya shambulizi dogo la kijeshi.

    Marekani na washirika wake wa Ulaya wanashuku kwamba Iran inaelekea kuendeleza silaha ya nyuklia, jambo ambalo Iran imekuwa ikilikanusha kila mara.

    Maafisa wa Marekani na Iran walikutana Uswisi siku ya Jumanne na walisema kuwa maendeleo yalikuwa yamepatikana katika mazungumzo yaliyolenga kudhibiti mpango wa nyuklia wa Iran.

    Lakini licha ya maendeleo yaliyoripotiwa, Donald Trump alisema baadaye kwamba dunia itajua “katika siku 10 zijazo, huenda” kama makubaliano yatafikiwa na Iran au Marekani itachukua hatua za kijeshi.

    Unaweza kusoma;

  3. Habari za asubuhi, karibu katika taarifa zetu