Tetesi za soka Ulaya: Man Utd, Chelsea, PSG zinamtaka Baleba

Chanzo cha picha, Getty Images
Paris Saint-Germain wako tayari kushindana na vilabu vya Ligi Kuu England kama Chelsea, Manchester United na Tottenham kwa kutoa ofa ya pauni milioni 100 kwa kiungo wa Cameroon mwenye miaka 22, Carlos Baleba, kutoka Brighton & Hove Albion. (Fichajes)
Tottenham Hotspur wameonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji Mmrekani aliyewahi kuichezea Chelsea, Christian Pulisic (27), ambaye yuko tayari kurejea England akitokea AC Milan msimu huu wa joto. (Teamtalk)
Spurs wanatafuta kocha wa muda kabla ya kujaribu kumrejesha kocha wa Marekani, Mauricio Pochettino, baada ya Kombe la dunia baadaye mwaka huu. (Sun)
Manchester United wana matumaini makubwa kuwa beki wa England mwenye miaka 32, Harry Maguire, ataongeza mkataba wake Old Trafford zaidi ya mwisho wa msimu huu. (Teamtalk)
Kipaumbele cha Newcastle United katika dirisha la usajili wa majira ya joto ni kusajili mshambuliaji, huku klabu hiyo ikitazamia kumuuza Mjerumani mwenye miaka 23, Nick Woltemade, baada ya uhamisho wake wa rekodi ya klabu mwezi Agosti. (Football Insider)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa Poland mwenye umri wa miaka 37, Robert Lewandowski, atasubiri kuamua hatma yake hadi baada ya uchaguzi wa urais wa klabu mwezi Machi, huku akiwa na ofa kutoka AC Milan, Atletico Madrid, Chicago Fire, Fenerbahce na vilabu vya Saudi Arabia. (Mundo Deportivo)
Bologna wamempa mkataba mpya wa miaka minne na nusu mshambuliaji wa Argentina mwenye miaka 21, Santiago Castro, huku Chelsea, Everton na Aston Villa zikiwa miongoni mwa vilabu vilivyokuwa vinamfuatilia. (Football Italia)
Manchester United, Arsenal, Chelsea na Tottenham ni miongoni mwa vilabu vya Ligi Kuu vinavyomfuatilia kwa karibu kiungo wa Serbia mwenye miaka 20, Aleksandar Stankovic, wa Club Brugge. (Teamtalk)
Manchester United wanatarajiwa kutuma wawakilishi kumuangalia beki wa Ufaransa mwenye miaka 25, Pierre Kalulu, wa Juventus, katika mechi dhidi ya Inter Milan. (Tuttosport)
Manchester United pia wanamfuatilia beki wa Gambia mwenye miaka 19, Abubacarr Sedi Kinteh, wa Tromso, pamoja na beki wa kati wa Hispania mwenye miaka 18, Hugo Fernandez, kutoka Valencia. (Mail)















