Tetesi za soka Ulaya: Bayern, Chelsea zinapigana vikumbo kwa Verbruggen

Chanzo cha picha, Getty Images
Bayern Munich wanapanga kumsajili kipa wa Brighton, Bart Verbruggen (23), katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi. (Talksport)
Chelsea wako tayari kupambana na Bayern Munich kwa ajili ya Verbruggen na wako tayari kutoa pauni milioni 50 inayotakiwa na Brighton kwa ajili ya kipa huyo wa kimataifa wa Uholanzi. (Teamtalk)
Beki wa England wa Manchester City, John Stones (31), huenda akaondoka klabuni hapo majira ya kiangazi mkataba wake utakapomalizika, huku Bayern Munich wakionyesha nia ya kumsajili. (Caught Offside)
Atletico Madrid wanachunguza uwezekano wa kumsajili beki wa Chelsea na Hispania, Marc Cucurella (27). (Fichajes)
Aston Villa wanamwania kiungo wa England wa Nottingham Forest, Morgan Gibbs-White (26), lakini Forest wanaweza kutaka ada nono ya hadi pauni milioni 65. (TeamTalk)

Chanzo cha picha, Getty Images
Tottenham wanamuona beki wa Real Madrid na Ujerumani, Antonio Rudiger (32), kama mbadala wa Cristian Romero (27) iwapo beki huyo wa Argentina ataondoka na kujiunga na Real Madrid. (Fichajes)
Borussia Dortmund wanataka kumpa beki wa Ujerumani Nico Schlotterbeck (26) mkataba mpya, huku Real Madrid wakionyesha nia ya kumsajili. (Bild)
Aliyekuwa kocha wa Marseille, Roberto de Zerbi, anaweza kuwa tayari kuinoa Tottenham, licha ya awali kupendelea kusubiri nafasi ya kuifundisha Manchester United. (TeamTalk)
Nottingham Forest watajaribu tena kumsajili kiungo wa Celtic na Ubelgiji, Arne Engels (22), majira ya kiangazi baada ya kushindwa kumsajili mwezi Januari. (Football Insider)
Juventus na Inter Milan zinatarajiwa kuwania saini ya kipa wa Tottenham na Italia, Guglielmo Vicario (29), majira ya kiangazi. (Gazzetta)
Manchester United wanaonekana kuongoza katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Everton na Senegal, Iliman Ndiaye (25), majira ya kiangazi. (Teamtalk)
Newcastle United huenda wakamgeukia kiungo wa Roma na Italia, Lorenzo Pellegrini (29), iwapo watampoteza Sandro Tonali (25) majira ya kiangazi. (Football Insider)












