Tetesi 5 kubwa za Soka jioni hii: Man City kufumua kikosi, kuondoa 10 akiwemo De Bruyne

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester City inapanga kufanyia marekebisho makubwa kikosi chao msimu huu wa joto, kwa kuondoa karibu wachezaji 10 akiwemo Kevin De Bruyne anayekaribia kukamilisha uhamisho wa kwenda timu ya daraja la pili ya Saudia.
De Bruyne, nguli huyo wa Ubelgiji akitarajiwa kukamilisha uhamisho wa kwenda ligi ya daraja la pili Saudia na Neom, FootMercato inaripoti.
Mkataba wake na City unamalizika msimu huu wa joto, ambapo De Bruyne amevivutia vilabu vingi, huku River Plate, Galatasaray na Fenerbahce na klabu ya MLS ya San Diego, zikimfukuzia.
Lakini ni Neom SC inaonekana kuongoza kumnasa Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 baada ya Wamarekani wa San Diego kukiri kuwa hawawezi kumnunua.
Victor Osimhen aikataa Juve, aitaka EPL

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji Mnigeria Victor Osimhen ameikataa Juventus ili kuhamia kwenye Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) huku akitarajia uhamisho wa Euro milioni 75 kutoka Napoli hadi 'moja ya klabu kubwa za Ulaya' kukamilika katika msimu huu wa joto.
Ofa ya Juventus ilikataliwa na Victor Osimhen, ambaye anapendelea kuhamia 'moja ya vilabu vikubwa barani Ulaya' kwenye Ligi ya EPL msimu huu wa joto.
Victor Osimhen ametumia msimu wa 2024-25 kwa mkopo huko Galatasaray, lakini mshambuliaji huyo, aliye na mkataba na Napoli, atakuwa akitafuta uhamisho wa kudumu mahali pengine msimu huu wa joto.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka kwa JuveFC (h/t Football Italia), mchezaji huyo wa kimataifa wa Nigeria aliombwa na Juventus ili ajiunge nao kabla ya msimu wa 2025-26, lakini alikataa ofa hiyo na kupendelea kuhamia Ligi Kuu ya Uingereza.
Kane haitaki EPL

Chanzo cha picha, Getty Images
Nahodha wa England Harry Kane amepuuza tetesi za kurejea Ligi Kuu ya enlgand katika majira ya msimu wa joto, akisisitiza kuwa ana furaha sana Bayern Munich.
Alipoulizwa kama kuna sehemu alikuwa anafikiria kurejea england siku moja, Kane alisema: "Sina hakika. Nimesema katika maisha yangu yote mimi si mtu ambaye napenda kufikiria mbali sana.
"Najua mengi yanaweza kubadilika katika soka kwa muda mfupi na mambo yanaweza kutokea, lakini mwishowe macho yangu yako hapa (Bayern).
Asensio, Rashford kubaki Villa?

Chanzo cha picha, Getty Images
Kocha Unai Emery anaisukuma klabu yake ya Aston Villa kumsajili nyota wa zamani wa Real Madrid, Marco Asensio kwa ada mchekea ya Euro milioni 15 kutoka Paris Saint-Germain (PSG) huku mchezaji wa kimataifa wa Hispania akiwa katika kiwango bora toka ajiunge kwa mkopo katika timu hiyo ya Ligi kuu England.
Asensio alikosa namba chini ya Luis Enrique katika mji mkuu wa Ufaransa, na kusababisha kutolewa kwa mkopo kwenda Villa mwezi Januari, akiungana na Marcus Rashford aliyetokea manhcetser United, ambaye pia anatakwa kubakishwa na Villa baada ya kuonyesha kiwango kizuri.
Mshindi huyo mara tatu wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, ameimarika chini ya Emery kwa kufunga mabao manane katika mechi 10 pekee, haswa akifunga mabao yote mawili walipoilaza Chelsea 2-1 mwezi Februari kabla ya kufunga moja na kutengeneza jingine walipoilaza Brighton 3-0 Jumatano (goal.com).
Chelsea kumfukuzisha kazi Postecoglou Spurs?

Chanzo cha picha, Getty Images
Kocha wa Tottenham Ange Postecoglou hatma yake kusalia kwenye klabu hiyo iko kwenye ya Chelsea. Spurs inacheza na leo Alhamisi na kama itafungwa basi kocha huyo atakuwa wa kwanza wa Tottenham kupoteza mechi zake nne za kwanza za ligi dhidi ya The Blues na huenda akawa kwenye kuti kavu la kufukuzwa
Itakuwa takwimu nyingine mbaya kwa kocha huyo aliye kwenye shinikizo la kutimuliwa . Na mwenyewe Postecoglou anaamini kuna makocha 'bora' wanaoweza kuchukua nafasi yake ikiwa klabu itaamua kwenda 'mwelekeo tofauti.'
(Skysports).















