Liverpool ni suala la wakati, hivi ndivyo itakavyoweka rekodi na kutwaa ubingwa wa EPL

Darwin

Chanzo cha picha, Getty Images

    • Author, Emlyn Begley
    • Nafasi, BBC Sport journalist
  • Muda wa kusoma: Dakika 3

Liverpool inakaribia kuweka historia nyingine katika Ligi Kuu ya England. Ushindi wao wa bao 1-0 dhidi ya Everton jana usiku, umewarejesha kileleni kwa tofauti ya alama 12, huku msimu ukiwa unakaribia kumalizika. Swali sio tena ikiwa watatwaa ubingwa, bali lini watahitimisha safari yao ya mafanikio.

Safari ya Liverpool Kuelekea Ubingwa

Katika mechi yao ya Jumatano, Liverpool waliibuka na ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Everton kwenye Merseyside Derby. Matokeo haya yaliwarejesha katika nafasi ya kwanza kwa tofauti ya alama 12, baada ya Arsenal kupunguza pengo hadi pointi 9 siku moja kabla kwa ushindi wao dhidi ya Fulham.

Takwimu zinaonyesha kuwa Liverpool wana nafasi ya asilimia 99.2% ya kutwaa ubingwa msimu huu, huku Arsenal wakibaki na matumaini hafifu ya 0.8% pekee. Hii ina maana kuwa Liverpool wapo katika nafasi ambayo haijawahi kutokea kwa timu yoyote kwenye historia ya ligi kushindwa kiutwaa ubingwa ikiwa na alama hizo, muda na mechi zilizosalia.

Kwa sasa, kikosi cha Arne Slot kinahitaji alama 13 tu kati ya 24 zilizobaki ili kujihakikishia ubingwa. Hata hivyo, kwa sababu wana tofauti kubwa ya mabao dhidi ya Arsenal (+43 kwa +30), huenda wakahitaji alama 12 pekee kufanikisha lengo lao.

Ikiwa wataweza kushinda mechi nne kati ya zilizobaki, moja ikiwa dhidi ya Arsenal basi ubingwa utakuwa rasmi wa kwao.

Je, Liverpool wanaweza kuweka historia ya kutwaa ubingwa mapema zaidi?

Tarehe ya mapema zaidi ambayo Liverpool wanaweza kutangazwa mabingwa ni 20 Aprili, wakati watakapomenyana na Leicester City ugenini.

Hii inaweza kutokea ikiwa Arsenal watapoteza mechi zao mbili zijazo dhidi ya Everton na Brentford, huku Nottingham Forest wakishindwa kupata ushindi dhidi ya Aston Villa au Everton. Liverpool nao watahitaji kushinda dhidi ya Fulham na West Ham katika kipindi hicho.

Iwapo hali hiyo itatimia, basi sare pekee dhidi ya Leicester itawafanya mabingwa wa Ligi Kuu ya England kwa mara ya 20 katika historia yao.

Luis Diaz and Dominik Szoboszlai celebrate

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Liverpool Inakaribia kutwaa Ubinga wa EPL

Ratiba ya Mechi Zilizobaki kwa Liverpool

5 April: Fulham (A)

12 April: West Ham (H)

19 April: Leicester (A)

26 April: Tottenham (H)

3 May: Chelsea (A)

10 May: Arsenal (H)

18 May: Brighton (A)

25 May: Crystal Palace (H)

Liverpool na uwezekano wa kuweka rekodi mpya

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Ikiwa kila kitu kitaenda vizuri, Liverpool wanaweza kulingana na rekodi yao ya msimu wa 2019-20, ambapo walitwaa ubingwa wakiwa na mechi saba mkononi. Hata hivyo, wanaweza pia kuifikia rekodi ya Manchester United (2000-01) na Manchester City (2017-18) kwa kutwaa taji wakiwa na mechi tano mkononi.

Timu kama Manchester United (1999-2000 na 2012-13) na Arsenal (2003-04) ziliwahi kushinda ligi wakiwa na mechi nne mkononi, na Liverpool wana nafasi ya kujiweka kwenye orodha hiyo ikiwa wataendelea na kasi yao ya sasa.

Iwapo watatwaa taji hili, litakuwa mapema zaidi kuliko ubingwa wao wa 25 Juni 2020, ambao ulitokana na msimu uliocheleweshwa na janga la Covid-19.

Liverpool wanaweza pia kuweka rekodi mpya ya tofauti kubwa ya alama kati ya mabingwa na mshindi wa pili. Rekodi ya sasa inashikiliwa na Manchester City, waliomaliza msimu wa 2017-18 wakiwa na tofauti ya alama 19 dhidi ya Manchester United. Kwa sasa, Liverpool wanaweza kufikisha pointi 97, na ikiwa wataongeza pengo lao kwa alama 8 zaidi, wataweka rekodi mpya.

Kwa ujumla Liverpool iko mlangoni kuelekea kutwaa taji lao la pili la Ligi Kuu katika mika ya hivi karibuni. Timu hii imeonyesha uthabiti, uimara na uwezo wa kushinda mechi muhimu.

Huku msimu ukielekea ukingoni, mashabiki wa Liverpool wana kila sababu ya kuanza kusherehekea. Ni suala la wakati tu kabla ya Reds kushika rasmi taji lao la Ligi Kuu kwa mara ya 20.

Matokeo ya mechi za Jumanne na Jumatano ni kama ifuatavyo

Jumatano - April 02

AFC Bournemouth 1 , Ipswich Town 2

Brighton & Hove Albion 0 , Aston Villa 3

Manchester City 2 , Leicester City 0

Newcastle United 2 , Brentford 1

Southampton 1 , Crystal Palace 1

Liverpool 1 , Everton 0

Jumanne - April 03

Arsenal 2 , Fulham 1

Wolverhampton Wanderers 1 , West Ham United 0

Nottingham Forest 1 , Manchester United 0