Tetesi 5 kubwa za soka Jioni hii: Madrid kumuuza Vinicius Junior kwa €300mil

Chanzo cha picha, Getty Images
Real Madrid wako tayari kumruhusu Vinicius Junior kuondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto iwapo dau la Euro milioni 300 litawekwa mezani, kwa mujibu wa ripoti kutoka Uhispania.
Vilabu kutoka Ligi kuu ya Saudi Pro League, Saudi Arabia hasa Al-Ahli na Al-Nassr, zinasemekana kuwa ziko tayari kumpa Mbrazil huyo mkataba mnono wa kiwango sawa na Cristiano Ronaldo.
Kama Ronaldo atasaini mkataba mpya Al-Nassr utamfanya kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani akitengewa Euro milioni 183 (£154m/$188m) kwa mwaka, sawa na Euro milioni 15 (£12.6m/$15m) kwa mwezi au euro milioni 3.8 kwa wiki. (Football transfers)
Usajili wa arsenal utakuwaje dirisha la kiangazi?

Chanzo cha picha, Getty Images
Arsenal imemtangaza hivi karibuni Mkurugenzi wa mpya wa Michezo Andrea Berta, anayechukua nafasi ya Egu Gaspar aliyeondoaka miezi michache iliyopita. Skyport imechambua vipaumbele vyake.
1. Ni kuongeza mikataba ya wachezaji 10 waliopo, ambao mikataba yao iko chini ya miaka miwili, akiwemo nyota wake Bukaya Saka,Gabriel Jesus, Gabriel Martinelli, walinzi William Saliba na Mbrazil Gabriel Magalhaes huku viungo Thomas Partey na Jorginho wakisalia na miezi miwili tu.
2. Kusajili wachezaji wanne, Mshambuliaji wa kati mmoja mshambuliaji wa wa pembeni mmoja, kiungo wa kati. Winga wa pembeni Nico Williams, Mlinda mlango Garcia, kiungo Martin Zubimendi na mshambuliaji Viktor Gyokeres.
Sancho kurejea Dortmund?

Chanzo cha picha, Getty Images
Borussia Dortmund wanadaiwa kutaka kumsajili Jadon Sancho kwa mara ya tatu ili kuchukua nafasi ya Jamie Gittens ambaye huenda akaishia Chelsea.
Sancho kwa sasa yuko Chelsea akitokea Manchester United , akionekana na yeye kutaka kuondoka kurejea Dortmund, Klabu iliyompa jina na kumtambulisha kama mmoja wa chaezaji mahiri wa ushambuliaji, akitokea pembeni (The sun)
Thierno Barry mbadala wa Jackson Chelsea

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa upande wao Chelsea wameripotiwa kumtaka mshambuliaji anayechipukia wa La Liga, Thierno Barry ili kuziba nafasi ya Nicolas Jackson.
Licha ya kuwa miongoni mwa vilabu vitano kwa ushambuliaji kwenye kampeni ya ligi kuu mpaka sasa, safu ya ushambuliaji ya The Blues imekuwa butu katika miezi ya hivi karibuni.
Pamoja na Cole Palmer kuchemka katika ufungaji wa mabao, Jackson hakuwepo tangu mwanzoni mwa Februari kutokana na jeraha la misuli ya paja, limechangia kwa klabu hiyo kuyumba katika kufumania nyavu.
Chelsea sasa wanamtaa Msenegali huyo kuwasaidia, ambapo wako tayari kutoa kitita cha £33.43m kumnasa Barry. (Sportmole)
Madrid kuinyang'anya Arsenal tonge mdomoni?

Chanzo cha picha, Getty Images
Real Madrid wameripotiwa kumfanya kiungo wa kati wa Real Sociedad Martin Zubimendi kuwa nyota namba moja kwa wachezaji itakaowasajili katika dirisha la uhamisho wa majira ya joto.
Kiungo huyo inatajwa kukubaliana kila kitu na Arsenal tangu mwezi Januari, akisubiriwa kujiunga nao mwezi Juni, baada ya dirisha kubwa la kiangazi kufunguliwa.
Madrid tayari wameshamalizana na mlinzi wa Liverpool, Trent Alexander-Arnold ambaye ataelekea Hispania mwishoni mwa msimu huu (Skysport)














