Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Msichana anayewapenda marehemu na kuwapodoa
Isabelle Walton hutumia muda wake mwingi wa siku kuwa na miili ya wafu. Kazi yake ni kuwatayarisha wafu "kwa ajili ya kuagwa kwao mwisho." Isabelle anasema anajivunia kazi yake.
Meneja wakitengo cha kuhifadhi maiti akiwa na umri wa miaka 24
Kuna harufu isiyo ya kawaida katika chumba cha kuhifadhia maiti.
"Tuna uingizaji hewa hapa, lakini watu hawajazoea kemikali tunayozotumia hapa," anasema Isabelle. Ingawa sihisi harufu ya aina yoyote.
Kuwa meneja wa chumba cha kuhifadhia maiti sio kazi ya kawaida kwa kijana mwenye umri wa miaka 24.
"Watu wanashangaa ni kwa jinsi gani mimi ni kijana na mwanamke ninafanya kazi hapa, kwa sababu bado ni taaluma inayotawaliwa na wanaume," anasema.
Isabelle alianza kama mkurugenzi wa mazishi wa kampuni ya AW Lyman huko Nottingham nchini Uingereza mnamo 2019, lakini alialikwa na chumba cha kuhifadhia maiti cha kampuni hiyo.
Akiwa na umri wa miaka 21, alianza kufanya kazi katika chumba cha kuhifadhia maiti. Pamoja na hayo, pia aliendelea na masomo yake katika taaluma ya uhifadhi wa maiti.
Akiwa mdogo zaidi kwa umri, alidharauliwa katika alipokuwa shuleni, lakini familia yake daima ilimuunga mkono.
Hata hivyo, marafiki zake hawakufurahishwa na kazi yake ambayo waliiona ni ya ajabu.
Hofu ya kifo na utulivu
Wakati mtangazaji wa TV Stacey Dooley alipokabiliwa na hofu kuhusu kifo chake na kushuhudia mchakato wa kuhifadhi miili kwa msaada wa kemikali ili isioze , binti Isabelle alikuwa naye na kumuonyesha namna mwili unavyohifadhiwa na kuwekwa katika hali ya kupendeza.
Stacey Dooley ni mtangazaji wa televisheni ambaye hivi karibuni alitumia muda wake katika chumba cha kuhifadhia maiti cha BBC One na kujaribu kukabiliana na hofu yake ya kifo ambayo amekuwa akiishi nayo kwa muda mrefu.
Hata hivyo, Stacey mwenyewe anasema kuwa hofu yake ni "hofu isiyo isiyoweza kuepukika".
"Nataka kuishi milele, lakini pia naamini kuwa haiwezekani," anasema Stacey.
Hata hivyo Isabelle ana mtizamo tofauti kuhusu kifo. Anasema kuwa mbali na kuwa na hofu, kuzungukwa na maiti wakati wote kumemfanya ahisi kifo kuwa cha kawaida.
"Najua nitatunzwa ikiwa kifo kitatokea," anasema.
Kuanzia kusafisha mwili hadi kuupodoa
Kuna miili 80 katika chumba cha kuhifadhia maiti. Kila mmoja huhifadhiwa kwa wastani wa siku 15-20.
Isabelle anasema watu wengi wanafikiri kwamba mtu aliyekufa anawekwa tu kwenye jeneza kabla ya mazishi. Lakini ukweli ni kwamba muda mwingi hutumika kuandaa miili ili ndugu jamaa na marafiki zao waweze kuwaona wapendwa wao na kukaa nao kwa muda wakiwa katika hali nzuri kabla ya kuzikwa au kuchomwa.
Isabels husafisha miili ya wafu, kuwachana au kunyoa nywele zao, kuwavalisha na kuwapaka vipodozi( make-up)
"Kama mtu amekuwa mgonjwa na kuwa hospitalini kwa muda mrefu, familia familia kwa mfano isingependa kumuona akiwa na ndevu ndefu," anasema.
"Wanataka mpendwa wao kuonekana amevaa vizuri, ameogo na kuwa na muonekano kama wa siku zote."
Kuutunza mwili kwa kemikali
Isabelle na wenzake pia hupaka asilimia 65 ya maiti kemikali ya kuzuia kuharibika ili iendelee kuhifadhiwa kwa muda mrefu.
Isabel anasema kuwa familia nyingi pia zinaomba huduma fulani za ziada, kulingana na kifurushi cha mazishi.
Hizi ni pamoja na kuupa mwili rangi sahihi na "kuitengeneza upya" ili kuonekana kama mwanadamu aliye hai.
Hii hufanyika zaidi katika hali ambapo maiti huwekwa wazi wakati wa mazishi.
Kwa mujibu wa Isabelle, "Niliweka bidii katika kila kitu ninachofanya. Sidhani kama watu wanatambua ni kiasi gani cha umuhimu na huduma inayotolewa katika kazi hii."
Mchakato wa kusafisha mwili
Wakati wa mchakato huu, mwili husafishwa huku mdomo ukiwa umefungwa. Damu huondolewa na maji yenye harufu humwagika karibu na mwili.
Maji maji yote na gesi katika sehemu za mwili pia huondolewa na kubadilishwa na maji ya kemikali ya kuzuia mwili kuoza.
Utunzaji wa mwili kwa njia ya kemikali na marufuku katika baadhi ya dini na kwa kawaida hii hutokana na sababu ya kemikali zinazohusika.
Wakati mwingine, Isabel anapaswa kuufanyia kazi zaidi mwili wa marehemu pale anapokufa kutokana na majeraha mfano ya ajali au kuungua kwa moto.
Kwa matukio kama haya mwili wa marehemu ulioharikika huondolewa kwenye na kisha mwili bandia hupachikwa kwenye mwili wake kipodozi maalumu cha nta ili awe na muonekano bora kwa jamaa zake na watu wake kwa ujumla watakaomtazama.
"Sio kama ' vipozi vya watu hai,' lakini tunatumia vipodozi vinavyotumika kwa maiti katika chumba cha kuhifadhia maiti, kwa hivyo vipodozi hivi vinakuwa na muongekano mzuri na kuweza kudumu kwenye ngozi baridi ya maiti," anaelezea Isabelle.
Changamoto ya kubadilisha mawazo ya jamii
Disemba hadi Machi katika majira ya baridi ni wakati wa shughuli nyingi kwa wakurugenzi wa mazishi kwani idadi kubwa ya vifo hutokea wakati huu.
Lakini kwa sasa katika chumba cha kuhifadhia maiti, Isabel anabeba miili mitatu hadi minne kwa siku.
"Hakuna madirisha ya kutosha katika chumba cha kuhifadhia maiti," alisema. "Wakati pekee ninapoona jua ni wakati ninapoenda kujitengenezea kahawa."
Kutembelea familia zenye huzuni kunaweza kuwa na hisia, lakini wanajaribu y hujaribu kuzingatia kazi yake zaidi, anasema.
Kwa mujibu wa Isabelle, "Bila shaka unapaswa kujaribu kuwafariji na sio wao kukufariji."
Anasema anataka kuzuia mtizamo hasi dhidi ya kazi zao - iwe ni kufanya kazi katika chumba cha kuhifadhia maiti au kuhudhuria mazishi.
Wanapoombwa kufanya kazi hii , mara nyingi hujipata ni wanawake pekee, lakini katika mazishi ya hivi karibuni wanawake wanne walijiunga na kazi ya kumazishi.
"Familia ya marehemu haikuwahi kuona kitu kama hiki hapo awali. Marehemu angefurahi kumuona akifanya kazi hii kama mwanamke mwenye nguvu, na anayejisimamia," anaeleza Isabelle.