Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Je unaifahamu mbinu mpya ya uchomaji wa maiti kwa kutumia maji?
Wakati Askofu Mkuu Desmond Tutu, mwanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi wa Afrika Kusini na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel alipofariki dunia karibu miaka miwili iliyopita, kile ambacho mtu huyu muhimu alikuwa ameamuru kwa mara ya mwisho Ili kuwa mfano kwa ulimwengu kufuata ni . kuchomwa kwa mwili wako kwa kutumia maji (aqua cremation), mbinu mpya ya usimamizi wa mazishi ambayo ni rafiki zaidi kwa mazingira.
Siku hizi, makampuni ya kibinafsi yanaanza kutoa huduma za uchomaji wa maiti kwa kutumia maji katika nchi nyingi. Hii inajumuisha Marekani, Canada, Mexico, Australia, Afrika Kusini, na baadhi ya nchi za Ulaya. Lakini bado haijajulikana sana, hii ni kwa sababu ni ghali na watu hawajazoea mazishi zaidi ya yale ya kawaida na uchomaji wa maiti.
Ingawa ujumbe unasema "Kuchoma kwa maji" ni kinyume kabisa. Lakini mchakato huu unaweza kuozesha mwili wa marehemu kwa urahisi na haraka kama kuchoma kwa moto. Pia hausababishi uchafuzi wa hewa au kuongeza utoaji wa kaboni unaosababisha ongezeko la joto duniani.
Kwa kweli, uchomaji maiti au uchomaji wa maiti kwa kutumia maji ni mchakato wa kuozesha maiti kwa kutumia mmenyuko wa kemikali unaoitwa "alkali hidrolisisi" au kuozesha tishu katika mwili na moto ambao una athari kali ya alkali.
Mwili wa marehemu huwekwa ndani ya tanuru ya chuma kabla ya kupelekwa kwenye maji ya moto yaliyochanganywa na alkali kama vile hidroksidi ya potasiamu au hidroksidi ya sodiamu 5%, ambayo huwachwa kutirrika juu ya mfu.
Iwapo jamaa za marehemu watachagua mbinu ya kuchoma na maji kupitia joto la chini , joto la maji hayo litadhibitiwa ili kutofikia kiwango cha juu cha maji hayo kuchemka. Hii itasababisha maiti kuoza polepole hadi tishu zote ziondoke ndani ya saa 14-16.
Lakini iwapo utachagua njia ya kuchoma maiti kwa maji ya joto la kiwango cha juu cha hadi nyuzi joto 160 huku shinikizo likiongezeka ndani ya tanuru,hii itaharakisha kuoza kwa mwili wa maiti kwa kati ya saa 4-6 pekee.
Mchanganyiko wa alkali huvunja bondi za kemikali za tishu mbalimbali katika mwili wa binadamu, hadi mifupa itakaposalia katika mfumo wa Kalsiamu safi ya phosphate , ambayo inaweza kusagwa na kuwa unga kuwapa jamaa .
Haina tofauti na majivu ya mifupa yanayotokana na kuchomwa kwa moto. Kwa sababu inaweza kutumika kwa sherehe ya mwisho au kuitawanya mahali ambapo marehemu alitaka itawanywe.
Mchanganyiko wa maji yaliosalia baada ya uchomaji huo, humwagwa katika mfereji wa maji chafu bila kuathiri mazingira.
Mchanganyiki wa kemikali unaotumika kwa mara ya kwanza uligunduliwa na Uingereza katika karne ya 19 ili kuwasaidia wakulima kuozesha mabaki ya wanyama yasiohitajika.
Kilichopatikana kutokana na mchakato huo ni gundi na gelatin.
Athari ya kemikali ilitumika baadaye katika miaka ya 1980 na 1990 kusafisha mabaki ya ng'ombe waliokufa kutokana na ugonjwa wa kichaa cha ng'ombe (BSE), na katika shule za matibabu kusaidia kwa ajili ya utafiti.
Awali kulikuwa na makampuni ya kibinafsi nchini Marekani yaliotengeneza mahali pa kuchomea maiti kwa ajili ya huduma za kuchoma maiti kwa umma kwa mara ya kwanza mwaka 2011.
Uingereza imeruhusu watu kutumia uchomaji maiti wa kutumia maji mwishoni mwa mwaka, kulingana na Co-op Funeralcare, mtoa huduma mkuu wa mazishi wa Uingereza. Hii itasaidia kufanya uchomaji wa maiti kwa kutumia maji kuwa wa bei nafuu. Mbinu hii imekuwa maarufu zaidi kama mbadala kwa kizazi kipya kinachojali mazingira.