Uingereza yatafiti mipango ya kuchora upya ramani ya Gaza

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Nyaraka za Uingereza zinaonyesha kwamba serikali ya nchi hiyo imetafiti mipango kadhaa ambayo ni pamoja na kuunganisha sehemu ya Sinai, Ukanda wa Gaza, visiwa vya Tiran na Sanafir, na sehemu ya Jordan ili kuunda eneo salama kati ya Misri na Israeli, ndani ya mfumo wa kutatua mgogoro kati ya Misri na Israel na kuondoa kikwazo chochote kinachozuia upatikanaji wa mafuta kutoka Mashariki ya Kati hadi Magharibi.

Miradi hii ilipendekezwa baada ya kushindwa kwa vita vya pande tatu kati ya Uingereza, Ufaransa na Israel dhidi ya Misri katika kukabiliana na kutaifishwa kwa Mfereji wa Suez na aliyekuwa kiongozi wa Misri Gamal Abdel Nasser mnamo Julai 26, 1956, katika kile kilichojulikana kama Mgogoro wa Suez.

Baada ya kumalizika kwa vita vilivyoshindwa, mnamo Novemba 11, 1956, Israeli ilisita kujiondoa kutoka Sinai, lakini ililazimishwa kuondoka chini ya shinikizo la kimataifa mnamo Machi 1957.

Je, eneo hilo litasimamiwa na kulindwa vipi?

Utawala huo utakuwa wa kimataifa, utakaotekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa, na kuwasilisha ripoti ya mwaka kwa Mkutano Mkuu wa Shirika hilo.

Kwa ajili ya usalama, mpango ulipendekeza kuundwa kwa kikosi cha kiraia ambacho kingefurahia uungwaji mkono wa Umoja wa Mataifa, au kuungwa mkono na wengi kutekeleza mamlaka katika eneo hilo.

Kikosi hiki hakina silaha isipokuwa kufikia malengo ya polisi au kukusanya mapato.

Vyanzo vya ufadhili ni vipi?

Shirika litakalochaguliwa kwa usimamizi litapewa mikopo iliyotolewa na wakopeshaji wakuu ambao watafaidika na "Mradi wa Sinai", hadi eneo hilo litakapoanza kufanya kazi na kuweza kujikimu kifedha.

Makampuni ya mafuta ya Ulaya na Asia yanayofaidika yanashiriki katika ufadhili huo.

Mradi huo ulitarajia kuwa ada zinazolipwa na makampuni zingetosha kufadhili mahitaji ya usimamizi na bima.

Je, Misri inaweza kukubali mradi huo?

Monorio, mkuu wa idara ya Mashariki ya Kati huko, The Economist, mnamo Desemba 13, 1956, ambayo ni, karibu miezi 3 kabla ya kujiondoa kwa Israeli kutoka Sinai aliweka dau kuhusu hitaji la Misri la pesa kwa miradi ya maendeleo.

Alisema, "Kukataa kwa Misri fedha kutaweka serikali yake katika makabiliano na watu ambao wanaamini kuwa rasilimali zao zinapaswa kutumika katika maendeleo na anasa na si kwa matukio ya maisha ya kusisimua kuvuka mipaka."

Aliongeza kuwa Israel ina msimamo huo huo, akibainisha kuwa kuanzisha eneo salama kati yake na Misri kutapelekea "kupunguza bajeti ya kijeshi kwa kiwango kinacholingana na rasilimali za ndani na mipango ya maendeleo.

Vipi kuhusu Saudi Arabia?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Mradi huo ulitarajia kwamba Ufalme huo utakuwa nchi ya Kiarabu iliyo tayari zaidi kukubali kuanzishwa kwa "Ukanda wa Sinai," kwani "itaiwezesha kuanzisha bomba la Saudi ambalo litasafirisha mafuta ya Saudi hadi Mediterania, ambayo itaokoa muda na pesa.”

Monorio alisema kuwa mpango huo utatoa "soko kwa gesi asilia ya Saudi na Kuwait," na alitarajia kwamba "hii pia ingevutia" nchi hizo mbili.

Katika kutetea muda wa kuwasilisha mpango huo kabla ya Israel kuhamisha Sinai, mwandishi wa Uingereza alisema, "Utekelezaji utakuwa mgumu zaidi mara ardhi (rasi ya Sinai) itakaporejea mikononi mwa Misri."

Je, eneo hilo litaanzishwaje?

Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa huunda muungano wa kununua ardhi, kisha kuunda shirika la kuendeleza eneo hilo.

Muungano huu utaipa Misri pauni milioni 300 kuisaidia kiuchumi, chini ya usimamizi wa wataalamu kutoka Umoja wa Mataifa, na utalipa kiasi hicho kwa kipindi cha miaka 20.

Nani anaendesha eneo hilo?

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anafanya usimamizi kupitia shirika la lilioanzishwa na muungano utakaonunua ardhi hiyo. Shirika hilo halitaku wa la kifaida, na lazima lilipe pesa hizo kwa nchi zinazoshiriki katika muungano, na pesa zozote zilizokusanywa baadaye kuhamishiwa kwa Umoja wa Mataifa.

Shirika la kimataifa lina majuku gani?

Umoja wa Mataifa hulipatia Shirika hilo wataalamu na kutoa mafunzo kwa wakazi wa eneo hilo la Kiarabu katika eneo lote, kwa lengo la kufikia yafuatayo: kuanzisha vinu 3 vya nishati ya nyuklia huko Al-Arish (kwenye Bahari ya Mediterania kaskazini mashariki mwa Sinai), Nakhl (katikati ya Sinai) na Sharm El-Sheikh katika Ghuba ya Aqaba, wakitekeleza miradi muhimu ya umwagiliaji maji, na kilimo cha mazao na matunda, uchunguzi wa mafuta, kuondoa chumvi kwenye maji, kutekeleza kampeni ya upandaji miti, ujenzi wa nyumba na miradi ya biashara katika sehemu zilizochaguliwa za mkoa.

Mradi huo unatoa umuhimu wa pekee kwa ujenzi wa mfereji mpya wenye urefu wa kilomita 75 unaoanzia Al-Arish hadi Gilat, ulioko magharibi mwa Jangwa la Negev kusini mwa Israel.

Udhibiti utafanyika vipi?

Chombo cha udhibiti kitakuwa kikosi cha polisi cha Umoja wa Mataifa chenye kazi za kipolisi katika:

* Ukanda wa upana wa kilomita 10 pande zote za mpaka kati ya Negev katika Israeli na Sinai.

* Upande wa magharibi wa Ghuba ya Aqaba, kutoka Gilat katika Israeli hadi Sharm El-Sheikh, na hii inajumuisha eneo la kilomita 10 kuzunguka jiji la Aqaba.

* Eneo lenye upana wa kilomita 10 kwenye kingo zote mbili za mfereji unaopendekezwa unaounganisha Gilat na Arish.

* Eneo lenye upana wa kilomita 10 kwenye kingo zote mbili za Mfereji wa Suez, liwe tayari kudhibiti mfereji huo endapo kutatokea uhasama ili kuhakikisha meli za nchi zote zinapita bila malipo kupitia Mfereji wa Suez.

* Kwa mujibu wa mradi huo, jeshi la polisi litazuia kupitishwa kwa silaha zozote kupitia au katika eneo la salama, na jeshi la Umoja wa Mataifa litafanya kazi iliyopewa kwa angalau miaka 10, na baada ya hapo litakuwa chini ya Umoja wa Mataifa.

Je, hali ya Mfereji wa Suez itakuwaje?

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kama ilivyoelezwa katika mradi huo, mfereji uko magharibi mwa eneo salama linalopendekezwa.

Misri itapokea ada za trafiki "mradi tu inadhibiti mfereji kwa mujibu wa mipango ya Umoja wa Mataifa."

Nyaraka hizo zinaonyesha kwamba Ofisi ya Mambo ya Nje ya Uingereza ilipitia kwa makini mpango huo.

Katika mjadala kuhusu hilo, Roberts, kutoka Idara ya Masuala ya Mashariki ya Ofisi ya Mambo ya Nje ya Uingereza, alimweleza Mbunge Wadd, katika mkutano wa moja kwa moja, kuhusu msimamo wa serikali kama ifuatavyo:

Kwanza: Tuna shaka sana kwamba Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu iko tayari kuacha umiliki wa eneo la (Sinai).

Pili: Ni hakika kwamba Jamhuri ya Kiarabu haitakuwa tayari kuruhusu Ukanda wa Gaza kuwekwa chini ya udhibiti wa shirika la kimataifa, licha ya udhibiti wa Israel.

Tatu: Wakati ufaao, mipango itabidi ifanywe kushughulikia matatizo tata ambayo sasa ni mada ya mzozo kati ya Israel na nchi za Kiarabu.

Nne: Hii haimaanishi kwamba hatupendezwi na mipango ya kushughulikia mustakabali wa kisiasa na kiuchumi wa eneo hili, ambalo ni uwanja wa operesheni za kijeshi.

Eneo linaundwaje?

Kulingana na mradi huo, Umoja wa Mataifa unanunua ardhi inayolengwa chini ya mfumo wa wa Israel, Misri na Jordan.

Mahakama ya Kimataifa ya Haki ina jukumu la kukadiria bei ya ardhi na kusambaza bei sawa kati ya nchi hizo tatu

. Njia ya reli inapanuliwa kutoka bandari ya Gaza hadi mji mkuu wa Jordan, Amman. Kwa hivyo, unapata ufikiaji wa Bahari Nyeupe.

Kuhusu kupanua njia hadi Bahari Nyekundu karibu na Aqaba, itaipa Israeli ufikiaji kupitia reli hadi Bahari Nyekundu, ikipitia ukanda mpya wa Umoja wa Mataifa

Je, nchi zingine zinaweza kufaidika na mradi huo?

Pendekezo la mradi huo lilionyesha matumaini yake kwamba reli ya Gaza-Amman ingeenea katika jangwa hadi Rutba nchini Iraq na kuenea ndani ya nchi hadi Ramadi, kisha hadi Baghdad, kisha hadi kwenye maeneo ya mafuta huko Kirkuk.

Upanuzi huu utaipa Iraq nafasi ya kusafirisha mafuta kupitia Bahari ya Mediterania, na itapunguza sana safari ya sasa ya usafirishaji, ambayo iko hadi Basra, kisha Ghuba hadi Mfereji wa Suez.