Ni nini kinachojulikana kuhusu familia ya kwanza ya watu wa Kale katika historia?

Katika miaka ya hivi karibuni, Ushahidi zaidi umepatikana kuhusu watu wa zamani Neanderthals, spishi ya binadamu ilioishi takriban miaka 430,000 iliopita hadi miaka 40,000.

Lakini mabaki hayo yaliotathminiwa ni ya watu binafsi na uhusiano kati yao bado haujabainika.

Kundi la wanasayansi kwa mara ya kwanza limefanikiwa kutambua familia za Neanderthernals kutokana na mabaki yaliopatikana katika mapango mawili nchini Siberia.

Matokeo hayo , yaliolezewa katika kifungu kimoja katika jarida la Asilia, lilichapishwa na watafiti katika Taasisi ya Max Planck for Evolutionary Biology mjini Leipzig, Germany.

Kazi hiyo iliongozwa na Svante Pääbo, ambaye alipokea Tuzo ya Nobel ya Tiba mwaka huu kwa kazi yake kuhusu DNA ya watu wa kale.

Miongoni mwa watu 13 ambao mabaki yao yalitathminiwa , wanasayansi waligundua baba na mwanawe wa kike Pamoja na mahusiano mengine.

Utafiti huo ulitoa mwangaza kuhusu jinsia jamii za watu wa kale walifanya kazi zao pamoja na jukumu la wanawake.

Je mabaki hayo yalipatikana wapi?

Mabaki ya mifupa hiyo na meno yalipatikana katika mapango mawili kwa jina Chagyrskaya na Okladnikov, katika milima ya Siberia na ina takriban miaka elfu hamsini na nne iliopita .

Mapango hayo yanapatikana sehemu ya mashariki kabisa ya eneo linalojulikana la Neanderthals, ambao waliishi sehemu za magharibi mwa Eurasia.

Nasaba nyingine ya binadamu iliyotoweka, Denisovans, yalikuwa sehemu za mashariki mwa Eurasia.

Usambazaji wa kijiografia wa Neanderthals ulikuwa mpana sana, kutoka pwani ya Ureno hadi Siberia ya magharibi, na kutoka kaskazini mwa Ulaya hadi peninsula ya kusini. Hadi sasa hakuna mabaki yaliyopatikana barani Afrika na inaaminika kuwa hawakuishi katika bara hilo.

Mapango hayo yanapatikana takriban kilomita 100 kutoka mahali ambapo mabaki ya awali ya Denisovan yalipatikana, lakini utafiti haukupata ushahidi wa kuzaliana. Aina zetu zilikuwa bado hazijafika eneo hili wakati huo.

Je ni kiwango gani cha uhusiano kilichogundulika

Watu 13 wa Neanderthal walijumuisha watoto watano na vijana. Kulikuwa na wanaume saba na wanawake sita.

Eneo la pango la Chagyrskaya lilitoa mabaki ya baba mtu mzima na binti yake tineja, ambaye anaaminika kuwa katika ujana wake.

Pia kulikuwa na mvulana wa kati ya umri wa miaka 8 na 12, pamoja na jamaa wa kike ambaye, kulingana na matokeo ya chembe za DNA , alikuwa shangazi, binamu, au bibi.

Wanasayansi walipata zana nyingi za mawe na mifupa ya wanyama kwenye mapangohayo.

Vitu hivi vinapendekeza kwamba Neanderthal waliokaa kwenye mapango haya waliishi katika jamii ndogo za wawindaji wa watu 10 hadi 20, wakila nyati, mbuzi wa milimani, na wanyama wengine.

"Utafiti wetu unatoa picha halisi ya jinsi jumuiya ya Neanderthal ingeweza kuonekana. Na hiyo inawafanya waonekane kuwa wanadamu zaidi kwangu," alisema mwanajenetiki Benjamin Peter wa Taasisi ya Max Planck ya Anthropolojia ya Mabadiliko, mmoja wa waandishi wa utafiti huo.

"Walikuwa watu ambao waliishi na kufa katika vikundi vidogo vya familia, pengine katika mazingira ya uhasama. Hata hivyo, waliweza kuvumilia kwa mamia ya maelfu ya miaka."

Ni nini kinachojulikana kuhusu wanawake

Jumuiya iliyochambuliwa inaonyesha kiwango cha chini cha anuwai ya maumbile, sawa na ile inayotokea kwa spishi zilizo katika hatari ya kutoweka, ambayo inaonyesha ukubwa mdogo wa vikundi.

Watafiti walilinganisha utofauti wa kijeni kwenye kromosomu Y, ambayo hurithiwa kutoka kwa baba hadi kwa mwana, na utofauti wa DNA ya mitochondrial, iliyorithiwa kutoka kwa mama.

Kuangamia

Neanderthal walikuwa na umbo nene kuliko Homo sapiens na nyusi kubwa zaidi.

Tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa waliunda sanaa, walitumia njia ngumu za uwindaji wa vikundi na walikuwa na vitu vya mfano.

Katika pango la Gorham huko Gibraltar, kwa mfano, muundo wa kufikirika uliofanywa na Neanderthals wenye mistari iliyovuka iliyochongwa kwenye mwamba ulipatikana.

Mwingiliano kati ya Neanderthals na spishi zetu sio moja kwa moja kabisa.

Kuzaliana kunajulikana kuwa kulitokea, kama inavyothibitishwa na ukweli kwamba idadi ya watu wasio Waafrika wa kisasa wana DNA ya Neanderthal iliyobaki.

Lakini ni jukumu gani Homo sapiens ilichukua katika kutoweka kwa Neanderthals, ambao, kama Denisovans, walitoweka mara tu baada ya spishi zetu kufika katika eneo lao bado inajadiliwa.