Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Je lini mwanamke mjamzito anafaa kufanya mazoezi ya mwili ni lini hapaswi?
Wanawake wanafaa kutembea wakati wa ujauzito ? Je wanaweza kutembea wakati wa ujauzito?
Wanawake wajawazito na familia zao hukabiliana maswali mengi ya aina hii.
Majirani na ndugu hutoa ushauri mbali mbali kuhusu hili na wakati mwingine ushauri unaotolewa huwachanganya zaidi akinamama wajawazito. Lakini je mwanamke mjamzito anapaswa kufanya mazoezi?
Je mwanamke mjamzito anapaswa kufanya mazoezi?
Kulingana wataalamu wa Idara ya kudhibiti na kuzuia magonjwa nchini Marekani wanashauri kwamba wanawake wanapaswa kufanya mazoezi mepesi ya mwili kwa mud awa dakika 150 au mazoezi ya viungo aerobics kwa wiki wakati na baada ya ujauzito.
Wakati na baada ya ujauzito, wanawake wanapaswa kutembea kwa miguu kwa kuinua kisigino , na kufanya shughuli hii kila siku.
Wanawake ambao walikuwa wakifanya mazoezi kabla ya ujauzito wanapaswa kuendelea.
Shirika la afya duniani WHO, linasema pia kwamba wanawake wanapaswa kufanya mazoezi rahisi au kutembea kwa dakika 150 wakati wa ujauzito.
Mazoezi ya kadri yanaweza kusaidia kupunguza , na hata kuzuia kabisa , pre-eclampsia(hali ya kiafya inayowapata baadhi ya wanawake wajawazito inayosababisha shinikizo la damu na kuongezeka kwa protini kwenye mkojo kunakoweza kuharibu figo) , kisukari, kuongezeka kwa uzito wa kupindukia wa mwili , matatizo wakati wa kujifungua, na huzuni baada ya kujifungua.
Mazoezi ya kadri huwa hayana athari mbaya kwa uzito wa mwili wa mtoto au kuongeza hatari ya kifo.
Kiligana na ripoti ya jarida la India, ’’Chuo cha Madaktari bingwa wa uzazi wa wanawake cha marekani kinashauri kuwa maozezi ya mama mjamzito yanapaswa kuwa ya dakika walau 20 hadi 30 .
Kwa kufany amazoezi hayo wanawake wajawazito hupunguza hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari, kujifungua mapema, kupunguza shinikizo la damu linalowapata mara kwa mara akinamama wajawazito (pre-eclampsia), na pia hupunguza uwezekano wa mama kufanyiwa upasuaji wakati wa kujifungua (CS)
“Kufanya mazoezi wakati wa ujauzito huongeza uwezekano wa mama kujifungua kwa njia ya kawaida ”
Daktari wa uzazi wa wanawake Bina Shah anasema, "Wakati wa ujauzito wanawake hawapaswi kufanya mazoezi kama vile kuruka juu, kukimbia, lakini wanapaswa kutembea kila siku .
Mwanamke mwenye matatizo ya kutoka damu wakati wa ujauzito wake au iwapo mfuko wa uzazi umeshuka chini hapaswi kutembea .”
“Wanawake wenye mimba za mapacha au watoto zaidi hawapaswi kwenda nje kutembea .
Wanawake ambao waliwahi kuwa na tatizo la kutoka kwa mimba kabla ya kujifungua pia hawapaswi kufany amazoezi ya kutembea .”
"Viatu na mavazi vinapaswa kuzingatiwa wakati wanapotembea, haupaswi kuvaa nguo kubwa au kuvaa viatu vyenye kisigino kirefu, vaaviatu vya michezo tu." anashauri.
“Mwanamke mjamzito anapaswa kutembea kandio ya barabara, katika njia ambayo haina mashimo , maji, na katika eneo lenye hewa safi . Bustani ni mahala bora pa kutembea kwa mwanamke mjamzito.
Aidha anasema , “Kutembea huufanya mwili kuwa wenye mkakamavu na huboresha mzunguko wadamu . Mazoezi ya kutambaa hayasababishi kuvimba kwa miguu.”
"Mwanamke mkakamavu zaidi wakati wa ujauzito ana uwezekano mkubwa wa kujifungua kwa njia ya kawaida."
'Fanya mazoezi kwa dakika 20 hadi 30 kila siku ‘
Dkt. Shiksha Gupta anasema , “Wanawake wanapaswa kutembea na kufanya mazoezi kwa muda wa dakika 20 -30 . Mazoezi humfanya mwanamke kuwa mkakamavu , kwahivyo hawezi kuwa na matatizo wakati wa kujifungua."
“Wakati wa ujauzito madaktari huwashauri wanawake kufanya aina fulani za mazoezi . Epuka kufany amazoezi wa kutazama video kwenye You Tube, ni hatari. Unafaa kupata ushauri kwa daktari wa viungo (Physiotherapist).”
Mtaalamu wa afya ya uzazi wa wanawake katika Kituo cha afya cha Allantis Healthcare, mjini New Delhi, Manan Gupta anasema, “Mazoezi haya humsaidia mwanamke kuufany amwili wake kuwa mkakamavu na pia kuuandaa mwili wake kwa ajili ya uchungu wa kujifungua na tendo lenyewe la kujifungua .”
Huku kujifungua kwa njia ya upasuaji hupunguza hatari ya kujifungua watoto wenye uzito wa mwili mdogo au kujifungua mapema.
Zaidi ya hayo mazoezi pia yanaweza kusababisha faida nyingi za afya kama vile kuzuia maumivu ya mgongo, kiungulia na kufura kwa tumbo, kuvimba mwili hasa miguu na uchovu . Husaidia pia wanawake kupata usingizi”, wanasema wataalamu.