Je, tunakula tu tunapohisi njaa?

Chanzo cha picha, Getty Images
Onur Erim
BBC
Uhusiano wetu na chakula ni mgumu, na mara nyingi sio wa kiafya.
Je, umewahi kujikuta ukkial vitafunio kwa ajili ya kujifurahisha tu, hata baada ya kula chakula chenye afya na cha kutosha? Huenda haya ni mazoea ya kula ambayo wataalamu huyaita “kula ili kujifurahisha.”
Wanasayansi wanaeleza wazo hilo kuwa “kula kusikochochewa na njaa bali kwa tamaa ya kula vyakula kwa kusudi la kujifurahisha,” mazoea ya kula ambayo yameitwa “hedon,” neno la Kigiriki linalomaanisha raha, Hedone, yaani mungu wa furaha katika imani ya kufikirika ya Kigiriki.
Ingawa kuna kiwango fulani cha raha karibu kila wakati tunapokula, ulaji wa "hedonic" yaani, wakati hatuhitaji kalori, mara nyingi huhusishwa na jamii ambazo zina urahisi wa kupata chakula na zenye njaa ni ndogo.
"njaa ya raha" ni nini?
Miili yetu hutumia nishati ya chakula, au kalori tunazopokea kutoka kwenye vyakula na vinywaji tunavyotumia.
Tunapochoma kalori zaidi kuliko tunavyokula, miili yetu hutenda kwa kutoa hisia ya kuongezeka kwa hamu ya chakula mfumo unaouambia ubongo wetu wakati hauna kitu, unaojulikana kama "njaa ya kimwili."
“Karibu kila mtu ana mazoea ya kula yenye kupendeza, na kila mtu ana tabia zinazoelekezwa na malengo zinazochochewa na raha,” asema James Stubbs, profesa wa hamu ya kula na uwiano wa nishati ya mwili katika Chuo Kikuu cha Leeds nchini Uingereza “Watu wengine hufurahia chakula kuliko wengine .”
Stubbs aongeza kwamba mbali na raha, mazoea yetu ya kula mara nyingi yanahusiana na mambo mengine, zikiwemo hisia-moyo na kukosa usumbufu ambao “huondoa utofauti kati ya njaa ya kimwili na njaa ya kukosa usingizi.”

Chanzo cha picha, Getty Images
Lakini je, sahani kubwa ya majani mabichi, kabichi iliyokatwakatwa, inaweza kutosheleza hitaji letu tunapohisi kutaka kula kwa ajili ya kujifurahisha tu? Hapana, si hasa!
"Kwa kawaida tunapata vyakula vyenye mafuta mengi, chumvi na sukari kuwa na manufaa kwa sababu vinaonyesha vyanzo vyema vya nishati," anasema Dk Bethan Meade, mhadhiri na mtafiti katika Kikundi cha Utafiti wa Hamu ya kula and Unene wa mwili wa kupindukia katika Chuo Kikuu cha Liverpool.
Lakini anaongeza kuwa kuna sababu nyingine zinazotufanya tuvutiwe na aina hii ya ulaji, na anasema, “Tunavutiwa na vyakula hivi kwa sababu ya nishati na raha vinavyotoa wakati wa kuvila, na inaweza kuwa vigumu kutofautisha kati ya vyakula hivyo, motisha nyuma ya vyakula hivi , ni njaa ya raha au hisia ya kibaolojia ya njaa ya mwili.

Chanzo cha picha, Getty Images
Pia, wingi wa vyakula hivyo vyenye mafuta mengi, chumvi na sukari pia unaonekana kuwa moja ya sababu zinazopelekea kufurahisha katika ulaji.
Ulaji wa vyakula visivyofaa kwa kuchochewa na tamaa ya raha umehusishwa na kunenepa kupita kiasi.
"Sasa tumezungukwa na wingi wa vyakula vitamu, vinavyopatikana kwa urahisi na vilivyo tayari kuliwa," asema profesa wa usawa wa nishati Profesa James Stubbs "Hii inakuwa kichocheo cha unene na unene kupita kiasi katika jamii ya kisasa."
Kulingana na Stubbs, haishangazi kwamba mtu mmoja kati ya wanane Duniani kwa sasa anaugua maradhi ya unene wa kupindukia.
Tunaweza kufanya nini?
Kinadharia kunaweza kuwa hakuna kitu kibaya kinachotokana na kula kwa raha, kulingana na wataalam, kwa sababu huchochea hisia kwamba unastahili chakula kizuri, kama vile umepewa zawadi, lakini kuna hatari ya kula kupita kiasi, na kuwa na uraibu , ambao huleta athari kwa afya.
Utafiti nchini Uturuki uliochapishwa Januari 2024 katika Jarida la Lishe ya Binadamu na ,Lishe ulichambua njaa ya hedonic kwa watu wazima wanene.
Waligundua kwamba njaa ya hedonic ilipoongezeka kwa watu wazima wenye uzito kupita kiasi, kujithamini kulipungua na walihisi kujinyanyapaa kunakohusiana na kuongezeka kwa unene na uzito wa miili yao.
Kwa hiyo tunapaswa kufanya nini ili kuepuka matumizi ya kupita kiasi yanayosababishwa na kula hedonic?

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Utafiti unatuambia kwamba njaa ya hedonic inaweza kupungua wakati watu wanapopoteza uzito wa mwili," Dk. Mead anajibu.
"Watu wanaokabiliana na aina hii ya njaa wanaweza kubadilisha mtazamo wao kuhusu chakula, au wanaweza kubadilisha jinsi wanavyoonyesha hisia zao kwamba wanastahili kula," aliongeza.
Kupunguza uzito, kuanza aina mpya ya ulaji, au kufuata mtindo mpya wa maisha mzuri kunaweza kuwa sio rahisi kwa wengi. Lakini kuna njia ya kuigeuza kuwa shughuli ya kufurahisha, anasema Profesa Stubbs.
"Kwa mfano, ikiwa unataka kuongeza shughuli zako za kimwili, fikiria juu ya shughuli gani zinaweza kuwa za kufurahisha zaidi kwako," Stubbs anaongeza "Je, hiyo itakuwa kufanya mazoezi? Labda sivyo? Je, itakuwa kutembea na marafiki au kucheza? jambo kuu ni "Jaribu kuelewa ni vipengele gani vya raha vinavyochochea maisha yako, na jaribu kuoanisha mazoea yako mapya na mambo yanayokupa raha."
Kula kwa uangalifu na kwa umakini inaweza kuwa njia ya kuzuia utumiaji wa kupita kiasi kulingana na ulaji wa hedonistic pia.
"Hatutaki kuwazuia watu kujihusisha na ulaji wa kufurahisha," Profesa Stubbs anasema "Tunataka kuelekeza raha katika ulaji bora."
Anasema inawezekana kuendeleza uhusiano mzuri zaidi na chakula, bila kuathiri unayoipata kutokana na vyakula vinavyokupa raha.
Stubbs anaamini kwamba tunaweza "kusonga mbele kuelekea kile tunachokiita mtindo wa maisha wa ishirini na themanini."
Mtindo wa maisha wa ishirini hadi themanini unawakilisha lishe, ambayo ni kwamba "mtu hula 80% ya vyakula vyake vya chini vya kalori na virutubishi vingi ambavyo huvifanya iwe ya kufurahisha zaidi, hii inamaanisha kuwa 20% hubaki kufurahia vyakula vinavyomfanya mtu binafsi kuhisi kuwa mwenye furaha, ikiwa ni pamoja na peremende zinazoongeza furaha maishani na mara nyingi huhusishwa na matukio na hali muhimu za kijamii,” kulingana na Stubbs.
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi












