'Mwanangu hakuwahi kujiona yuko salama ndipo akauawa kwa kupigwa risasi'

AFP

Chanzo cha picha, AFP

Kwa wastani karibu mtu mmoja kwa saa hupigwa risasi na kufariki nchini Afrika Kusini, wataalam wanasema.

Na uzoefu ulioishi kwa baadhi ya watu unadhihirisha ukubwa wa vurugu za kutumia bunduki.

"Kila usiku kuna risasi. Risasi, kila siku," alisema mkazi mmoja wa Soweto, ambaye aliomba hifadhi ya jina.

Ilikuwa katika kitongoji hiki kikubwa nje kidogo ya Johannesburg ambapo watu 15 walipigwa risasi na kufa katika baa iliyokuwa imejaa watu mapema mwezi huu, mwathirika mwingine alifariki baadaye hospitalini.

Kundi la watu wenye silaha walivamia kabla ya saa sita usiku na kuanza kufyatua risasi kisha wakatoweka usiku huo.

Tukio hili na lingine la hivi karibuni la Tavern yameonesha msisitizo jinsi nchi inavyoweza kutokuwa salama.

Nilitembelea Soweto baada ya mauaji ya watu wengi huko na watu walikuwa bado wanamshtuko. Lakini kuna imani ndogo kwamba mamlaka itachukua hatua.

“Nimeishi hapa miaka mingi, tukiripoti polisi hawaji, wanasema hili eneo ni marufuku kuingia kwa jinsi lilivyo hatari, sielewi ni vipi wanaweza ni eneo lililopigwa marufuku wakati kuna watu wanaoishi hapa," mkazi mmoja alisema.

Unaweza pia kusoma

Zimepita wiki chache tangu wakati huo na bado hakuna mtu aliyekamatwa.

Lakini vurugu za kutumia bunduki si tatizo geni kwa Afrika Kusini au ni moja la kipekee kwa Soweto.

ggg
Maelezo ya picha, Mtoto wa Lesley Wyngaard, Rory alipigwa risasi na kuuawa wakati ametoka na marafiki
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Lesley Wyngaard ni mama anayeombeleza huko Cape Town Eneo ambalo baadhi ya jamii zimezingirwa na ghasia za magenge na silaha.

"Wameondoa sehemu ya moyo wangu. Haitakuwa sawa tena, wamechukua sehemu yangu," Lesley Wyngaard akizungumzia maisha tangu kifo cha mtoto wake wa kiume miaka saba iliyopita.

Rory, 25, alipigwa risasi nyuma ya kichwa chake alipotoka na marafiki zake usiku katika kitongoji cha Mitchells Plain, kisa cha kuwa mahali pasipofaa kwa wakati usiofaa.

Kitongoji cha Mitchells Plain kinaonekana kuwa katika eneo lenye fujo na magenge ya watu wanaopigana mara kwa mara na watu wasio na hatia mara nyingi wanaingizwa kwenye mapigano hayo.

Miaka saba baada ya kifo cha Rory, Bi Wyngaard alisema vurugu bado zinaendelea.

Mabaki ya mwili wake yalizikwa katika bustani ndogo katika uwanja wa kanisa.

"Yupo salama sasa, hana maumivu. Hakuna anayeweza kumdhuru tena," alisema huku akiweka vizuri chombo cha maua karibu na majivu ya mwanawe.

Kwa mujibu wa wataalam wa uhalifu, furugu za kumia bunduki zimezidi kuwa mbaya. Wanasema kwa wastani watu 23 wanauawa kwa kupigwa risasi kila siku nchini Afrika Kusini, hiyo ni juu ya watu 18 miaka sita iliyopita.

ggg
Maelezo ya picha, Wataalamu wa mausla ya uhalifu wanasema vurugu za kutumia bunduki zimezidi kuwa mbaya nchini Afrika Kusini, kwa wastani watu 23 wanauawa kwa kupigwa risasi kila siku.

Lakini kwa nini vurugu za bunduki zimeenea sana?

Mtaalamu Prof Lufuno Sadiki anadhani kuwa uhusiano wa nchi na vurugu ni mkubwa.

"Hatuwezi kupuuza historia ya nyuma ya nchi yetu," alisema, akimaanisha jinsi mfumo wa ubaguzi wa rangi uliohalalishwa ulivyotekelezwa kabla ya kusambaratishwa karibu miongo mitatu iliyopita.

"Mfumo wa ubaguzi wa rangi wenyewe ulikuwa wa fujo na wa kikatili sana" ambapo vikosi vya usalama na jamii zote zilikuwa na silaha. "Utamaduni huo wa kumiliki silaha uliendelea," alisema.

"Katika siku hizi, Waafrika Kusini wamepoteza imani na polisi na kwa sababu ya ukosefu huo wa uaminifu pamoja na imani raia wengi sasa wanajizatiti."

Wataalamu wengi wanakubali kwamba silaha haramu ni tatizo kubwa hapa.

Utafiti wa hivi karibuni wa Mpango wa kimataifa dhidi ya Uhalifu uliopangwa uligundua kuwa baadhi ya bunduki na risasi za hali ya juu huingizwa nchini kutoka nchi jirani za Zimbabwe na Msumbiji kupitia mitandao ya kupanga uhalifu.

Lakini silaha pia hupotea kutoka kwa vikosi vya usalama.

Mwaka jana, wizi kadhaa uliripotiwa katika vituo vya polisi kote nchini ambapo mamia ya bunduki ziliibiwa.

Wakosoaji wanasema kuwa mamlaka haziwezi kufuatilia bunduki halali.

Rory Wyngaard aliuawa kwa silaha kama hzio.

"Tuligundua wakati wa kesi mahakamani kwamba Rory aliuawa kwa bunduki ya polisi. Ilipotea au kuibiwa kutoka kwao lakini aliuawa kwa bunduki ya polisi," alisema Bi Wyngaard.

ggg
Maelezo ya picha, Wyngaard anaweka maua karibu na majivu ya Rory. Mmtoto wake aliuawa na bunduki ya polisi iliyopotea au kuibiwa miaka saba iliyopita.

Kesi yenyewe mahakamani iliishia kufutwa kwa sababu ya kosa la kiutawala, ambalo lilikuwa pigo jingine kwa familia.

Polisi wanasisitiza kuwa wanafanya jambo kuhusu tatizo la silaha.

Wanasema kwamba zaidi ya miaka 10 iliyopita wamepata 70% ya bunduki zilizopotea - mara zinapopatrikana bunduki hizi huaribiwa mara moja..

Adele Kirsten ambaye amekuwa akishawishi kwa miongo kadhaa kuwa Afrika Kusini bila bunduki alisema kwamba ikiwa nchi hiyo ina matumaini yoyote ya kupunguza ghasia za utumiaji bunduki, juhudi za pamoja zinatakiwa kuwekwa katika kupunguza idadi ya bunduki katika mzunguko.

"Tunalazimika kunyonya silaha haramu lakini mara tu unapoondoa kundi la bunduki haramu, unapaswa kuzima bomba," alisema.

Wakati kumekuwa na wito mpya wa kuweka sheria kali za bunduki za Afrika Kusini zaidi ikiwa ni pamoja na kufanya iwe vigumu zaidi kwa watu kupata leseni ya bunduki kwa ajili ya kujilinda kwanza, watetezi wanaounga mkono bunduki wanasema hilo sio suluhisho.

"Sio tatizo kwa raia au mtu binafsi kumiliki kihalali bunduki. Ni tatizo la magenge ya uhalifu kupata mikononi mwao aina hizo za silaha," alisema Damian Enslin, ambaye ni mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Guwners cha Afrika Kusini.

"Tayari tuna sheria nzuri za kumiliki bunduki, tunaweza kuwa na sheria bora zaidi duniani lakini kama hakuna mtu anayezisimamia ni kazi bure."

Kwa familia zilizo ondokewa na wale wanaowapenda kutokana na ghasia za bunduki suluhu za matatizo ya bunduki haramu zinakuja polepole mno.

Kwa Bi Wyngaard na familia yake hakuna kitu wanachotarajia, hakuna haki, hakuna kufungwa, ni familia tu ambayo bado inapambana na kupoteza mtoto wao wa kiume.

Sasa anawashauri wazazi wengine katika jamii yake ambao wamepitia uzoefu sawa na njia ya uponyaji.

"Mambo sio mazuri, yanazidi kuwa mbaya.

"Siku zote huwa nawashauri watu kuhisi kile unachohitaji kuhisi kwa sababu kitu cha thamani, kitu ulichopewa na Mungu kimechukuliwa kutoka kwako. Ulichukuliwa mtoto wako, ni aina mbaya ya maumivu."