Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Jinsi ya kudhibiti hatari ya shinikizo la damu
Kuchunguza shinikizo la damu yako ndio njia bora ya kujua kama una tatizo la shinikizo la damu kwa sababu baadhi ya watu hawana uwezo wa kung'amua mapema dalili zinazohusiana na hali hii.
Takriban nusu ya watu bilioni 1.3 wanaoishi na shinikizo la damu hawana ufahamu kuhusu hali zao.
Afrika ina kiwango cha juu cha watu wanaokabiliwa na maradhi ya shinikizo la damu (27%) huku Marekani ikitajwa kuwa na kiwango cha chini cha zaidi cha watu wanaokabiliwa na haloi hiyo (18%), kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani.
Nchi zilizo na kipato cha chini na na zile zilizo na kipato cha wastani zimeshuhudia idadi kubwa zaidi ya watu wazima walio na shinikizo la damu kutokana na ongezeko la hatari ya shinikizo la damu miongoni mwa watu hao.
Shinikizo la damu ambalo halijathibitiwa huongeza kwa kiasi kikubwa madhara makubwa ya kiafya kama vile ugonjwa wa moyo, kiharusi, na figo kushindwa kufanya kazi—hali hizo zinaweza kusababisha kifo cha mapema, kulingana na WHO.
Ufuatiliaji wa mara kwa mara ni muhimu kwa utambuzi wa mapema ili kudhibiti shinikizo la damu.
Maelezo haya yatakusaidia kuelewa jinsi ya kufuatilia na vipimo vya shinikizo la damu, kwa kuzingatia viwango vya WHO, na kukupatia muongozo kuhusu hatua za kuchukua ili kulinda afya yako.