Iko chini
Jinsi ya kutumia kifaa hiki
Mambo ya kufanya
Unaweza kutumia kifaa hiki ikiwa wewe au mtu unayemsaidai kututumia:
- Ana umri wa miaka 18 au zaidi
- Amewahi kufanyiwa vipimo vya shinikizo la damu na mtaalamu wa afya ama kwa kutumia kifaa cha kufuatilia shinikizo la damu nyumbani
Mambo ya kuepuka
Hutakiwi kutumia kifaa hiki kama wewe ama mtu unayemsaidia kukitumia:
- Ana umri wa miaka 17 au chini ya miaka hiyo.
- Ni mjamzito
- Anatumia dawa ambazo zinaweza kuathiri shinikizo lako la damu.
- Ikiwa umefanyiwa upasuaji au kuumia
- Ikiwa haujisikii vizuri na unadalili mpya kizunguzungu, kichefuchefu au kuumwa na kichwa
- Ikiwa hivi karibuni umeonana na mtaalamu wa afya kuhusu shinikizo la damu yako na kukupa usharui
- Haupaswi kutumia kifaa hiki kubaini dalili zozote. Ikiwa una wasiwasi na na shinikizo la damu yako, muone daktari
Vidokezo vya kupima shinikizo la damu kwa usahihi
Unapofanya vipimo vya shinikizo la damu nyumbani kuna mambo unastahili kuzingatia ili kupata matokeo sahihi
- Kaa kwenye kiti kilicho wima chenye sehemu ya nyuma ya kuegemea
- Kanyanga miguu yote kwenye sakafu.
- Weka mkono wako juu ya meza na utulize mkono
- Vaa nguo ya mikono mifupi.
- Tulia kisha pumua kama kawaida na usiongee wakati wa kufanya vipimo.
- Chukua kipimo kingine dakika chache baada ya kipimo cha kwanza ili kuthibitisha usahihi wake.
- Pima shinikizo la damu asubuhi na jioni.









