Je, vinywaji vyenye afya vinaweza kusababisha kuoza kwa meno?

Sharubati

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 4

Kunywa maji ya matunda yenye ladha au glasi ndefu ya sharubati ya machungwa inaweza kuonekana kama mbadala mzuri kwa soda, lakini watafiti wanaonya kuwa chaguzi hizi "za afya" zinaweza kuwa na madhara zaidi kuliko tunavyofahamu.

Utafiti uliofanywa na watafiti wa chuo, King's College London nchini Uingereza uligundua kuwa vinywaji kama vile chai ya matunda au sharubati ya machungwa vinaweza kuharibu kabisa tabaka gumu la jino, tabaka la nje linalolinda meno dhidi ya mmomonyoko.

Lakini habari njema ni kwamba uharibifu huu hauwezi kuepukika. Watafiti walio na uzoefu wa zaidi ya miaka 20 wamegundua kuwa muda na njia ya kunywa vinywaji inaweza kuleta tofauti kubwa katika kuzuia mmomonyoko wa meno.

Ilinibidi kuijaribu mwenyewe, kwa hivyo nilitembelea timu ya watafiti na kuchunguzwa meno yangu.

Kuna tofauti gani kati ya kutoboka na mmomonyoko wa meno?

Kuanzia ujana, tumezoea kuonywa na wazazi wetu kuhusu matundu, mashimo madogo yanayoonekana kwenye meno yako na jinsi peremende na chokoleti vinaweza kuharibu tabasamu lako.

Unapokula vyakula vya sukari, bakteria asilia wanaoundwa kwenye meno yako hula mabaki ya sukari kwenye kinywa chako, na kusababisha matundu kwenye meno yako. Isipokuwa mashimo haya ni makubwa sana, yanaweza kurekebishwa kwa kuyajaza.

Lakini mmomonyoko wa meno ni tofauti kabisa. Asidi katika baadhi ya vyakula na vinywaji hushambulia moja kwa moja gamba la jino, hatua kwa hatua huidhoofisha na kuiondoa pamoja na safu inayofuata (dentin), na kufanya jino liwe na hatari zaidi ya uharibifu.

Gamba la jino hulinda tabaka jembamba, lakini haiwezi kulinda kutokana na uharibifu unaoendelea unaosababishwa na asidi na sukari. Mara tu inapoharibika, uharibifu unakuwa wa kudumu.

Meno

Chanzo cha picha, Getty Images

Mmomonyoko wa meno hutokea wakati tabaka la jino linapokabiliwa na matumizi ya kupita kiasi ya vyakula na vinywaji vyenye asidi na sukari," anaonya Dk. Polypheos Charalambous, daktari wa meno na mshiriki wa timu ya utafiti.

Anaongeza, "Ikiwa haitatibiwa, upotezaji wa gamba la jino unaweza kusababisha shida kama vile kubadilika kwa rangi ya meno, nyufa au kingo zenye ncha kali na hata kubadilika kwa rangi ya meno ambayo hulifanya lionekane kuwa laini."

Jinsi na wakati wa kunywa bila kuathiri meno yako

Dk. Charalambous alifanya majaribio rahisi ya kupima asidi ya mdomo wakati akinywa sharubati ya machungwa, kwa kutumia kifaa maalum cha kubainisha kiwango cha asidi (pH).

Ili kudumisha meno yenye afya, kiwango cha pH kwenye mdomo kinapaswa kuwa karibu 7, lakini matokeo yalisababisha mshangao :

- Kunywa mara kwa mara kulipunguza pH hadi 4.7, na iliuchukua mdomo sekunde 18 kurudi kawaida.

Kuiacha sharubati kinywani kwa sekunde 10 kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa asidi, na kupona kulichukua mara tano zaidi.

Na daktari wa meno
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Jaribio lilionesha kuwa kuweka vinywaji vyenye tindikali kinywani huongeza uharibifu maradufu, kwa sababu hii huongeza muda wa asidi inapogusana na uso wa jino na huongeza nguvu yake.

Dk Charalambous anasema, "Ili kulinda meno yako, epuka kuweka vinywaji vyenye tindikali kinywani mwako kwa muda mrefu. Ni vyema kutumia majani ili kupunguza kugusa meno yako, kwani utafiti umeonesha kuwa utumiaji wa majani hupunguza mmomonyoko wa meno unaosababishwa na vinywaji vyenye kaboni."

Kwa mfano, watu ambao walikunywa vinywaji vyenye tindikali mara mbili kwa siku kati ya mlo kama vile soda, maji yenye kipande cha limau, au chai ya matunda ya moto, walikuwa na uwezekano wa mara 11 zaidi kuwa na mmomonyoko wa meno wa wastani hadi kuwa mkali.

Wakati vinywaji hivi vinatumiwa na chakula, hatari hii inapungua kwa nusu.

Kwa hivyo, kwa kuweka muda wa matumizi yako kwa busara, ama na, kabla, au mara baada ya chakula chako, unaweza kulinda meno yako vizuri zaidi.

Ni vinywaji gani vina madhara zaidi kwa meno?

Vinywaji

Timu kutoka Chuo cha King's College London ilifanya jaribio la kulinganisha athari za aina nne tofauti za vinywaji kwenye tabaka laa jino, kwa kutumbukiza sampuli za katika sharubati ya machungwa, cola, ayran, na chai ya matunda.

Baada ya saa moja, uharibifu uliotokea ulikuwa sawa na ule uliosababishwa na vikombe vitatu vya kila kinywaji kwa siku kwa siku mbili, na picha za darubini zilionesha wazi athari za kutu kwa namna ya mistari ya giza ndani ya sampuli.

Matokeo yalikuwa ya kushangaza:

Vinywaji baridi vilisababisha kiwango cha juu cha mmomonyoko,

Ikifuatiwa na sharubati ya machungwa,

Kisha chai nyekundu ya raspberry,

Wakati maziwa yaliyochanganywa na maji (ayran) yalikuja katika nafasi ya mwisho katika suala la madhara, na kuifanya kuwa na madhara madogo kwa meno.

Ayran ni kinywaji cha kitamaduni kinachojulikana katika nchi kadhaa, kama vile India, Pakistan, Lebanon, Syria, Uturuki, Iran, na Armenia.

Je, kuna kikomo cha kawaida cha mmomonyoko wa meno?

mmomonyoko wa jino hutokea kwa kawaida katika maisha yote, kama sehemu ya mchakato wa kisaikolojia wa kuzeeka," anaeleza Dk. Polypheos Charalambous.

Lakini anaonya kwamba mambo kama vile lishe, mazoea ya kila siku, au hali fulani za kiafya, kama vile reflux ya asidi, inaweza kuharakisha mchakato huu.

Anaongeza kuwa madaktari wa meno wana uwezo wa kutathmini kiwango cha mmomonyoko kwa kutumia waelekezi wa kitaalamu, lakini matokeo yake yanaweza kuwa ya kutisha, kwani tabaka la jino haliwezi kurejeshwa pindi linapomomonyoka, hivyo kuzuia siku zote ni njia bora zaidi.