Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Apple iPhone 15: Je simu hii mpya inaweza kupiga 'radi bila umeme'?
Ninapoandika haya bado kumesalia saa kadhaa kabla ya Apple kuzindua toleo la hivi karibuni la bidhaa yake inayouzwa zaidi, iPhone.
Katika wiki chache zilizopita tumeona simu ikipata shinikizo kutoka EU na Uchina.
Ulimwenguni kote, mauzo ya simu za smartphone kwa ujumla yanapungua, na simu yenye kutarajiwa kuwa na mazingira ya uhalisia halisi ya Apple - ambayo kampuni ilionekana kuiweka kama iPhone ya siku za usoni - haitauzwa hadi mwaka ujao.
Wakati utakapowadia, itauzwa kwa bei ya juu kabisa ya $3,500 (£2,780).
Na kwa hivyo, wakati huo huo, tunakutana na kizazi cha 16 cha simu iliyobadilisha simu za smartphone kabisa wakati ilipozinduliwa mnamo 2007.
Inaweza kuonekana kama kejeli lakini bado inavutia watu wengi hii leo - tayari kuna karibu matokeo ya utafutaji wa Google bilioni tano kwa neno "iPhone 15", licha ya kwamba hakuna hakiki rasmi kutoka kwa kampuni yenyewe ya Apple.
Ukianza kuangalia kwa undani na kufuatilia uvumi na "yaliyovuja" ambayo yanasambaa, utaona kuwa aina ya iPhone 15 inaweza kuwa nyepesi kidogo kuliko zilizotolewa awali, ikiwa na chipu iliyoboreshwa, betri yenye kudumu kwa muda mrefu, kamera bora na chasi ya titani.
Vizazi vya simu za Apple, kama simu zingine nyingi, wakati mwingi huwa zimeboreshwa.
Ni mojawapo ya masuala yanayolaumiwa kwa kupunguza mauzo duniani kote.
Watu wanatumia simu zao kwa muda mrefu zaidi - sio tu kwa sababu ni ghali kifedha - lakini pia kwa sababu hakuna tena ushawishi mkubwa wa kukusukuma kununua simu mpya iliyoboreshwa.
"Nadhani kampuni ya Apple labda inatambua kuwa wamefikia hatua ambapo kuna idadi kubwa ya iPhones kiasi kwamba kudumisha tu idadi hiyo ni mafanikio makubwa," Ben Wood, mtaalam wa smartphone alisema.
Anakubali kuwa ingawa labda hatutashuhudia iPhone tofauti sana kwenye hafla ya Apple ya kila mwaka ya Septemba huko Marekani jioni hii, tutakachoona ni kampuni tajiri iliyobobea katika utoaji wa bidhaa kwa mashabiki wake.
Baada ya kusema hivyo, kuna kitu kimoja ambacho haujawahi kuona hapo kabla, na ikiwa uko Ulaya, hakika utabaini hili.
IPhone 15 hakika itakuwa na sehemu ya kebo ya kuchaji ya USB-C.
Kwa sasa iPhones zinategemea kebo ya umeme inayomilikiwa na kampuni yenyewe, wakati simu zingine nyingi - ikiwa ni pamoja na zingine zilizotengenezwa na Apple - huwa zinatumia USB-C.
Tofauti kuu kimuonekano ni kwamba hizi mbili zina maumbo tofauti.
Kwa hivyo ikiwa, kwa mfano, una iPhone na Kindle, chaja yako ya iPhone haitatosha kwenye eneo la Kindle (kifaa cha kusoma cha kielektroniki) na kinyume chake.
Apple imesisitiza kwa muda mrefu kuwa utofautishaji wa bidhaa daima husababisha uvumbuzi mkubwa.
Pia imeshinikiza kuchaji bila kutumia waya kama njia mbadala kwa miaka kadhaa - simu zote tangu iPhone 8 zimeanza kutumika.
Hata hivyo, EU imekuwa na kiasi cha kutosha, na kutangaza kuwa vifaa vyote vinavyobebeka vinahitaji kuendana na chaja inyotumika kuchaji simu za aina zote ulimwenguni ifikapo Desemba 2024.
Na sekta nyingine ya teknolojia ya watumiaji wa vifaa vya umeme bado haijaanza kupokea mabadiliko ya kutumia mfumo mpya wa kuchaji simu wa kimataifa, hata kama Apple ingeiruhusu.
Lakini unaweza kuwa sawa kuongeza kebo hiyo kwenye droo yako ya kebo badala ya kuitupa - Ben Wood anasema kuna soko kubwa la simu za mitumba za iPhones, haswa barani Afrika.
"iPhones zinaingia mikononi mwa watu ambao hawakuweza kuzinunua hapo awali ... na hilo linawafunga kwenye mfumo wa ikolojia wa Apple," alisema.
EU sio eneo pekee linaloweka sheria.
Wiki iliyopita China iliripotiwa kupiga marufuku iPhone kutoka kwa majengo ya serikali kwa misingi ya usalama.
Hili halihusiani sana na simu yenyewe bali linahusiana zaidi na mzozo wa teknolojia unaoendelea kati ya China na Marekani - lakini ilisababisha bei ya hisa za Apple kuyumba.
Watu wengi nchini Uchina hutumia simu za Android, lakini iPhone ndiyo yenye mauzo ya juu zaidi.
Kwa kuongezea, ni changamoto kwa Apple kwa sababu bado hutengeneza bidhaa zao huko.
Imekuwa ikijaribu kuondoka – kwa mfano, iPhone 14 imetengenezwa nchini India, - lakini bado inahitaji kampuni na viwanda vya China.
Apple bado inahitaji China. Lakini sisi wengine tunahitaji au tunataka iPhone mpya kiasi gani? Tunakaribia kufahamu hili.