Kombe la Dunia 2022: Mfaransa Kylian Mbappe akimpiku Olivier Giroud baada ya rekodi ya kufunga mabao

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Zinedine Zidane, Michel Platini, Thierry Henry, Just Fontaine.

Ufaransa imekuwa na wachezaji wa ajabu katika historia yao lakini ni Olivier Giroud ambaye sasa anaweza kudai kuwa miongoni mwa magwiji wa nchi hiyo.

Mshambulizi huyo wa AC Milan amekuwa mfungaji bora wa Ufaransa kwa wanaume alipoiweka timu yake mbele katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Poland katika hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia.

Lakini katika siku yake muhimu - alipofunga bao lake la 52 la kimataifa - mshambuliaji huyo wa zamani wa Chelsea na Arsenal alifurahishwa na uchezaji mzuri wa mchezaji mwenzake Kylian Mbappe.

Vijana wa Didier Deschamps hawana mzaha wanapolenga kutetea taji lao na safu yao inaongozwa na mshambuliaji mkongwe Giroud mwenye umri wa miaka 36 na Mbappe mwenye umri wa miaka 23.

"Huu ni ushindani wa ndoto zangu," alisema mchezaji bora wa mechi Mbappe, ambaye alifunga mara mbili na kuchangia bao la Giroud. "Ni kitu ambacho nimekuwa nikijiandaa kimwili na kiakili.

"Tunafanya vizuri lakini [tuko] mbali sana na lengo la kushinda fainali."

'Mchezaji mpira wa kipkee'

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kama vile Lionel Messi wa Argentina anavyowatoa mashabiki kwenye viti vyao kwa msisimko, Mbappe anaifanyia Ufaransa vivyo hivyo na alikuwa kwenye kiwango bora dhidi ya Poland.

Mbappe aliamsha shangwe kubwa alipomweka beki wa pembeni wa Aston Villa, Matty Cash kwenye upande wake wa nyuma na kugeuka haraka lakini mkwaju huo ukatoka nje hadi wavuni.

Akiwa ametoa pasi ya bao la kuongoza la Giroud, Mbappe alionyesha umahiri wake wa kumalizia pasi kwa kugonga bao lake la kwanza kwenye paa la wavu kabla ya kupachika bao la pili kwenye kona ya mbali.

Sasa ndiye mfungaji bora wa shindano hilo akiwa amefunga mabao matano na kuongeza mabao manne aliyofunga kwenye kampeni ya Ufaransa ya ushindi wa Kombe la Dunia 2018, tayari amempita Diego Maradona wa Argentina, aliyefunga nane, huku Mreno Cristiano Ronaldo pia akifikisha idadi hiyo.

Akiwa na umri wa miaka 23, Mbappe ndiye mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kufunga mabao tisa Kombe la Dunia, akivunja rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Eusebio, aliyeifungia Ureno mabao 8 akiwa na umri wa miaka 24 na siku 182.

"Tunajua kuhusu Kylian," Deschamps alisema. "Tayari tumemwona na anazungumza kwenye uwanja wa mpira.

"Anajua anaweza kubadilisha mechi kwa sasa. Anacheza kwa furaha na tabasamu. Ufaransa ilihitaji Kylian Mbappe mkubwa usiku wa leo na walipata mmoja."

Mshambulizi wa zamani wa Premier League Dion Dublin alisema kwenye BBC One: "Anacheza mchezo huo kana kwamba yuko uwanjani. Ni mwanasoka wa ajabu."

Chris Sutton, akizungumza kwenye BBC Radio 5 Live, alisema: "Hatimaye ilimfikia Kylian Mbappe na mambo kadhaa mazuri kutoka kwake.

"Hii ilikuwa utendaji mzuri kutoka kwa Ufaransa. Kuna majaribio magumu zaidi yajayo lakini ilikuwa ni maonyesho ya Kifaransa na taarifa kwamba sisi bado ni timu ya kushinda."

Giroud asalia thabiti ‘kiakili'

th

Huenda wengine walihisi miaka bora ya Giroud ilikuwa nyuma yake alipoondoka Arsenal majira ya joto yaliyopita na kuhamia Italia lakini alifunga mabao 11 na kuisaidia Milan kushinda taji la Serie A.

Giroud ana nyota wanaomzingira kikosini kama Mbappe na Antoine Griezmann wanaowavutia wengi .

Lakini Giroud ni kipenzi cha Deschamps na anajua anacholeta kwenye timu kwa kutokuwa na ubinafsi huku akipewa dakika zaidi wakati huu kwa sababu ya kuumia kwa Karim Benzema kabla ya mechi.

Kwenye Kombe la Dunia lililopita, Giroud alicheza michezo yote katika ushindi wao nchini Urusi, lakini katika dakika 546 za mchezo, hakushindwa tu kufunga bao lakini hakuwa na shuti hata moja lililolenga lango.

Jinsi mambo yanaweza kubadilika. Giroud ameshafunga mara tatu kwenye mashindano haya, lakini atafahamu kuwa rekodi yake ya jumla inaweza isidumu sana kutokana na Mbappe kuwa tayari ameifungia Ufaransa mabao 33.

"Giroud amekuwa mchezaji muhimu siku zote," alisema Deschamps. “Miaka minne iliyopita hakufunga lakini tunaona ubora wake.

"Ameweza kubaki na nguvu kiakili. Amevunja rekodi ya Henry, na Mbappe anaweza kuishinda siku moja. Kufunga mabao mengi katika ngazi ya kimataifa ni mafanikio makubwa."

Beki wa zamani wa Uingereza Rio Ferdinand alisema kwenye BBC One: "Lazima uwe na mtazamo sahihi kufanya kile Olivier Giroud anafanya, huku watu wakisema wakati fulani hakuwa mzuri.