Kuitengenezea Urusi "Jehannamu": Nini kinajulikana kuhusu kombora jipya la Ukraine la droni?

Chanzo cha picha, Zelensky
Katika siku ya majeshi ya Ulinzi nchini Ukraine, kuna zana mpya za kijeshi zilizoonekana. Zana hizi ni pamoja na kile kinachojulikana kama "Kombora la droni au "drone-missile" au ndege isiyo na rubani inayoitwa "Hell". Kabla ya hapo, hakuna kitu kilichojulikana kuihusu.
Rais Volodymyr Zelensky alitoa picha ya silaha hiyo. Kulingana naye, tayari limejaribiwa katika mapigano na makombora ya aina hii yameanza kuzalishwa kwa wingi.
"Ukraine yetu, silaha ambazo tayari zimethibitisha matumizi ya kupambana. Leo, kundi la kwanza llilipelekwa kwa vikosi vyetu vya ulinzi. Kwa sasa kazi tuliyonayo ni kuongeza uzalishaji na matumizi," alisema Rais.

Chanzo cha picha, Herman Smetanin
"Mtengenezaji wa Kiukreni aliunda kombora la droni kutoka mwanzo kwa wakati wa mfupi wa matengenezo ya silaha kuwahi kurekodiwa - ndani ya mwaka mmoja. Silaha hiyo tayari inaweza kupambana na kwa mafanikio makubwa, "alisisitiza.
Ndege hii isiyo na rubani, alisema, inaruka kwa kasi ya kilomita 700 kwa saa kwa umbali wa hadi masafa hadi kilomita 700.
Aliongeza kuwa, kazi inaendelea kila wakati ili kuongeza kiwango cha ulinzi wa bidhaa kwa ajli ya vita vya elektroniki, kuboresha sifa za uendeshaji na usahihi wa uharibifu wa maeneo yanayolengwa. Aina mpya za vilipuzi vya makombora zinatengenezwa ili kupanua orodha ya malengo yanayowezekana.

Chanzo cha picha, Herman Smetanin
Kwa kuchambua picha na video zilizochapishwa za droni ya "Hell", tunaweza kusema kuwa silaha hii ni mpya kabisa kwa Jeshi la Ukraine.
ndege hii haionekani kupaa kutoka ardhini, bali hupaa kutoka angani labda kutoka kwa vilipuzi vya mstari wa mbele au wapiganaji.
Ikiwa hii ni kweli, basi tuna mbinu mpya ya kuzindua UAVs, ambayo haikutumika hapo awali wakati wa vita vya Urusi na Ukraine.
Kwa mfano, ndege isiyo na rubani inayofanya mashambulizi kwa muda mrefu "Lyuty" hupaa kwa haraka kwenye njia ya ndege, na Tu-141 ya Usoviet iliyobadilishwa ("Strizh") - hutoka kwa kizinduzi maalum kikubwa.

Chanzo cha picha, Zelensky
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Kwahivyo, inaweza kusemekana kuwa kombora la "Hell" lisilo na rubani liko karibu kufanana na makombora ya cruise kuliko droni ya kawaida.
Pia linafanana na mabomu ya glide ya Magharibi ya juu kama vile AASM ya Kifaransa (HAMMER), ambayo pia ina nyongeza ya roketi na mfumo wa urambazaji.
Hatahivyo, kiwango cha ndege kilichotangazwa cha Ukraine cha "Hell" ni mara 10 zaidi. Inawezekana kwamba hii ni kwasababu ya kilipuzi kidogo cha makombora, Ukraine haielezi kuhusu vilipuzi vya makombora katika ndege hizi zisizo na rubani.
Katika mkia wa "Hell" unaweza kuona injini ya turbojet ya mbali, mbele – kuna king'amuzi (sensor) ya kasi (Pito tube).
Kwa ujumla, ndege hii isiyo na rubani ni sawa na ndege ya "Palyanytsya" iliyowasilishwa mwishoni mwa mwezi Agosti. Lakini, haikuwa na injini ya mbali, ilikuwa na vifaa vya rada vinavyoweza kuhamishwa kwenye mkia na ilizinduliwa, kama ilivyoelezwa, kutoka kwenye jukwaa maalum.
Eneo hilo pia lilitajwa kuwa katika eneo la kilomita 600-700.
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi












