Je, droni za wavu za Urusi zinafanyaje kazi?

cx

Chanzo cha picha, RUSSIAN TACTICAL EQUIPMENT SITE

Maelezo ya picha, Droni zenye wavu
    • Author, Sergey Morfinov
    • Nafasi, BBC

Video za ndege zisizo na rubani zinazodondosha nyavu kwenye ndege nyingine zisizo na rubani - zimeonekana hivi karibuni kwenye chaneli za Telegraph za Urusi.

Machapisho haya yanadai kuwa hilo ni "suluhisho bora" katika vita vya anga dhidi ya ndege zisizo na rubani za adui. Hii ni ndege isiyo na rubani inayoendeshwa na rafadha (propela) iliyo na kifaa cha kudungua wavu dogo.

Droni hizo huruka hadi kwenye droni zingine za Ukraine, na zikiwa angani huzidondoshea wavu ambazo huingia kwenye mapanga ya droni za adui na huanguka.

Katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita, video kadhaa kama hizo zimechapishwa kwenye chaneli za Telegraph za Urusi. Vyanzo vingine vya Urusi vinakiita kifaa cha kurushia wavu "Tarantula."

Ukubwa uliotajwa wa nyavu hizo ni mita mbili tu. Bei ya Tarantula kwenye tovuti za Urusi ni takribani dola za Kimarekani 800.

Pia unaweza kusoma

Je, zina ufanisi?

xz

Chanzo cha picha, RUSSIAN TACTICAL EQUIPMENT SITE

"Tunapeleka polepole maendeleo haya katika vitengo vya jeshi, hadi iwe ni suluhisho bora zaidi kuzuia droni," chaneli ya jeshi la Urusi iliandika.

"Mfumo huu umeonyesha ufanisi kwenye uwanja wa vita. Swali pekee ni kuhusiana na matumizi. Kitu chochote ambacho kinaweza kuathiri mali ya adui kinaweza pia kudhuru yetu. Tumia kwa busara,” chaneli hiyo hiyo ilisema siku chache baadaye.

Video zinaonyesha kuwa wavu hizo zimeweza kutumika kwa mafanikio dhidi ya ndege nyepesi zisizo na rubani, pamoja na zile nzito - zenye propela sita, nane au zaidi.

Ikiwa Tarantula zitafanikiwa kwa kiwango kikubwa, zinaweza kubadilika na kuwa droni za kawaida katika jeshi la Urusi.

Hata hivyo, ujumbe wa matumaini kutoka kwa wataalamu wa kijeshi wa Urusi kuhusu uwezo wa ndege hizo, unajumuisha na kiwango fulani cha utangazaji wa bidhaa hiyo kwa niaba ya wazalishaji.

Dmitry, kamanda wa kikosi cha droni cha Wanajeshi wa Ukraine, katika maoni yake kwa BBC, alitathmini uwezo wa ndege hizo kwa mashaka sana.

"Uwezekano wa kukamata ndege isiyo na rubani kwenye wavu ni ndege moja kati ya elfu. Wakati huo huo, kuna uwezekano mkubwa wa kupoteza droni yako mwenyewe. Unaweza kuruka kwa wiki nzima na usikamate droni yoyote,” anasema.

x

Chanzo cha picha, TELEGRAM

Maelezo ya picha, Droni ya FPV
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kulingana na mwanajeshi huyo, ufanisi wa ndege za wavu unatiwa chumvi baada ya mafanikio ya kudondosha idadi ndogo ya ndege.

"Katika wiki mbili, wamedondosha droni moja. Hii ni mbinu isiyo na ufanisi na ya kupoteza muda na rasilimali za droni."

"Unapoona ndege isiyo na rubani ya adui, kwa maoni yangu, njia sahihi zaidi ni kuruka juu yake, kushuka na kuipiga propela. Ikiwa utafanya kila kitu kwa usahihi, hutopoteza droni yako, na ndege ya adui itavunjika na kuanguka. Nilifanikiwa kuangusha ndege zisizo na rubani mbili au tatu za Urusi,” anasema Dmitry.

Mmoja wa maripota wa vita kutoka Urusi, ambaye sasa anasifu ndege za watu, alisema mwezi Novemba 2023,ndege hizo sio za kuaminika sana.

Udhaifu wa ndege za wavu ni pamoja na ukweli kwamba mafanikio yao yanategemea mambo mengi; ni lazima uione droni ya adui kwa wakati muafaka, bila ya ndege yako kuonekana, pia usubirie muda ambapo ndege ya adui imekaa mahali pamoja kwa muda mrefu ili kuikaribia na kulenge wavu.

Vita vya droni

sx

Chanzo cha picha, FACEBOOK/ALEKSANDR MELNIK

Maelezo ya picha, Hivi ndivyo mtando wa wavu unavyoonekana

Makundi yanayounga mkono Urusi yalianza kurusha ndege zisizo na rubani kote Ukraine mwaka 2014. Na mwanzo wa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, matumizi makubwa ya upelelezi haswa kwa ndege zisizo na rubani yalibadilisha kabisa mbinu za vita.

Paolo Lumiere, mchambuzi kutoka Ukraine, ana shaka kuhusu ufanisi wa ndege za wavu, hasa kwa droni zinazoweza kubadilika haraka. Lakini anakubali kwamba Warusi wanaweza kuziboresha kiufundi ili kufanya kazi vizuri zaidi.

asx

Chanzo cha picha, TELEGRAM

Ingawa kwa upande wa Ukraine, kuweka kamera katika pembe tofauti ili kutazama juu au vihisi vya kufuatilia kinachokuja kutoka juu, hayo yanaweza kusaidia dhidi ya droni za wavu.

Kunaweza hata kuwa na ulinzi wa mitambo kwa namna ya vikapu karibu na drone na propela zake, kikapu ambacho kitazuia propela kuingizwa kitu.

Pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Rashid Abdallah na kuhaririwa na Seif Abdalla