Vita vya Ukraine na Urusi: Uwepo wa droni inamaanisha hakuna eneo lililo salama

Kuna maeneo machache ambapo unaweza kuona eneo linalokaliwa na Warusi ukiwa upande wa Ukraine.
Ukingo wa magharibi wa mto Dnipro katika jiji la Kherson ni mojawapo.
Huwezi kuona wanajeshi wa Urusi kwenye ukingo mwingine wa chini wa mto wenye kinamasi, lakini unajua wapo.
Mizinga inayorushwa unapoingia kwenye jengo la ghorofa lililotelekezwa inatumika kama ukumbusho wa haraka haraka.
Hakuna jipya katika suala la urushaji wa makombora vitani. Lakini kitengo tunachokutana nacho kinahusika na moja ya uvumbuzi muhimu wa uvamizi huu: ndege zisizo na rubani au droni.
Tunapokumbatiana kando ya jengo na kujificha kwenye ngazi, tunaingizwa ndani kutoka kwenye upepo wa baridi kali hadi kwenye joto la sebule iliyo na wanajeshi.
Harufu ya sitroberi imeenea kwa juu, wanajeshi hawa wakiwa wameketi kwenye viti na mwonekano wao wa utulivu huku wakishika makopo ya kinywaji cha Monster energy.

Artem, rubani mwenye umri wa miaka 20, ghafla anakaa. Wanaambiwa Warusi wamezindua droni kutoka upande wa pili wa maji.
"Kutoka eneo tunalolijua," anaeleza Tymur, kamanda wa kikosi cha Samosud cha 11 cha Walinzi wa Kitaifa wa Ukraine.
"Lengo letu ni kuharibu marubani. Tuna viwianishi, kwa hivyo tunasafiri kwa ndege kuelekea huko sasa hivi."
Kuna angalau dazeni za ndege zisizo na rubani kwenye sakafu - zote zikiwa zimepakiwa mabomu.

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Ndege moja isiyo na rubani inatolewa nje huku Artem akiweka kifaa kinachowekwa kichwani ambacho hutoa uhalisia wa hali ilivyo kwa mvaaji.
Tunatazama kwenye runinga anapokipeperusha kuvuka mto hadi katika eneo linalokaliwa. Kutoka kwa mtazamo huu, hakuna dalili za wazi za uwepo wa maisha.
Kilomita chache baadaye, ndege isiyo na rubani ya Artem inawasili kwenye eneo la viwanda. Inapita ghala kabla ya kuelea jengo lililo karibu kama pale tulipokaa.
Hatimaye anaona antena karibu na dirisha kwenye kisima cha ngazi, na kuruka moja kwa moja ndani yake. Skrini inageuka bluu. Artem anapumua na kuondoa vifaa vyake vya sauti.
"Tulipofanya hivi mara ya kwanza ilisababisha hisia," anasema Artem. "Sasa hii imekuwa jambo la kawaida."
"Sikupata muda wa kutosha wa kucheza michezo ya kompyuta wakati wa [uvamizi wa Urusi] ulipoanza. Lakini sasa naielewa!. "Wanazindua ndege nyingine isiyo na rubani lakini skrini inabadilika kuwa samawati mara tu inapovuka mto. Warusi wamewasha mfumo wao unaofahamika kama ‘jamming’.
Kisha, ya tatu unafuata. Wakati huu inafanikiwa, na Artem anarudi kwenye jengo la ghorofa.

Anaweza kuthibitisha kuwa antena imeharibiwa. Zikiwa zimesalia dakika 10 kabla ya betri kuzima, anaenda tena kuona ni kitu gani kingine anachoweza kugundua au kuharibu.
Kitengo chake kimekuwa kikilenga barabara kuu ambayo Warusi hutumia kupeleka vifaa. Raia wamepigwa marufuku kuendesha katika eneo hilo, kwa hivyo, marubani wa ndege zisizo na rubani za Ukraine wanashambulia chochote chenye magurudumu.
Artem anaona kituo cha ukaguzi cha Urusi na kuruka kuelekea huko. Kwa bahati mbaya kwake, wanatumia bunduki kupitia mfumo wa jamming na skrini inabadilika kuwa bluu anapokaribia. Anashusha pumzi tena.
"Haijalishi ni mara ngapi tunashambulia sehemu zilezile, [Warusi] huziimarisha tena na tena," anasema Tymur. "Ni kana kwamba hawana hofu."
Huku kila ndege isiyo na rubani ikigharimu karibu $500 (£396), ni mzunguko wa mara kwa mara wa kurushwa, kutafuta na kuharibu.
Hata hivyo, matokeo yake yanaweza kuwa muhimu. Tymur anasema timu yake iliwahi kuharibu mfumo wa makombora wa ulinzi wa anga wa S-350 wenye thamani ya $136m.

Ndege zisizo na rubani inamaanisha Warusi hawawezi kujificha popote ndani ya kilomita 10 (maili sita) katika eneo la vita.
Lakini, muhimu zaidi, wavamizi wanafanya vivyo hivyo kwa Waukraine.
Chini ya uangalizi wa mara kwa mara wa ndege zisizo na rubani na mashambulizi ya adui, taratibu dalili za uwepo wa maisha zimekuwa yakipungua katika mitaa ya Kherson.
Kando na kivuko kidogo zaidi juu ya Dnipro karibu na mji wa Krynky, mashambulizi ya Ukraine hapa ni ya uchunguzi tu, na yanahitaji uvumilivu.
"Tunafanya kazi saa 24," anasema. "Tunaharibu kila aina ya ndege zisizo na rubani, haswa Shahed zilizotengenezwa na Iran."
"Viwanda vya Urusi vinafuata hali ilivyo kijeshi. Wanaongeza nguvu zao kila wakati. Kwa wakati huu, vinafanyakazi bila kukoma."
Huku misaada mingi ya kijeshi ikiwa imekwama chini ya mizozo ya kisiasa nchini Marekani na Umoja wa Ulaya, Ukraine inapaswa kwendana na hali hiyo na kuwa makini zaidi.
Kifurushi kipya cha msaada wa kijeshi cha £2.5bn kutoka Uingereza imekaribishwa hapa, na £200m kati ya hizo zikitengwa mahususi kwa ndege zisizo na rubani.
Lakini Rais Volodymyr Zelensky pia ameahidi kutengeneza ndege hizo milioni moja ndani ya mipaka ya Ukraine.
Kwenye viunga vya Kherson kwenye uwanja wenye barafu, marubani hufanya mazoezi ya safari za ndege zisizo na rubani wakiwa wamefunga chupa za plastiki chini yao, badala ya maguruneti.
Inachukua masaa 14 tu ya mafunzo ili kufuzu kama rubani wa ndege zisizo na rubani. Serikali ya Ukraine inawahimiza watu kushiriki katika mafunzo ya bure, na pia kutengeneza ndege zisizo na rubani nyumbani ili kuzituma vitani.

Inakubalika na wengi kwamba ubunifu sasa unahitajika kutokea mara moja ili kubadilisha hali katika maeneo ya vitani.
Kamanda mkuu wa Ukraine Jenerali Valerii Zaluzhnyy aliambia jarida la Economist mwezi Novemba kwamba Urusi na Ukraine "zimefikia kiwango cha teknolojia ambacho kinatuweka kwenye mkwamo".
Tatizo la Ukraine haijawahi kuwa kile ambacho imepewa na washirika, lakini itakuwa hivi hadi lini.
"Wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia, usafiri wa anga ulizinduliwa," "Na sasa tunaanza vita vya siku zijazo vya ndege zisizo na rubani, ambapo labda katika kipindi cha miongo miwili zitageuza wimbi la vita vyovyote vile," Ukraine ilisema.
Imetafsiriwa na Asha Juma.















