Kwa nini maji yanayozunguka mabaki ya meli ya Titanic bado ni hatari

Kutoweka kwa nyambizi ya Titan iliyokuwa mabaki ya meli ya Titanic imeibua maswali kuhusu hatari zinazohusiana na safari kama hizo.

Wakati fulani katika msimu wa vuli kipande kikubwa cha barafu kilipasuka kutoka kwenye barafu kusini-magharibi mwa Greenland. Kwa muda wa miezi iliyofuata, ilielea polepole kuelekea kusini, ikiyeyuka polepole kufuata mikondo ya bahari na upepo.

Kisha, usiku wa tarehe 14 Aprili 1912, barafu yenye urefu wa mita 125 (410ft) - yote iliyosalia ya kipande cha barafu kinachokadiriwa kuwa 500m (1,640ft) kilichoacha fjord huko Greenland mwaka uliopita - kiligongana na meli ya abiria ya RMS Titanic ilipokuwa ikifanya safari yake ya kwanza kutoka Southampton nchini Uingereza hadi New York, Marekani.

Ndani ya muda wa chini ya saa tatu meli hiyo ilikuwa imezama, na kuwaangamiza zaidi ya abiria 1,500 na wafanyakazi waliokuwa wameiabiri.

Mabaki ya meli hiyo sasa iko karibu 3.8km (12,500ft) chini ya maji karibu maili 400 (640km) kusini mashariki mwa pwani ya Newfoundland.

Milima ya barafu bado inahatarisha usafiri wa meli - mwaka wa 2019 milima ya barafu 1,515 ilisogezwa kusini hadi kwenye njia za meli zinazovuka Atlantiki wakati wa miezi ya Machi hadi Agosti. Lakini sehemu ilipo mabaki ya meli ya Titanic ina hatari zake, kumaanisha kwamba kutembelea eneo la ajali la meli hiyo maarufu zaidi ya duniani kunaleta changamoto kubwa.

Baada ya kutoweka kwa nyambizi ya kitalii iliyokuwa na watu wa watu watano wanaolipa kutembelea eneo la ajali ya Titanic, BBC inaangalia jinsi eneo hili la sakafu ya bahari lilivyo.

Kuelekeza chombo kwenye kina kirefu

Bahari ya kina kirefu ni giza. Mwangaza wa jua hufyonzwa haraka sana na maji na hauwezi kupenya ndani zaidi ya mita 1,000 (futi 3,300) kutoka juu ya maji. Ukipita sehemu hiyo, bahari iko katika giza la milele. Titanic iko ndani ya eneo linalojulikana kama "midnight zone" kwa sababu hiyo.

Safari za awali kwenye eneo la ajali zimeelezea kushuka kwa zaidi ya saa mbili kupitia giza kuu kabla ya sakafu ya bahari kuonekana ghafla chini ya taa za chini ya nyambizi.

Ramani za kina za mabaki ya ajali ya Titanic zilizounganishwa kwa miongo kadhaa ya uchanganuzi wa ubora wa hali ya juu, hata hivyo, zinaweza kutoa vidokezo ya kadiri vitu vitakavyoonekana. Sonar pia huruhusu wafanyakazi kugundua vipengele na vitu zaidi ya mwanga mdogo unaoangaziwa chini ya maji.

Manahodha wa nyambizi wanaoweza kuzama chini ya maji pia wanategemea mbinu inayojulikana kama (accelerometers and gyroscopes) urambazaji wa angavu , kwa kutumia mfumo wa viongeza kasi na gyroscopes kufuatilia nafasi na mwelekeo wao kuhusiana na mahali pa kuanzia na kasi inayojulikana.

Unaweza pia kusoma

Nyambizi ya OceanGate hubeba mfumo wa hali ya juu unaosaidia usongezaji unaojitosheleza ambao unachanganya na kitambuzi cha sauti kinachojulikana kama Doppler Velocity Log ili kukadiria kina na kasi ya gari inayohusiana na sakafu ya bahari.

Hata hivyo, abiria waliokuwa kwenye safari za awali za Titanic wakiwa na OceanGate wameeleza jinsi inavyokuwa vigumu kupata njia wanapofika kwenye sakafu ya bahari.

Mike Reiss, mwandishi wa vichekesho vya televisheni ambaye alifanya kazi kwenye The Simpsons na kushiriki katika safari na OceanGate kwenye Titanic mwaka jana, aliiambia BBC: "Unapofika chini, haujui mahali ulipo. Ilibidi tupepese macho kama watu wasio na uwezo wa kuona chini ya bahari nikijiambia Titanic iko mahali fulani pale, lakini ni giza tupu hivi kwamba jambo kubwa zaidi chini ya bahari lilikuwa umbali wa yadi 500 (futi 1,500) na tulitumia dakika 90 kuitafuta."

Kuongezeka kwa shinikizo la maji

Kadiri chombo kinavyosafiri ndani ya bahari, ndivyo shinikizo la maji linaloizunguka hukua. Kwenye bahari ya mita 3,800 (futi 12,500) chini ya maji, Titanic na kila kitu kinachozunguka hustahimili shinikizo la karibu 40MPa, ambalo ni la ukubwa mara 390 kuliko zile zilizo juu ya bahari.

"Ili kupata taswira kamili, hiyo ni takriban mara 200 ya shinikizo la kile kilicho kwenye tairi la gari," Robert Blasiak, mtafiti wa bahari katika Kituo cha Ustahimilivu cha Stockholm katika Chuo Kikuu cha Stockholm, aliambia kipindi cha Leo cha BBC Radio 4. "Ndio maana unahitaji chombo cha chini ya maji ambacho kina kuta nene sana."

Kuta za nyuzi za kaboni-na-titani za tangi ya chini ya maji ya Titan zimeundwa ili kuipa kina cha juu cha kufanya kazi cha 4,000m (ft 13,123).

Mawimbi ya chini ya bahari

Bahari ya kina kirefu pia huchafuliwa na mawimbi ya chini ya maji. Ingawa kwa kawaida hayana nguvu kama yale yanayopatikana juu ya maji, bado yanaweza kuongeza mwendo wa maji kwa kiasi kikubwa.

Yanaweza kuelekezwa na upepo kwenye eneo linaloathiri safu ya maji chini, mawimbi ya kina kirefu au tofauti katika msongamano wa maji unaosababishwa na joto na chumvi, inayojulikana kama mikondo ya thermohaline.

Matukio adimu yanayojulikana kama dhoruba za benthic - ambazo kwa kawaida huhusiana na eddies juu ya maji- pia yanaweza kusababisha mawimbi yenye nguvu na yasio ya kawaida ambayo yanaweza kupoteza chombo kwenye bahari.

Kinachojulikan akuhusu mawimbi ya chini ya maji yanayozunguka meli ya Titanic, ambayo imegawanyika katika sehemu mbili kuu baada ya upinde na usukani kugawanyika ilipozama, kilitokana na utafiti wa kuchunguza mwelekeo katika sehemu ya chini ya bahari na kusogea eneo linalozunguka mabaki ya meli hiyo.

Sehemu ya mabaki ya Titanic inasadikiwa kuwa karibu na sehemu ya chini ya bahari iliyoathiriwa na mkondo wa maji baridi, yanayotiririka kuelekea kusini yanayojulikana kama Mkondo wa Magharibi wa Mpaka wa Magharibi.

Mtiririko wa "mkondo huu wa chini" huunda matuta yanayohama, mawimbi na mifumo yenye umbo la utepe kwenye mashapo na matope kando ya sakafu ya bahari ambayo yamewapa wanasayansi maarifa juu ya nguvu zake. Miundo mingi ambayo wameona chini ya bahari inahusishwa na mawimbi dhaifu hadi wastani.

Baadhi ya wataalamu wanatarajia mawimbi ya chini ya maji yataendelea kusukuma pole pole meli ya Titanic na hatimaye mabaki yake yatazikwa kwenye mashapo.

Gerhard Seiffert, mwanaakiolojia wa bahari ya kina kirefu ambaye hivi majuzi aliongoza msafara wa kukagua mabaki ya meli ya Titanic, aliiambia BBC kwamba haamini kwamba mkondo wa maji katika eneo hilo ilikuwa na nguvu ya kiasi cha kusababisha mawimbi yachini ya maji.

"Sijui kama kuna mawimbi yanayoweza kuwa tishio kwa chombo chochote kinachosafiri katika eneo la Titanic," anasema. "Mawimbi.. katika muktadha wa mradi wetu wa uchoraji ramani, iliwakilisha changamoto kwa usahihi wa uchoraji ramani, sio hatari kwa usalama."

Hali ya mabaki ya meli ya Titanic

Baada ya zaidi ya miaka 100 chini ya bahari, Titanic imeshuka hatua kwa hatua. Athari ya awali ya sehemu kuu mbili za chombo kilipogongana na sakafu ya bahari, ilijipinda na kupoteza sehemu kubwa za mabaki.

Baada ya muda, vijidudu vinavyolisha chuma vya meli vimeunda "rusticles" yenye umbo la icicle na vimefanya mabaki ya meli hiyo kuzorota. Ukweli ni kwamba, wanasayansi wanakadiria kwamba shughuli ya juu ya bakteria kwenye sehemu ya nyuma ya meli - hasa kutokana na kiwango kikubwa cha uharibifu - inasababisha baadhi ya mabaki ya miaka 40 kuzorota kwa kasi zaidi kuliko sehemu ya upinde.

Mtiririko wa tope

Ingawa ni jambo lisilowezekana, mtiririko wa ghafla wa mchanga kando ya sakafu ya bahari umechangia kuharibu na hata kubeba vitu vilivyotengenezwa na binadamu kwenye sakafu ya bahari hapo awali.

Tukio lengine kubwa - ni pamoja na lile lililokata nyaya za kupita Atlantiki kwenye pwani ya Newfoundland mnamo 1929 - lilichochewa na matukio ya mitetemeko kama vile matetemeko ya ardhi. Kuna ongezeko la hatari ya matukio haya, ingawa hakuna dalili yoyote kwamba tukio kama hili huenda lilisababisha kutoweka kwa nyambizi ya Titan.

Kwa miaka mingi, watafiti wamegundua dalili kwamba sehemu ya chini ya bahari karibu na mabaki ya Titanic imekumbwa na maporomoko makubwa ya ardhi chini ya maji siku za nyuma.

Kiasi kikubwa cha tope kinaonekana kuteremka kwenye mteremko wa bara kutoka Newfoundland kuunda kile wanasayansi wanakiita "ukanda usio na utulivu".

Wanakadiria tukio la mwisho kati ya haya "hatari" lilitokea maelfu ya miaka iliyopita.