'Siwezi kuondoka Afrika Kusini, nina mtoto hapa'

Mkuu wa kampuni ya programu za kompyuta Stanford Mogotsi anasema bado ataishi Afrika Kusini, licha ya changamoto za kuendesha kampuni ndogo ya teknolojia ya mawasiliano nchini humo.

 "Ni nyumbani kwangu, nina mtoto hapa, nina familia hapa," anasema mkuu huyo mwenye umri wa miaka 46.

 Bw Mogotsi ni mmiliki mwenza wa kampuni ya kutengeneza programu za kompyuta yenye makao yake mjini Johannesburg -Nane Solutions na rafiki yake na mshirika wa kibiashara Kabelo Mashisi, 45.

 Wote wameanzisa mbali tangu walipokuwa wakikua pamoja katika miji ya Afrika Kusini wakatui wa ubaguzi wa rangi.

 Kila mmoja wao alisomea masomo ya sayansi ya kopmpyuta, na walifanya kazi katika makampuni ya IT, kabla ya kuanzisha kampuni yao , Nane mwaka 2006.

Kazi yao ya awali ilikuwa ni ya kutoa ushauri – kuyashauri makampuni kama vile MTN, kampuni kubwa zaidi ya mtandao wa mawasiliano ya simu za mkononi , na kampuni inayomilikiwa na taifa ya umeme-Eskom.

 Lakini walibaini kuwa kazi ya ushauri ilikuwa inasumbua kwasababu walitaka kutengeneza programu za kumpyuta kuanzia mwanzo, kuliko kushauri tu.

 Mafanikio yao ya kwanza makubwa yalikuwa ni kubuni mfumo wa Shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA wa kuweza kuwamudumia wafanyakazi wa kujitolea katika Kombe l Dunia la 2010 , lililofanyika nchini Afrika Kusini.

 Halafu katika mwaka 2017 walibuni programu ambayo ilisaidia kampuni ya kutengeneza pombe ya Heineken kuboresha mfumo wake wa usafirishaji nchini humo. Mradi mwingine mkubwa ulikuwa ni wa kutengeneza programu (App) kwa ajili ya huduma ya video ya simu unaojulikana kama Talk360.

Lakini mafanikio hayo hayakupatikana kirahisi. Nane ambalo ni neneo la Kiswahili, linalomaanisha namabari nane lilichaguliwa kwasababu kampuni hiyo ilikuwa na waasisi wanane.

Hatahivyo, kuhama kutoka kazi ya ushauri na kuanza biashara ya kutengeneza programu ya kompyuta , na halafu athari za sheria kali za ‘’lockdown’’ za Covid-19 zilizowekwa na Afrika Kusini viliwafanya wote isipokuwa Bw Mogotsi na Bw Mashisi kujiondoa kwenye biashara hiyo.

"Ni vigumu sana kupata kazi wakati una kampuni ndogo," anasema Bw Mogotsi. "Ni lazima tushindane na makampuni ya kimataifa, na watu wanaoweza kuwa wateja huwa wanataka kwenda kwenye makampuni haya ambayo yalifanyiwa majaribio na makubwa ya teknolojia ya mawasiliano -IT2, hususan wakati uchumi wa Afrika Kusini ni wa mashaka."

Huku Bw Mogotsi na Bw Mashisi wanabaki Afrika Kusini, Profesa Coulter anasema kwamba tatizo kubwa linaloendelea nchini Afrika Kusini ni kuondoka kwa watu wenye ujuzi wa IT – watu wanatafuta kazi katika nchi za kigeni.

 "Wanafunzi wetu wengi sana sasa wanaondoka kwenda Ulaya, Marekani, Asia, na wanafanya vyema sana maishani mwao, tunajivunia sana maisha yao," anasema.

 "Na kama sehemu ya watu wenye ujuzi wanaokwenda mbali na Afrika Kusini wanapata fursa ya haraka ya kupata ajira sawa na mawakili na madaktari ."

 Matokeo yake hawa vijana wte wenye taaluma ya teknolojia ya Mawasiliano- IT wanapata kazi ng’ambo, Profesa anasema kwamba makampuni katika sekta hii nchini Afrika Kusini sasa yanahangaika kujaza nafasi zao. 

Bw Mashisi anasema kuwa "kimshahara hatuwezi kushindana" na ule unaotolewa na makampuni makubwa ya ng' ambo.

Licha ya kuondoka kwa wasomi wengi wa IT nchini Afrika Kusini bado kuna makampuni yenye mafanikio yanayoanza ambayo yanatengeneza bidhaa maarufu.

 Mfano ni programu hii ya kompyuta inayofahamika kama EskomSePush, ambayo iliwatahadharisha watumiaji kote nchini Afrika Kusini ni lini watarajie kukatwa kwa umeme.

 EskomSePush ni kampuni iliyoanzishwa na Dan Wells (35) pamoja na Herman Maritz, waliozindua programu hiyo mwaka 2015 na kuiendesha kutoka katika nyumba zao mjini Cape Town.

Inakusanya na kupangilia mipangilio migumu kutoka kwa Eskom na serikali za mitaa kote nchini Afrika Kusini.

Halafu taarifa hutumwa kwa watumiaji kuwafahamisha ni lini umeme utapatikana katika maeneo yao na kwa muda gani.

Bw Wells anasema kwamba katika kipindi cha miezi sita ya kuanzishwa kwa programu hiyo, watu 250,000 wamekwisha ipakua, "jambo ambalo lilikuwa ni la kushangaza wakati huo".

Anaongeza kuwa leo programu iki "katika siku milioni saba, na takriban watu milioni hubofya kupata taarifa mara moja".

 Kama kuna kitu kinachowaunganisha Waafrika Kusini ni mapenzi ya mchezo, huku Kriketi ukiwa ni mchezo wa tatu unaopendwa zaidi nchini humo.

Programu yake inaweza kutambua mara moja ni magongo mangapi yamepigwa na kila mchezaji kutokana na kurekodi mechi ya majaribio au mechi nyingine.

 Hii inamaanisha kwamba mkufunzi wa kriketi anaweza kucheza video kadhaa za picha fulani, bila kulazimika kutazama picha zote kufahamu uwezo wa mchezaji.

 Hii itasaidia timu na mkufunzi kutathmini mchezo na ni wapi marekebisho yanaweza kufanyika.

 Wakati programu yake bado iko katika awamu ya utafiti, Bw Moodley anasema kwamba kutokana na kwamba kuna wawekezaji wanaofaa na washikadau ataangalia jinsi yay a kujenga programy hiyo ya kibiashara

 Lakini wakati huo huo lengo lake ni kusaidia kizazi kijacho cha Afrika Kusini cha wachezaji wa kriketi . "Ninataka kuifanya iwe ya hapa na kujaribu kuisaidia timu yetu ," anasema.